“Mshawishi mpenzi, mshawishi yule bwege aibe pesa mingi kwenye Account ya Serikali ili na sie wenye bahati tukayajenge maisha.🧎♂️” Max alimwambia Rose wakiwa wameketi juu ya kitanda kizuri jamani, hakipo Tanzania kitanda hicho ni kitanda kikubwa cha kuvutia, chumba walicho azima ni chumba cha fahari sijapata kuona mie.🌷🌺
“Ondoa hofu na wasiwasi Love wacha niendelee kulikoreza penzi la kinafki kwake, wacha niendelee kumshawishi amuache mkewe, nitamsonga hadi asongeke na kwa uzuri nilionao lazima nimuingize mtegoni.” Rose alimpiga mabusu Max mdomoni, Max akayapokea yale mabusu kwa tamaa.“Ukihitaji mawazo juu ya mpango wako usisite kunishirikisha, Love ninakupenda. Tukifanikiwa kuzipata hizo billioni mbili💵💲 lazima tuhame nchi ya Tanzania.” ✈️🛩️Max alimshawishi Rose.
“Mbona tutatanua,💃🕺 mbona tutazichezea hizo pesa🤣, mbona tutaringa, mpenzi kitu kikubwa ni kupendana, tusiachane Baby.” Rose alijifanya kudeka kisha akaendelea kunena.
“Yule boya ninamjua vizuri sana, nikimshawishi kidogo tu na kumpiga busu la shavuni tayari Keisha lainika kama ute ute wa yai🥚🐣🍳, hachelewi kunitimizia haja zangu atafanya tu, atafanya kama nitakavyo, wiki mbili zijazo mara baada ya Chirstmass akirudi kutoka Namibia mambo yataiva.” Rose alitia nanga.
“Nakutegemea mpenzi, 💝💕I love you so much.” Max alitia neno akampa ulimi 💏💋wake Rose muda kidogo wakawa hoi bin taabani, hamu ya kuendelea kuvunja amri ya Sita ya Mwenyezi Mungu iliwazidia nao hawakusita kuizidisha.😍
BI. MKUBWA ANAFUKUZWA👵
Likizo ya siku tano kuisha Waziri Beni pamoja na Kampani yake walifanya kurudi Nyumbani Tanzania. Wameponda raha hadi kuchoka, wamechezea pesa watakavyo bado ile mifuko ya wapambe inahitaji na pia inatamani pesa kutoka kwenye mikono ya waziri Beni, hawachoki kumbembeleza. Hawana mashauri mazuri tena yanayofaa, hawana elimu yoyote ile juu ya masuala ya kisiasa au matumizi ya pesa. Si wamemuona Waziri Beni ana pesa zake na tena wamemuona Waziri Beni anajua kutoa, anatoa bila kinyong’onyiro (kinyongo) wacha wamkombe, wacha wamchune, wacha wamlie hadi abakie mifupa.
Basi nakwambieni hapo nyumbani kwa Waziri Beni hapakuwa na amani🥷💪, kutwa kuchwa Waziri Beni anamchukia mkewe, anamdharau na kumshusha thamani yake. Yote haya ni matokeo ya mipango anayoipanga Secretary Rose. Secretary wake ameanza kumpika Waziri Beni ili amuache mkewe, ikiwezekana ampe taraka isiyo na sababu.
“Mpe taraka yake Mpenzi, Mfukuze huyo yanini utembee na wazee wakati warembo Mashallah tupo sie.” Rose alideka Ofisini kwa Waziri Beni.
“Wazo lako ninalifanyia kazi mpenzi, hapa natafuta kasababu ka kummegua yule Bi. Kizee pale Nyumbani.” Waziri Beni aliongea.
“Sababu 😠……………. Mbona sababu zipo nyingi tu mpenzi, moja ya sababu wewe mwambie hivi nimekuchoka wewe ni Mzee na mimi bado ni kijana ninahitaji kuishi na kijana wa rika langu.” Rose aliongea
“Hivi!! Eti eh!” Waziri aliongea kwa mshangao.😲🙀
“That’s all, usiogope wewe ni mwanaume uliyekamilika na sifa ya mwanaume aliyekamilika haogopi.🏋️♀️” Rose aliongea tena.
.
“Ni hivi Rose, mie sipingani na mawazo ya moyo wako unajua yule ni mke wangu wa ndoa na pia nimedumu naye ndoani kwa takribani miaka 32, mpaka sasa tumejaliwa kuwa na watoto watatu, nikimfukuza kama Umbwa 🐕🦺🦴 watoto hawawezi kunielewa.” Waziri Beni alijitetea.
“Ni hivi Rose, mie sipingani na mawazo ya moyo wako unajua yule ni mke wangu wa ndoa na pia nimedumu naye ndoani kwa takribani miaka 32, mpaka sasa tumejaliwa kuwa na watoto watatu, nikimfukuza kama Umbwa 🐕🦺🦴 watoto hawawezi kunielewa.” Waziri Beni alijitetea.
“Kwahiyo unampenda sana mkeo kuliko mimi eeh!” 🥴 Rose alijifanya kuonesha hasira.
“Simaanishi hivyo Mpenzi, ninakupenda sana wewe😘 kuliko yeye, wewe ni Malkia 👸kwangu yule ni Bi.kizee tu, eti mpenzi umeona wapi na wapi Bi. Kizee afanane na Malaika?👼” Rose aliposikia maneno haya akasuuzika mtima wake na kuingiwa na furaha.
“Sasa mpango huko hivi mpenzi nitajaribu kumtenga na kumrudisha kijijini🛖 kwao akae huko kwa muda mrefu, ili mie na wewe tuponde raha na starehe, nakwambieni kwa muda huo mrefu ni lazima kikongwe yule anisahau ili mie na wewe tuponde raha na starehe au unasemaje Malaika wangu?” Waziri Beni aliongea kizembe zembe.
“Mmh! Mie nataka umuache kabisa mpenzi.” Rose alijifanya kununa na kumchukia Bi. Mkubwa, mke wa Waziri Beni.
“Sijakataa nitamuacha tu, jaribu kuvumilia pole pole ndio mwendo.” Beni aliongea.
(Itaendelea SEHEMU ya 5
No comments:
Post a Comment