Friday, September 13, 2024

KUKU WA KIZUNGU...sehemu ya pili

 



Sehemu ya pili


Usiku uliingia na kumkuta Islama yupo juu ya sofa anatizama Televisheni kuna tamthiliya ya kifilipino inaitwa THE PROMISE ametokea kuipenda asikwambie mtu, alikua akiifuatilia sana kupitia Televisheni za huko kwao England, anaifuatilia hadi huku  Afrika, kwani asipoiona kwenye televisheni basi ataipata kupitia Computer laptop yake pale tu ajapojiunga na BANDO la Internent. Siku iliyofuata Islama alidamka kivivu vivu, kukosha vyombo, kupuguta deki , kufua viwalo vyake vichache pamoja na kujifurahisha kwa mazoezi ya viungo vyake vya mwili.      

   “ Upweke” Islama aliwaza akiwa anafua viwalo vyake vichache       

   “ Upweke unaudhi, upweke unachukiza, upweke unakondesha na matokeo yake upweke unaweza kuua,” Islama aliwaza tena, ndani ya siku mbili tatu hizi za kuwepo Afrika alihitaji kuwa na mtu wa karibu sababu huko kwao England anaye BOY lakini boy wake hakutaka kumuunga mkono waje pamoja Afrika. Sio kwamba tatizo la boy wake kukataa kuja Afrika ni nauri, hapana nauri ipo tena ipo pesa mingi labda tuseme kwa kifupi boy wake hakupenda kuja kuinjoy life huku AFRIKA YA MASHARIKI.

Islama ni binti mwenye umri wa miaka 22, kwake mapenzi sio mageni, lakini upweke? Mmh! Upweke asingeliweza kuustahimiri, kwa sababu upweke ukondesha na kuua.  Akapata wazo, lazima awe na Boy wa kupiga naye story mbili tatu,  wapoteze muda na kujifurahisha, wajizoeze na kuzoea mengi yahusuyo maisha yao.        

    “Sijui nifanye nini ili kupigana na huu upweke wa siku mbili tatu ndani ya Afrika? sijauzoea.”Islama akaacha kufua viwalo vyake naye akajishika tama, mawazo kibao yakiutibua mtima wake siku mbili tatu za kuwepo ndani ya ile nyumba aliyoazima alijiona kama ameketi miaka na miaka  hakuitaji upweke umtafune,alihitaji mtu wa kuwa karibu naye.   

        “Nitaongea na Balozi,” Aliwaza.“ Nitamweleza, nitamwambia ninahitaji MTUMI (mtumishi), boy wa kunisaidia kazi mbali mbali za hapa nyumbani, ninahitaji starehe zaidi, kupumzika na kufurahia maisha ya kiafrika.” Wazo lake lilikuwa hilo tena alihitaji kumshirikisha Balozi aliyempokea amsaidie kutafuta Mtumi wa ndani. Amekwisha fanya uchaguzi anahitaji Boy wa miaka kama vile Ishirini au Ishirini na mitano amsaidie shuhuli mbali mbali za pale nyumbani.     

                   ##################################

       “Shaka ondoa,” Balozi alimweleza yule mgeni ambaye tayari siku ya leo amemweleza  juu ya matamanio ya moyo wake, yaani Islama anahitaji kuwa na mtumishi wa ndani kijana mdogo wa umri wake.      

    “Haitachukua muda mrefu kumpata huyo Mtumi ambaye mimi nitakuletea, muhimu ni wewe humjali huyo mtumi ambaye nitakuletea, mpe chakula bora, maji, mavazi pesa na pia ushauri bora. Hakika utawapenda sana Watanzania sababu Watanzania ni watu wapole, watu wema wenye huruma na waaminifu siku zote.” Balozi aliongea.       

      “Ninashukuru sana Balozi kwa msaada wako,” Islama alimjibu Balozi kwa ufupi     

        “Worry off” Balozi aliongea tena,      

       “Je leo una ratiba gani ya Ziada siku ya Leo?    

          “Hata sina Balozi,”        

      “Ungependa tutoke Out kidogo ukawasalimu wenyeji wako, wapate kukuzoea na kufurahi pamoja na wewe?”           

      “Ningependa Balozi. Wacha niende chumbani nikajtupie vazi la kutoka nalo Out ili nami nikajinafasi. Islama aliongea naye akaingia chumbani kwake, akavaa  gauni lake moja jeupe lenye madoa madoa meusi akapendeza mbele ya macho ya Balozi huyu ambaye alizidisha matamanio yake kwa huyu mgeni mwenye ENGLISH FIGURE ‘Modo’         

       “ Kumbe wajua kuvaa eeh! Haki! Lazima upate mwananume Maasai wa kukuoa hapa Maasai land.” Balozii alitania.       

         “Teeh teeh teeh” Islama alicheka

 “Mwanamke kupendwa ni haki yake.” Islama aliongea.     

        “Shaabash! Kitu kama hicho,” Balozi aliongea, amevalia mavazi ya kimaasai, kanga karibia mbili tatu laini zenye madoa madoa mekundu na meusi, zina maua maua na urembo. Katupia Lubega mabegani mwake, kanga na hiyo Lubega ni zenye mistari ya kila dizaini, chini ya miguu yake ametupia  MAKURUBASI (Makatambuga au Malapa) shanga zimejaa miguuni, mikononi na hata shingoni kwake, daima upendelea kutembea na Sime kiunoni kwake ni mrefu mweusi tii ukimtizama waweza kudhani ni wa umri kati ya miaka 40 au 45. Mcheshi japo ni mwingi wa matamanio ya ngono, wanawake wawili waliomzalia watoto watatu  yamkini hajatosheka nao, hamu yake ni kuufurahisha mwili wake kwa mapenzi.      

          “Umzuri kama Malaika.”Balozi alimtania Islama wakati wote ule wawili wale walikuwa wakipita pita ndani ya kijiji cha MAASAI LAND, Islama kwa sababu alikuwa ni mgeni alifanya kuzubaa zubaa huku na kule akiwatizama watoto, vijana wazee na watu wengine wakiwajibika kwa kazi za kila siku                Wanawake walikuwa bize kupamba nyumba zao mpya walizojenga wao wenyewe walizipamba hizo nyumba kwa michoro pamoja na maua, wanaume walijiweka bize kuchonga na kutengeneza pinde, mikuki na mishale, vijana walionekana wakiwaswaga Ng’ombe na kuwaingiza bandani, wakati watoto wakicheza na kuuburudisha utoto wao.              

  “Asante sana, Mungu amenijalia, lakini pia hata wewe Balozi u mzuri, ngozi black, mavazi na mapambo yaliyo mwilini mwako yanavutia.” Islama alongea          

          “Ninategemea siku moja waweza kuja kunipa nafasi ya kuwa mgeni ndani ya nyumba yako.” Balozi aliongea Islama akacheka.      

             “Teeh teeh teeh, wacha kwanza niwe mwenyeji  hapa Maasai Land, niyazoee mazingira, niwazoee watu pamoja na vyote vinavyo kizunguka kijiji.”         

             “That’s  great.” Balozi alitabasamu, moyoni mwake akijisemea, “Nitafurahia ofa ya kuwa na wewe maishani mwangu, sijapata kumla Kuku wa kizungu, sio haba yawezekana ni mtamu mwenye radha ya Asali” Matamanio yalimzidi Balozi, wakaendele kutembea tembea wakikitizama kile kijiji kilicho jaa nyumba zenye makuti na paa za mbavu za Umbwa.

"""""""'"''''''""""""

Jumamosi ya leo Islama alikuwa akimwagilia mwagilia Bustani yake nzuri ya Maua yenye rangi za aina mbali mbali, yapo yenye rangi nyekundu, pinki blue na zambaru mengi zaidi ni yenye rangi ya kijani, anayapenda sana maua sababu maua yanamvutia sana machoni kwake, mara nyingi umkumbusha na kumrudisha nyuma zile siku alipokuwa Sekondari nyumbani kwao England, mwalimu wake wa somo la Biox (biology) alimfunda vizuri juu ya uzuri wa Maua, Maua kama mapenzi yenye ubora na uzuri japokuwa maua hayadumu kwa muda mrefu usinyaa na kunyauka, hilo halimtishi Islama kama ni kupenda kapenda na kupenda huko ni kupenda kuanzia moyoni.     

       Aliendelea kuyamwagia maji yale maua yake, taaratibu taaratibu, kumbu kumbu juu ya jioni ya jana alipotoka Out pamoja na Balozi zilimjia, alijikuta anakumbuka jinsi gani alivyomwona mwanaume mmoja kijana mweusi wa asili, mrefu kama twiga, sio mwembamba sana kama asilimia kubwa ya vijana alio waona hapo Maasai land.Kijana huyu alimvutia sana Islama, ubora na mwonekano wa Yule kijana uliufanya moyo wa Islama udunde mapigo, ndu! Ndu! Ndu! Kwa ubora na mwonekano wa yule kijana wa kiafrika, akamtizama ajabu, akamtizama almanusura aanguke kwa kujikwaa, kwa bahati nzuri Balozi hakujua hilo waliendelea kuzuru kijiji cha Maasi land.      

      “Anachunga Ng’ombe Mbuzi na Kondoo” Islama alimuwaziia yule kijana aliyeuteka moyo na mtima wake. kijana aliyekuwa bize akiwaswaga swaga Mbuzi, Kondoo na Ng’ombe waliotoka malishoni.          

     “Mbona moyo wangu unaenda kasi,” Islama alijikuta anaacha kuyamwagia maji yale maua, akajishika upande uliopo moyo wake, lo! Mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi zaidi, jasho lilimtoka moyoni.      

        “Mmh! Sijawahi kupenda, Haki! Leo ndio ninajikuta ninapenda maishani mwangu.” Picha ya boy wake David aliyemuacha huko England ilianza kujichora machoni kwake, akamfananisha David pamoja na huyu kijana anayechunga Mbuzi na Kondoo hata hivyo hakupata picha halisi, alisikia sauti ikimnongoneza masikioni kwake:  “Huyu mwafrika uliyemuona jana ni zaidi ya David mpenzi wako, huyu ni mzuri ameboreka, angalia waafrika ni wazuri watanashati, BLACK IS BEAUTIFUL.”     

   “Mmmh!” islama alijikuta anaachia mguno        “Nifanye nini ili nimpate yule kijana, mbona moyo wangu umempenda kwa ghafra, ingawaje sijawahi kupenda kwa matamanio haya,” Alichanganyikiwa.     

    “Idont know what to do? Siju nifanyaje?” alijikuta yupo njia panda hana mbele hana nyuma mapenzi yamemkamata kweli kweli na ukitegemea mapenzi kikohozi hayana kificho. Basi Islama akajichumia moja ya Maua yenye rangi nyekundu pale bustanini kwake.   

         “Tanzania is beautiful anda her peoples too” Kimomboo kilimtoka mdomoni, akiyanusa nusa maua yake yenye harufu njema puani, kwake Maua ni manukato yaliyojaa mapenzi, kwake maua ni bahati njema, kinachomvunja moyo kuhusu maua ni jinsi gani yanavyonyauka na kudondoka, hapendi kuona hivyo, anapenda kuyaona yakimea miilele kwa sababu kwake maua ni mapenzi.”        

   “knock knock nock, hodi hodi!” Islama aliisikia sauti ambayo sio ngeni masikioni kwake, tayari amekwisha izoea, ni sauti ya Balozi Ole anaijua vizuri sauti ile        

      “Come on in, karibu balozi Ole.” Islama alimkaribisha Balozi Ole, akiutizama mlango wa kuingilia  nyumba yake  (Geti) hapo ndipo sauti ya kugongwa kwa lango lake ilisikika.    

      “Pita Balozi Ole, lango lipo wazi nimelirejesha tu.” Balozi Ole aliingia amebeba kifurushi kidogo kilichofungashwa na kuzibwa kwa kitambaa kizuri cha kimaasai nyuma yake ameambatana na kijana amabaye Islama alipomwona tu, we! Mapigo yake ya moyo yakamwenda kasi kama Roketi juu ya Mawingu, asitake kuamini kama kweli yule kijana aliyekuwa akimuwazia muda si mrefu leo hii ameambatana na Balozi            Ni kijana aliyemuona jana, kijana anayeufanya moyo wake uende mapigo mazito, kijana naye mfanya Islama kupumua pumzi ndefu na nene nzito ajabu, yeye binafsi amekiri kwa kusema ‘HAJAWAHI KUPENDA NDIO MARA YAKE YA KWANZA KUFANYA HIVYO”               

Itaendelea sehemu ya Tatu

Fungua blog ujisomee hadithi zingine

Binya kwenye maandishi unafurahia.

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...