Friday, October 4, 2024

KUCHEPUKA SIO DILI... Sehemu ya kwanza



Sehemu ya kwanza

 ANATOKA HOME.

Maisha ya leo yamebadilika sana, maisha ya leo ni tofauti na maisha ya zamani, dunia ya leo sio kama ile dunia ya zamani, dunia ya zamani watu walifanya kazi kwa muda mrefu sana pasina kuchoka waliwekeza nguvu zao  zote kwenye shughuri zilizo waletea kipato. Starehe kwao haikupewa kipaumbele kwa sababu ngoma ziliwatosha watu hawa kujiburudisha mara baada ya kufanya kazi nzito, pombe ilikua ni kinywaji cha burudani, hadithi ziliwafunda na kuwaonya kutokana na hayo mazuri waliyo jivunia jamii zao zilionesha mabadiliko sio kidogo bali mengi yenye wingi.


                  Dunia ya sasa watu hawataki kujibidisha kwenye shughuri  kama kilimo, uvuvi na uwindaji, lakini watu hao hao ndio wanao ongoza kwa kuhama na kukimbilia mijini wakidai kuwa huko ndiko kwenye maisha mazuri, huko ndiko kwenye kazi nzuri kwenye raha burudani na starehe, hwataki kurudi Vijijini, hwataki kuyakumbuka mashamba mifugo na mali asili zingine, hawataki kuzisikia shida zilizopo vijijini wanacho taka wao ni raha, furaha na  uzuri wa maisha yasiyotumia nguvu nyingi.


                      Hawa wapendao starehe, wamo ndani ya majiji makubwa makubwa na yale yaliyo endelea kama vile Dar es saalam, Arusha, Mwanza, Mbeya na sehemu zingine. Baadhi ya hawa watu wengi wao ni wale walio oa na kuolewa wanategemewa na familia zao, wanafanya kazi kwa masaa nane kwa siku. Zaidi ya hapo wapo wale ambao hawajaoa na kuolewa  baadhi yao sio waaminifu katika maisha yao, hawawajali wenzi wao, wanawatoroka wenzi wao na baya zaidi wana wasaliti (wanachepuka) wenzi wao na pia hawahudumii familia ipasavyo.


                Embu ungana nami katika kisa cha bwana mmoja aliye julikana kwa jina la Mawe, bwana huyu aliishi maeneo ya Sinza kijiweni ndani ya jiji la Dar es saalam. Ana kazi nzuri, aliajiriwa katika kampuni moja iliyopo Kariakoo. Mshahara wake mkubwa na mzuri uliweza kutosheleza familia yake yenye mke na watoto watatu.  Wahenga walisema masikini akipata matako ulia bwata. Mshahara wake hakuutumia vizuri yeye binafsi aliutumia mshahara wake kwenye burudani anasa na starehe. Hayo ndiyo mambo ambayo bwana Mawe aliyapenda maishani mwake.


                 Kwa ufupi bwana Mawe hakuwa na ile tabia ya uvivu kazini, alikua ni miongoni mwa wale wachapa kazi, watu wenye juhudi zao, watu wanaojituma zaidi kazini kwao. Lakini siku zote kizuri hakikosi kasoro. Ikawa hivyo tena aliutumia mshahara wake  wote, aliutumia vibaya tena vibaya na ubaya wayeye kutumia vibaya mshahara wake hakuonesha kuijali familia yake.


Aliacha pesa kidogo sana nyumbani kwa ajili ya familia, wakati huo huo fedha zake nyingi alizitapanya kwa wanawake wanao chuna mabuzi na sasa aliangukia chini ya miguu ya mwanadada mmoja aliye itwa Rehema. Huyu ndiye alikuwa akimchuna na kumlia pesa zake, Rehema alifanya kuzitafuna pesa za bwana Mawe mara tu apatapo mshahara.


                 Rehema alizishobokea pesa za buzi lake, hakukoma kuagiza vitu vya bei gharama, hakuchoka kulipangia buzi lake sehemu za burudani, starehe na anasa, Rehema alijiona yeye ni mwenye neema sana kuzitafuna pesa za bwana Mawe.


                 ####################



No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...