Sunday, September 15, 2024

WAMEZIDI sehemu ya Saba (Mwisho)

 

Hadithi

 

WAMEZIDI



Tulipoishia sehemu ya sita


        'Mmmh! Tungoje, labda ndio hivyo tena nitauziwa Mbuzi kwenye gunia.” Max aliwaza, anasubiri hicho kitoto kitakacho zaliwa, moja kwa moja kikiisha kuzaliwa ni lazima kipimwe DNA ili kuangalia uthibitisho iwapo hicho kitoto ni cha kwake Max au la! Maana hapa  Mjini ni shidaa!  Utafiti umefanyika  watafiti wanasema asilimia 44 ya wanawake wenye watoto watoto hao sio watoto waliozaa na waume zao, bali watoto hao ni kutokana na Michepuko, mahawara na wapenda starehe za haraka haraka. Max alitia Shaka


Sehemu ya 7 (Mwisho)

                ########################

          “Kwa hiyo Mama unataka tumpe Mumeo hizo fedha za Bandia si ndivyo eti eeh!?” Aisha Mtumishi wa Benki kuu ya Tanzaia alimuuliza mke wa Waziri. Bi. Mkubwa👵 amemuita Aisha amempa Somo japokuwa Aisha amekuwa mgumu kuafikiana na  yule Mwanamama.

       “Kitu kama hicho, Aisha we huoni kuwa Mume wangu ni FISADI anataka kuhujumu uchumi, anataka kuiingiza Nchi katika hasara ya mabillioni ya shillingi kutwa kuchwa yeye na Safari, Safari na yeye, mara CHINA, NORWAY, USA,  AUSTRALIA, SOUTH AFRIKA, INDIA na kwengine kwingi anakwenda huko kuomba mikopo  ambayo haisaiidi Nchi na Serikali, Mikopo hiyo inazidi kulibebesha taifa mizigo na hasara.” Mke wa Waziri aliongea.

              “Ni aibu kwa nchi yetu nchi imekuwa ni nchi ya maomba omba wakati huo huo Viongozi wanatia fora katika uombaji na utawanyaji wa pesa za mikopo. Wengi wa hawa viongozi wetu wanazichezea pesa kwa mambo ya Starehe, vimada na michepuko. Sikiliza Aisha nimefanya juu chini kuzitengeneza Billion mbili ambazo sio pesa halali bali ni pesa za Bandia.” Bi. Mkubwa aliongea maneno yaliyomshitua na kumshangaza Aisha.

              “Mama kwa kweli hili jambo mie kwangu ni mzigo na pia siliwezi kwa sababu ni kosa kisheria kwa Mtumishi wa Benki yoyote ile ndani na nje ya Nchi ya Tanzaniaa kuwapa wateja wake Pesa za Bandia, baya zaidi Mumeo ni Waziri wa fedha labda hizo fedha anataka kufanyia shuhuli za kiuchumi nafikiri itakuwa aibu kwa sisi iwapo tukigundulika kuwa  tunatoa pesa za bandia. Tena hizo pesa zijaposambaa ndani ya nchi, uchunguzi utafanywa na baada ya uchunguzi huo kufanywa mie nitatiwa hatiani,” Aisha alimpa somo Bi. Mkubwa.

           “Sikiliza  binti unenayo sio mzigo kati ya mimi na wewe, bali unenayo lazima yawe mzigo kwa wapambe wamtiao nuksi mume wangu, ukikubali kunisaidia nitawashirikisha Polisi nitawaomba watulinde mimi na wewe, lengo letu ni kuwatia hatiani hawa wahujumu uchumi. Ni aibu kuona au kusikia kuwa nchi nzuri kama Tanzania ina kila kitu cha thamani na kila kitu chenye hadhi ya juu ajabu bado tunashuhudia viongozi wakiomba omba nje ya Nchi. Haipendezi tena haifai hata kidogo.” Bi.Mkubwa aliongea.

         “Siasa za kuomba omba misaada zimepitwa na wakati, lazima tujitegemee sisi wenyewe kuelekea katika uchumi mzuri wa Viwanda.” Bi. Mkubwa aliongeza neno.

            “Kama nilivyokueleza lengo litakuwa ni kuwatia hatiani wabaya wetu, mimi na wewe tuziokoe pesa za Serikali Pesa ambazo zikitumika vizuri zitaweza kuwanufaisha Watanzania wanaoishi maisha ya chini, wajengewe barabara, wawekewe miundo mbinu ya maji safi na salama, wapelekewe umeme pamoja na mahitaji mengine ya kijamii.” Aliongea mke wa waziri maneno ambayo yaliingia moja kwa moja ndani ya kichwa cha yule binti. Japo kwa hofu na kwa wasi wasi mwingi alikubali yale maneno aliyoambiwa na mke wa waziri.

                    #####################

               Siku ya siku waziri Beni alienda Benki, akajichotea yale Mabillioni ya Pesa yamejaa Kweli kweli, yamejaa kwenye mifuko ya plastick, yamejaa na kushindiliwa hadi kwa juu na baada ya matimizo ya ile haja Waziri Beni aliyapeleka moja kwa moja nyumbani kwake akampatia hawara wake Rose, akampatia kwa furaha kama Mwendawazimu. Rose alizipokea zile pesa alizopewa na Waziri Beni tena asilolojua kama usiku wa kiza’ akazitwaa zile pesa alizomwomba Waziri Beni akazipeleka Benki kwa madai kuwa atazifanyia shuhuli za kimaendeleo. Na hata hizo shuhuli zenyewe bado hakuzitaja zaidi ya maneno ya mahaba na mabembelezo makuu.

###################

           Jambo la kwanza mara baada ya Max na Rose kuzikamata zile Pesa walipanga kutoroka nchi, Lazima waende Manchester City ili wakafurahie maisha lakini Kabla hawajatoroka walihitaji kuziweka zile pesa Benk kwenye Account mpya ili wakifika huko Manchester wazihamishie kwenye Account nyingine mpya. Basi wakaenda Benki kuu ya Tanzania wakamwita Aisha, hawamjui wala hawajui tena hawajuani, wakamwomba awahifadhie zile pesa kwenye Account yao ambayo ni Account ya siri mno tena wameifungua muda si mrefu.

            Aisha alizipokea zile pesa kwa lengo la kuziweka ndani ya ile Account ya hawa wawili waliomwomba awahifadhie, mastaajabiko zile pesa Aisha alizigundua tena aligundua kuwa ni pesa za Bandia, akapiga simu Polisi Polisi wakaja wakawatia ndani wale waja wawili wamejaa hofu na kushangaa wasitake kuamini kuwa ati zile pesa ni pesa bandia.

                ##########################
            Zilipita siku mbili tatu mara baada ya Max na Rose kutiwa Lokapu, habari za kuushitua ulimwengu zilisikika Radioni, Raisi wa Tanzania akatangaza kujiuzuru kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha na mipango ya nchi. Lo! Bi. Mkubwa, mke wa waziri Beni alimanusura adondoke chini na kuzirai alipoambiwa kuwa mumewe amevuliwa cheo, cheo kikuu, cheo kitamuu, cheo chenye Fedha.

          Beni tayari alikwisha amriwa aachie ngazi ili kuupisha uchunguzi ulioendelea kufanyika juu ya tuhuma zake za kupotea kwa pesa nyingi za taifa na Serikali, Pesa ambazo hazikujulikana ni wapi zilipopotelea, lo! Masikini Beni hakuamini kama ipo siku moja atashuhuudia Polisi wakimkamata na kumtia pingu mikononi. Wakamtupia Rumande huko nako anasubiri uchunguzi uendelee kufanyika ni wapi Pesa mingi za Serikali amezichimbia?

                Max na Rose nao wapo Jela wanasubiri kupelekwa Mahakamani ili wakajibu shitaka la kutakatisha pesa, kuirubuni Benki kwa kuipatia Pesa Bandia. Wameshituka sana mara baada ya kusikia ati mpambe wao na mtu wao wa karibu Waziri Beni ametumbuliwa.Oh! Sijui watamsingizia nani? Aliyewapa hizo Fedha maana ishakuwa kesi juu ya kesi wamechanganyikiwa sana wanakuna vichwa vyao wasijue ae wala Bae. Lo! Mmh! Imbombo jilipo (Kazi ipo) imbombo ngafu (kazi nzito kweli kweli.)

             Mimi, Viva, Dino na Joe wamelikimbia Jiji, wamekwenda Vijijini mara baada ya kusikia tetesi za yaliyowakuta wapendwa wao Max, Rose na Waziri Beni kesi ya kupotea kwa pesa Mingi za Serikali sio jambo dogo. Mmh! Wameona wacha wawachinjie Rose, Max na Beni juu ya Bahari. 

Wamepanda Majahazi hao wametoka baru kama kifuu kinachowaka moto, kwa sasa wamejificha huko Zanzibar, wanaogopa mkono wa Serikali. Wakati wa raha waliburudika pamoja na Waziri Beni lakini wakati huu wa dhiki wameona hawana jinsi wacha wapae juu ya nyungo watoweke na kukimbilia Zenji.

           Ishakuwa hivyo tena mapigo ya moyo yanamwenda kasi na kusi Bi. Mkubwa mkewe Beni, anampenda sana mumewe hajui sijui itakuwaje hatima ya baba watoto wake? Sijui!? Mmh! walisema wahenga akenda juu Kipungu hafiki Mbinguni, Mpanda ngazi hushuka, aliye juu mgoje chini, yamemkuta Waziri Beni.

Mwisho.








No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...