Monday, October 7, 2024

I miss you Lupita... Sehemu ya tano

 


I miss you Lupita
“Tena,” Raisi Antonio aliendelea kuongea.
“Tena, from now and so on, nisitake kuusikia usumbufu wowote ule ambap wewe utauita taarifa, chonde chonde nisitake kusikia taarifa zozote zile kwenye vyombo vya habari, taarifa ambazo wewe utawaambia waandishi wa habari, taarifa mbaya utakazosema kuhusu mimi na mke wangu Lupita. Kumbuka mimi ni Serikali na Serikali ni mimi, mimi nipo juu ya Serikali.”
        “Ujapotaka kuniletea za kuleta na mimi nitakuletea za kuleta, hakika utajuta na kuikumbuka vizuri siku yako ya kuzaliwa.” Antonio alinitisha, akaamka pale alipoketi na kutaka kuondoka.
        “Kama utakuwa na shida yoyote ile usisite kunitafuta, hupo huru kuanzia sasa kuja Ikulu, Karibu Ikulu tupate vikombe vya kahawa.” Antonio aliongea anatembea kwa kutumia mkongojo wake unaomsaidia kujisukuma sukuma akaondoka akaniacha ni mwingi wa hasira, sijui nitamdhibiti namna gani, yeye ni Serikali aliye juu ya Serikali”
Ilipita miezi mitisa sasa tangu litokee tukio la mke wangu Lupita kunitoroka na kuniacha upwekeni. Niliamishiwa Australia, niliamishiwa kwa lazima sio kwamba nimefukuzwa nyumbani bali nimelazimishwa kuingia ndani ya Siasa, Nimepewa cheo cha Ubalozi, kuiwakilisha Nchi ya BARA.
        Nimepewa cheo hicho makusudi ili niwe mbali na mke wangu wa zamani Lupita, Nimepewa cheo hicho kwa kusudi ati nijitahidi kumsahau mke wangu mpenzi Lupita, ni maumivu, maumivu moyoni, maumivu na kidonda cha mapenzi siwezi kumsahau, bado ninampenda, japo nguvu za kulithibiti zee lake hizo ndizo sinazo. Sina nguvu  za kumrudisha yule nimpendaye, nabaki kila siku nikimwaga machozi na kusema I MISS YOU LUPITA. Nafanya kutazama picha tulizopiga siku ya harusi yetu, nina zibusu zile picha tena ninajisemea I MISS YOU LUPITA, ooh! Machozi, machozi ya uchungu, uchungu wa kupokonywa mke wangu mpenzi. Mpenzi wa moyo wangu LUPITA.
        Asubuhi ya leo, Secretary wangu mrembo, mwenye asili ya kihindu kaniletea Bahasha kubwa, iliyotoka Posta, imetoka nyumbani BARA nami nikaifungua taaratibu nikaanza kuisoma. OH! MY GOD OF MY GOODNESS! nilishituka pale nilipoiona Kadi, kadi ya mwaliko mwaliko wa harusi, harusi ya Mke wangu mpenzi wa moyo wangu Lupita pamoja na Raisi Antonio……… Moyoni niliumia, nikajisikia kujuta nikajiona sifai kwa sababu ya kumpoteza yule nimpendaye  mtu mwingine mwenye madaraka yake amenipokonya, ninajiona dhaifu, ninajiuliza moyoni mwangu ‘kwanini nilishindwa kumlinda yule nimpendaye? Kwanini nilishindwa kumpiigania Lupita? Kwanini nilimuacha aende?’ Tizama leo nimetumiwa kadi ya muhaliko wa aharusi yao ninaambiwa siku sio nyingi ni Mwezi ujao, harusi ya Lupita na Raisi Antonio itakuwa ni bonge la harusi, harusi ya kukat a na shoka ndani ya nchi ya BARA.
        “Upuuzi.” Najisemea Moyoni mwangu
        “Nani aende kwenye harusi ya yule aliyenitema moyoni mwangu?”
        “ Oh! Japo kuwa ningali bado ninakupenda wacha niseme, I MISS YOU LUPITA.” Sijui amensikia? Any way nina imani amesikia ujumbe wenyewe ndio huu,nina imani yupo kuusoma, ila naomba nimwambie  neno moja tamu neno lisilo nitoka mdomoni mwangu, “IMISS YOU LUPITA.”
        Maliki-Shua analia kila siku ananiambia, “Baba NIME MMISS MAMA, ni lini atakuja Australia, ili tufurahi pamoja,  tule vyakula vitamu yva wenyeji wa Austalia, tucheze ngoma za Wenyeji wa Australia, tuzunguke sehemu za miji mbali mbali ya Australia,.” Machozi yanamtoka mwanangu lakini ooh! Wacha niseme neno moja I MISS YOU LUPITA
     Siwezi kuendelea tena kuandika. 

“IMISS YOU LUPITA.”

MWISHO

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...