FUTURE DESTROYER.
SEHEMU YA KWANZA
SIKU MBAYA.
“Nisamehe sana mke wangu nisamehe mpenzi wangu, nisamehe ninakuomba.” Dini haba aliongea machozi yakimbubujika. Sauti yake ilikua haitoki vizuri mdomoni, sauti yake hafifu sana, amekata tamaa.
“Kwanini Dini haba? kwanini unaniua? Kwanini hutaki niishi ili nifurahie pamoja na wanetu?” Eve aliongea akilia sana ndani ya chumba ambacho Dini haba alilazwa humo.
“Shetani mke wangu, Shetani alinipitia, Shetani aliniongoza na kwa hakika Shetani ameniweza na kunimaliza.” Dini alijitetea. Amekonda, ameisha na kumalizika, amechoka na tena hajiwezi.
“Ulipaswa kuwa mwaminifu kwangu, ulipaswa unipende mimi tu, unilinde na pia unikumbuke mimi tu. Tizama Dini haba, tizama unaniacha pekee yangu, unaniacha pamoja na na watoto, ni nani atakaye kuwa radhi kuwasaidia watoto hawa ambao hawatakuwa na baba yao mzazi?” Eve aliongea kwa uchungu zaidi, anatizama future ya wanawe wapenzi Maya na Mainesi.
“Watunze watoto wetu, watunze bila kuchoka, watunze kwa uvumilivu wako wote, sipendi kukuachia mzigo wa kuwalea wanetu lakini ndio hivyo tena, sina jinsi, lazima nitaondoka, siku zangu sio nyingi, tayari zimehesabiwa.” Dini haba alikata tamaa na kufa moyo akijua fika kwamba hana muda mrefu wa kuishi duniani, kwa jinsi alivyodhoofika mwenzangu ukimwona utamuonea huruma.
“Amekonda kweli kweli, amekonda na kuwa mwepesi kama karatasi, amekonda hatamaniki, mapele yamejaa mwili wake wote, nywele hana kichwani, zote zimepukutika, kukohoa hakweshi anabanja kweli kweli, kuharisha hakukomi anahara vibaya, kutapika, imekuwa mazoea hana hamu na maisha.
“Iiiiii! Uuuuh! Iiiiih!.” Eve alilia akitafakari juu ya future yake yeye na wanawe wapenzi Maya na Mainesi, ni kama vile analiona giza mbele yake, ni kama vile hapati picha halisi, future yake anaiona kama imefedi awei (fade away) imepotea na sio kupotea tu bali pia imepotezwa na mumewe mpenzi Dini haba.
“Sikuwa mwaminifu kwako mpenzi, nilijifanya kukupenda sana wakati huo huo nilikuwa nina wamiliki wanawake wengi wengine, wapendao anasa na starehe za dunia hii, nilijifanya kukupenda kumbe wakati huo huo nilikuwa nina wamiliki wanawake wengi wengine, wapendao anasa na starehe za dunia hii, nilijifanya kukupenda kumbe wakati huo huo tamaa yangu ilikua ipo juu. Niliuficha ukweli na uhalisia wa mapenzi yetu, tazama leo ninajuta. Dini haba aliongea kwa kusikitika.”
Kweli tamaa mbele mauti nyuma, heri kumuheshimu Mwenyezi Mungu na kuyafanya yale yote apendayo mwanadamu ayafanye, kuliko kuupoteza muda mzuri duniani kwa kushea mapenzi na wale wote wa pendao anasa. Wanawake wazuri wenye kutamanisha, wazuri wenye mvuto wa ajabu, wazuri wa maumbo ya kutamanisha wazuri wenye sura za kuvutia wazuri ajabu.
Uzuri wa Dini haba yeye alijiona ni dume, dume rijari, hakaukiwi hamu na matamanio ya mwanamke. tena yeye umpa mke wake haki yake kila siku atakayo mkewe wakati huo huo kabla ya kumpa mkewe hiyo haki ni lazima awe amekwisha pita pita kwenye madanguro au kwenye mabaar ya mabaamedi aonje onje ule mvuto naye aridhie na kuridhika kabla hajarejea kariakoo nyumbani kwa mkewe.
koh koh koh koh. Dini Haba alikohoa na kubanja, ama kweli amechoka, ameisha na kupoteza uzuri wake wote, amekuwa kama vile sio yeye, amekuwa mfano wa wale wakimbizi walio kosa chakula miezi na miezi, maduka yake yote ya nguo, maduka matatu aliyokodisha (aliyo azima) hapo kariakoo mtaa wa uhuru hanayo tena, amefirisika tena hajafirisika bure, bali amefirisika kwa sababu ya huu ugonjwa umtesao, ugonjwa unao mgharimu ,ugonjwa unao mtia hasara ya umasikini.
“Ninaondoka mke wangu, ninaondoka nikiwa masikini wakati zamani nilikuwa tajiri wa kutegemewa, ninaondoka mtupu wakati nilikuwa nina kila kitu mwilini mwangu, ninaondoka ni mwenye aibu wakati nilikuwa ni jasiri na hodari, oooh! Masikini! Unisamehe mke wangu.” Chozi lilimtoka kijana yule mwenye umri mdogo wa miaka 30 ni kweli alikuwa tajiri lakini sio tajiri bilionea bali tajiri mwenye mamilioni ya shilingi Benk, mwenye magari, mwenye maduka ya biashara, maduka matatu aliyo kodisha hapo kariakoo.
Ajabu leo hii kuuguza ugonjwa wake, ugonjwa wa aibu, ugonjwa wa Ukimwi, ugonjwa umemgeuzia umasikini, yale maduka matatu hayana kitu, ni meupe peee kama chaki, yanahitaji mpangaji mwingine wa kuingia hapo ili biashara iendelee na maisha yaendelee kupiga hatua.
Hayo magari anayo yamiliki nduguze, ndugu wa damu yake wameyachukua na kugawana, wana yatumia ovyo ovyo kama vile wao ndio walio yanunua, hawana uchungu na mali ya ndugu yao. Hizo pesa zilizopo Benki zimechotwa zote zimeliwa na hao ndugu wa upande wa DIni haba, ndugu hawa wasio na huruma wakafanya kumuachia Dini nyumba yake aliyoijenga hapo kariakoo.
Baya zaidi hawa wanandugu wangali wameanza kuimendea hiyo nyumba, wanaitamani sana weshajua kuwa ndugu yao hana uhai tena, mkewe ni miongoni mwa wale watarajiwao kuzikwa mara baada ya mumewe kufa. Ndio maana hawa wana ndugu hawana hofu na mashaka, pole pole ndio mwendo, subira yavuta heri, mdogo mdogo taratibu watafika.
“Nina kiu….” Dini alimwambia Eve aliyekuwa yungali analia amesimama pembezoni mwa kitanda alicho lala Dini upande ambao Dini amelaza kichwa chake, wanatizamana.
“Nipe maji ninywe.” Dini aliomba apewe maji ili atulize koo, azimishe kiu yake. Eve akayachukua maji safi yaliyokuwa ndani ya jagi akayamimina ndani ya glass safi baada ya kumaliza kuyamimina akamgea mumewe apooze kiu yake. Hakujua kuwa kile kitendo cha kumgea mumewe maji kilikua ndio maagano kati ya yeye na mumewe, hakujua kwamba hiyo ndiyo safari ya mumewe kwenda kupumzika, hakujua kwamba huo ndio mwisho wa kumuona mumewe.
Akiwa angali analia analia sana, ndani ya dakika sita za kilio chake, Eve alimwita mumewe karibia mara tatu, lakini mumewe hakumwitikia, alimtikisa sana lakini bado tu mumewe alikua angali mgumu kuamka. Akayatizama mapigo ya moyo ya mumewe, duh! Mapigo ya moyo yalikua hayapandi wala hayashuki akafanya kumtikisa tikisa tena lakini majibu yalikua ni yale yale, mumewe asingeliweza kuamka tena. Hapo ndipo Eve alianza kulia kwa sauti kuu, sauti ambayo iliwawafanya madakta na wauguzi waje haraka ili kujua kunani? (kulikoni? Kuna nini?)
#########
Mara baada ya mumewe kutangulia mbele ya haki, Eve aliachwa upwekeni, akiwa angali pekee na wanawe mabinti wawili Maya ambaye ndiye binti mkubwa mwenye umri wa miaka kumi na miwili. Mainesi Aliyekuwa na umri wa miaka sita tu. Mtu na dadaye wlipishana umri wa miaka sita tu.
Kifo cha mumewe kiliyabadirisha kabisa maisha ya Eve hali ya umasikini tayari ilikwisha gonga hodi nyumbani kwake, zile zama za kuishi kwa raha akimtegemea mumewe pasina kujibidisha na shughuri yeyote ile tayari zilikwisha fikia kikomo na sasa alihitaji kujishughurisha ili apate kuyanusuru maisha yake yeye pamoja na nawe wapenzi Maya na Mainesi.
Ajabu iliyoje yule mwanamama aliyejaliwa raha na fahari siku ambazo mumewe alikuwa hai leo hii siku hizo zimegeuka na kuwa siku za mawazo na masikitiko, hana mbele hana nyuma, anajitahidi hivyo hivyo kuzipiga bei nyanya, vitunguu, karoti na mboga mboga za majani kunako kigenge alicho kifungua. Hicho kigenge kinamsaidia kidogo kupata vijisenti vya kumuwezesha awalishe wanawe, ajinunulie mahitaji kidogo na kuifadhi akiba. Japo ni kidogo hata hivyo hana budi kushukuru mungu kwa haya machache anayo msaidia.
Pesa zote za akiba aliyo achiwa na mumewe, yale mamilioni ya shilingi hana tena, yamechotwa na kutafunwa na ndugu wa mumewe. Magari ya fahari aliyo zoea kutembelea hana tena, yameuzwa yote na zile pesa zilizopatikana kutokana na hayo mauzo ya magari zimetafunwa na hao ndugu wa mumewe. Biashara ya mumewe (yale maduka matatu ya nguo pale kariakoo) haipo tena, imekufa na kufirisika.
Ameachiwa nyumba pekee na hata baada ya maisha kumwendea kombo Eve alijikuta akiviuza vitu vyote vya ndani (fanicha) hakua na jinsi alijikuta anauza mali zile za bei gharama kwa makubaliano ya bei ya kutupwa na kuhuzunisha, bei ya hasara hasara, alifanya hivyo apate kuyaboresha na kuyasukuma maisha yake na ya wanawe wapenzi Maya na Mainesi.
#####
Itaendelea
No comments:
Post a Comment