Thursday, September 19, 2024

LETS TAlK ABOUT THIS LOVE

 PENZI LENYE MAPENZI.




Mkuki ndani ya moyo penzi lenye mapenzi,

Ninaweka kimbilio, roho yangu Ibarizi,

Hapo ndipo shikilio,makazi mema malezi,

 

Penzi lenye mapenzi, makazi mema makuzi,

Huduma yenye malezi,malezi mema makuzi,

Makuzi ya mfinyazi, mfinyinzi ni laazizi,

 




Hapo ndipo shikilio, meoteana mizizi

Hapo kuna timizio, la haja ya mapenzi,

Tena kuna matakio, ya heri zenye faradhi,

Mkuki ndani ya moyo,penzi lenye mapenzi,

Ndani kuna ufunuo, ufunuo wa mapenzi,

Hapo tena kuna tuo, la mema yenye mapenzi,

 



Ndani kuna ufunuo, wa mema yenye mapenzi,

Huo ndio ufunguo, ufunguo wa matatizi,

Hima moyo wangu tua, ulipate hilo penzi

 

Ndani kuna ufunuo,wa mema yenye mapenzi,

Huo ndio ufunguo, ufunguo wa matatizi,

Hima moyo wangu tua, ulipate hilo penzi.

 



Hima moyo wangu tua, ulipate hilo penzi,

Penzi lisilo bagua, penzi lisilo chagua,

Penzi la kwangu tua, penzi ua kunjua.

 

Penzi lisilo bagua, penzi lisilochagua,

Penzi nililoamua, likifa talifufua,

Penzi limejifunua, kwangu lanisimua,

 



Penzi hili haliumi, lanipa raha ndani,

Penzi halichomi, lanipa raha usoni,

Tena penzi halisemi tajanitupa jangwani

 



No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...