1
Ndoto ya kutisha.
SEHEMU YA KWANZA
Nilipo liona shimo kubwa zaidi sikujishauri mara mbili mbili, nilifata kshia nikajitumbukiza ndani bila kujali kilichomo ndani nilitumia sekunde kadhaa ku kuifikia sakafu ya shimo lile, kulikuwa na giza nene haijawahi tokea, nilishindwa hata kuviona viungo vyangu binafs. Hewa ilikuwa ni nzito sana, nilipapasa papasa nikagunduwa kuwa upande moja ulikuwa unaendelea yaani kama andaki, moyo ukiendelea kuruka mapigo, akili imesimama na macho hayafanyi kazi, nilisikia sauti ya vuuu ikivuma ghafla kimya kilinitawala halafu sikujuaa kinachoendelea
Jina langu ni Rashidi Mbwana Kidas, nilijibu kwa sauti ya kukwama kwama wkati yule Mkwiranyinza yaani mkuu wa wazee akiendelea kunihoji pia fahamu zangu zilikua zikinirudi taratibu taratibu hadi pale nilipokuja kugundua kuwa nimerudi tena mikononi mwa Wangunjwasi watu ambao wanakula nyama za binadamu wenzao. Mapema asubuhi ya leo nilikuwa porini nikiwinda nijipatie kitoweo na kwa mbali nilipomuona swala aliyenona nilimlenga na mshale, kituuu! Tumboni kwa kawaida huwaga sikosei.
Ila kabla swala hajadondoka chini alipigwa na rungu lenye ncha tofauti tofauti tena lile rungu lina visu vya chuma pande mbili za kupigia. Nililistaajabu lile rungu nikashindwa kulitolea majibu hata babu yangu mzee Kidasi aliyemiliki maarungu mengi kuliko mtu yeyote kijijini kwetu Mng’ta hakuwahi kuwa na rungu la aina hiyo yaani halielezeki. nikajishauri atakuwa ni mwindaji mwenzangu ngoja nisoge tukagawane nyama. Nilipofika swala alipo sikuamini Macho yangu hawa ni binadamu au?” Nilijihoji.
Kwa upande wa uso walikuwa wana macho makubwavyenye viini vyekundu, macho yenye nyusi chache. zilizo onekana zimenyofolewa kwani vinaacha vidonda ambayvyo damu yake iliyoganda inaacha alama nyekundu juu ya vidonda, wanapua kubwa zenye matunndu ya kutosha kupitisha mdomo wa chupa ya soda na nafasi ya kidole kimoja ikabaki
Midomo yao ni mipana yenye meno yaliyo achana takribani sentimenta mbili unusu kutoka kwenye mjino hadi mjino tena miisho ya midomo yao imechanika chanika harafu ina rangi nyeupe kama vifaranga vya kuku ndimi zao nyembamba ndefu nyekundu zilizo chanika chanika yote tisa kumi midomo yao ilitoa harufu kali iliyonipa kizungu zungu kwani muda wote wao wana kenua. Watu hawa hawaongei Kiswahili wanaongea kwa kinjwasi lakini uwezo wa ajabu ulinijia nikawa nawajibu kwa kinjwasi pia. Wangunjwasi wapatao sita walinizunguka mimi na yule swala wakiniangalia kwa dharau kisha mmoja ambaye ni mfupialiyeonekana kuwa kiongozi alinifata akaanza kunihoji;
MGUNJWASI: Pesechuki pesika? Pwipenshupata (umefata nini kwenye himaya yetu?)
MIMI: Pswitanjei (Nisamehe)
MGUNJWASI: Potatakisepwetikwapa (umetokea wapi?)
MIMI: Pistwanjei (Nisamehe)
MGUNJWASI:Pwipwi pistwasnjewo pisgoteda (Mbebeni atasamehewa nyumbani)
Aliwaamuru wenzake wanibebe nikibubujika na machozi nilizidi kumuomba msamaha lakini nilikuwa nampigia mbuzi gitaa.
Yeye aliye kiongozi alitangulia na mmoja kuondoka akifuatiwa na mwingine mmoja aliyeonekana ‘bodguard’ ingawa ndiye mzee kati ya wote. Kisha wawili walimbeba swala na wawili wengine walinibeba mimi kutokana na uzito wangu kundi hili la mwisho lilikuwa linatembea taratibu taratibu kwa sababu hiyo katika kuhangaika kwangu nilifanikiwa kujirusha toka mabegani na wale wenzao waliokuwa mbele hawakuyajua yanayoendelea nyuma kwani walituacha umbali kidogo.
No comments:
Post a Comment