Sunday, October 13, 2024

1. Ooh! Maskini!!

 


OOOH! MASIKINI!!!

   


MOJA

MAJONZI.

                 Shaaban na Nela hawakutegemea, maishani mwao mwote kama siku moja wangeliishi katika maisha yale, maisha yaliyojaa manyanyaso, mateso na utumwa mwingine mwingi ambao mtoto wa Kiafrika hakupaswa kutendewa. Mateso aya kwa shaaban na na Nela ilikua ni kama ndoto kuyasikia ajabu leo na kesho wanakumbana nayo.

               Yallabi! Toba! Leo hii watoto wale wamekumbana na changamoto nzito, changamoto hiyo inaumiza vichwa na nafsi zao kila wakijaribu kuyakumbuka maisha waliyopata kuishi pamoja na wazazi wao Shaaban na Nela wanalia, wanalia vilio vikuu, vilio vinavyo umiza mioyo yao, nafsi zao na akili zao za kitoto

               Hawakutarajia kama  ipo siku Mwenyezi Mungu angelifanya maamuzi yake, maamuzi ya kuwatenganisha  watoto hao pacha kutoka kwa wazazi walio wapenda sana, wangali wadogo bado, wadogo wenye umri wa miaka mitano. Katika umri huo baba na mama yao walipatwa na umauti, ajari ya gari, gari iliyoporomoka na kuingia mferejini. Kipindi hicho wazazi  wao walitoka Lushoto Tanga walikokwenda kutalii,  kubadirisha mazingira,  kufurahia uzuri wa milima na vilima vya Lushoto, kupigwa pigwa na baridi ya Lushoto, mvua isiyo koma pamoja na umande.

                 Looh! Kifo hakitabiriki, hawakujua wazazi wa Shaabani na Nela, hawakujua kwamba wangelipatwa na ule umauti uliotokana na ajari mbaya, gari lao liliporomokea kwenye mtaro (mfereji wa maji taka) na ubaya wa bara bara za Lushoto Tanga Haki! Mwenyezi mungu azilaze roho zao pema peponi, gari yao up iliacha njia ikaporomoka na kuingia mtaroni ikajigonga gonga juu ya mawe mazito makubwa yaliyo vunja vunja vioo vya ile gari, vioo hivyo vikawakata kata baba na mamae Shabani na Nela.

                Looh! Ombea chochote katika maisha yako lakini mpendwa usiombee kifo, kumbuka kwamba kabla umauti haujawachukua baba na mama Shaabani na Nela, watoto hawa waliishi kama vile ni watoto wa kifalme. Madekezo mengi mapendeleo mengi mapendo na matimizo ya kila kitu ambacho watoto wale walitamani, walililia, waliona, walinusa walihisi au walifikiria.


               Msubisi Jacob ndilo jina la marehemu baba yao, alikua ni Bosi wa TRA (Tanzania revenue authority) sijui ni shirika la kodi? Sijui ni kampuni? Sijui ni taasisi? Sijui. Pesa mingi, mshahara kibao, marupu rupu kibao. Kuna nyumba mbili na horofa moja, kwenye hati za nyumba hizo hukosi kuliona jina la Shaabani na Nela. Kuna magari matatu binafsi, gari moja ndilo walitumialo baba na mama Shaabani na Nela, ni hii prado iliyoporomoka na kusererekea kwenye mtaro wa maji machafu na kusababisha vifo vya wazazi wa Shaaban na Nela


                 Magari mawili yaliyo salia ni zawadi kwa Shabani na Nela, magari haya yamenunuliwa kwa bei gharama, magari haya yanatunzwa na kuifadhiwa kwa ajiri ya Shaabani na dadaye Nela, wangali ni wadogo wacha wadeke na kudekezwa, wakiisha kufikisha umri wa miaka kumi na minane watakabidhiwa mali hizo, kwa sasa acheni watoto wadeke na kudekezwa wangali ni wadogo sana.


                Naomi ndilo jina la mama yao Shaabani na Nela, awali kabla hajaolewa na Bwana Msubisi bibie alikua ni mwisilamu akiitwa Nusrati lakini kutokana na mapenzi yake mazito kwa Bwana Msubisi alijikuta anabdiri dini na kumfuata mumewe. Nusrati ni mwenye uchotara wa kiarabu na kiafrika aliamua kutoka pemba kwenda Dar es saalam wakati huo huo aliamua kutoka kwenye uislam na kwenda kwenye ukristiani


                   Kielimu, Naomi amesomea masuala ya fedha (uhasibu). Naomi aliajiriwa na Benk moja kubwa ndani ya jumuhia ya Afrika Mashariki (EAC). Watoto wao pacha walipo zaliwa wazazi hawa wenye hekima walifanya kuwafungulia Account Benk, kwenye hizo Accouunt Wazazi wale waliwatunzia watoto wao pesa nyingi kwa ajiri ya maisha ya Kesho na kesho kutwa, ujana na uzee. Maisha hayatabiriki ndio maana Msubisi na Naomi walihitaji kutunza pesa kwa ajiri ya watoto wao Shaabani na Nela.


                  Shaabani na Nela walipofikisha miaka sita, Msubisi na Naomi walikwisha panga kuwapeleka watoto wao New York, Marekani. ili wakaanze rasimi masomo yao, walihitaji kuwapeleka kule ili watoto wakabadirishe mazingira na kufurahiamaisha ya kizungu na fahari ya maisha ya wenzetu walioendelea. Zaidi


              Mpango ulikua ni kuhakikisha Shaabani na dada yake Nela wanaishi huko huko Marekani, wamalize vyuo wapate kazi warudi nyumbani Tanzania kuwasaidia wazazi wao na jamii yao. Lakini dah! Ya Mungu mengi, wao wanapanga Allah anapangua, walicho pangiwa kamwe hawawezi kukipangua. Ndio hivyo basi isiwezekane wa chini angojwe juu na wa juu atangojwa chini yale maisha mazuri yenye raha na furaha yakaporomoka yakashuka na kupotea mara baada ya vifo vya wazazi wao Shaabani na Nela.


Itaendelea

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...