Saturday, September 14, 2024

WAMEZIDI sehemu ya Tano (5)

 


Urudi kijijini mama watoto ninataka uende ukapumzike huko hadi pale nitakapokuita.” Waziri Beni alimshitua mkewe.

            “Eeh! Mume wangu kulikoni mbona wanishitua kwa kauli hizo!?” Bi. Mkubwa alishangazwa na uamuzi wa Mumewe.
           “Mimi ndio mumeo, mume akisema amesema kwa hiyo wewe kazi yako ni kutekeleza tu.” Waziri Beni alitoa neno kwa ukali.
            “Lakini mume wangu …………”
             “Lakini nini!?” Waziri Beni alimkatisha mkewe kunena.
              “Maisha ya kijijini yalivyo magumu ni heri na afadhari ya mjini. Kwanini unataka ukanitupe huko kusiko na heri wala tija? Niende kwenye hali ngumu ya maisha, Kijijini                                                                                                                                                                                                                                                                                                    hakuna maji , hakuna umeme, hakuna Hosptali wala barabara nzuri kama za huku kwetu Mjini.”
         “Wewe mwanamke hivi una matatizo gani? Kwani kitendo cha wewe kwenda Kijijini ni lazima ufuate barabara nzuri za kwenda Mbinguni? Hospitali, maji na umeme. Wacha hao wanaoteseka huko Kijijini waendelee kuteseka.” Beni alimjibu mkewe kwa dharau.
          “Mume wangu usiseme hivyo ujuwe wewe ni waziri na waziri ni kichwa cha Serikali ulipaswa huwe mstari wa mbele kuishawishi Serikali ikupatie fedha ukayaboreshe maisha ya watu wa Kijijini, kuwadharau hakutoshi.” Mke wa waziri alinena.
         “Hilo nalo halikuhusu, angalia lile linalokuhusu nimesema rudi kijijini hadi pale nitakapokuita au nitakapokuja kukuchukua.” Beni alitoa msimamo wake mkewe hakuwa mbishi japokuwa moyo wake haukuafikiana na mawazo ya mumewe. Je, aondoke au je, asiondoke? Uamuzi huo anao yeye binafsi anampenda sana mumewe lakini kwa mtindo huu wa kulazimishwa aondoke pale nyumbani alivunjika moyo, hatimaye aliona wacha afanye lolote lile analoweza kufanya, aondoke, hana jinsi, mume wake ni shidaa!
######################

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...