Kila siku nilikua ni Binti mwenye furaha
Wazazi wangu walinidekeza nami nilideka
Ni vile tu majirani na marafiki zangu wakinicheka
Tena walithubutu kunizomea
" Hilo, Hilo... Zaifu hiloo."
"Hilloo baba na mama yako hawana NGOZI... Hiloooo." Maneno haya yaliniuma kila siku
Sikuwaonesha darili wazaz wangu
Kwamba naumizwa na maneno pamoja na kebehi za majirani
Nilijifungia chumbani
Nilibaki nalia tuπ chumbani kwangu mie Debora Na Zingo πππ¦sokwe wangu
Masikin mieπππ
Baba na Mama walinipenda
Pendo la kupendeka
Pendo lililozidi pendo
Pendo maradufu
Na madekezo yao kwangu yalipaMBA MOTO
Leo navaa gauni jipya na kiatu jipya
Kesho nanunuliwa PIZZAπ midoli na vitu vya kuchezea
Keshokutwa napelekwa ⛱️ π️ beach kuchezea MAJI
Lakini bado tu huzuni haikuniisha
Pale majirani na marafiki wakinicheka eti baba na mama YANGU hawana NGOZI
Nooo!
kulia kwangu kuliniumiza zaidi.
Sikuzitaka ZAWADI walizonipa wazaz wangu
Tena nilizibutulia hukooo!
Nikadharau
Sababu ya HASIRA HASARA
Mie Debo na Sokwe wangu Zingo tukapakia
Tayari kuondoka
Tena kwenda mbali na nyumbani
Tusirudi Tena
Tusirudi kwenye midomo na kelele zao majirani
Lakini kadri nilivyozitazama zile picha
Ndivyo nilivyopata kuelewa
Mtoto asiye na NGOZI alipewa NGOZI ya baba na mama yake
Yaani baba na mama walijuchuna NGOZI zao Ili kumfunika YULE NTOTO ASIYE NA NGOZI
Wale wazaz wawili waliokua wakilia niliwatambua
Ni baba na mama YANGU
Na yule mtoto asiye na NGOZI ni mimi
Kumbe mimi nilizaliwa bila NGOZI
Kumbe baba na mama walijichuna NGOZI na kunifunika Ili NIWE mzuri wa kupendeza
Nikaanza kuliaππ Tena Kwa sauti iliyosababisha baba na mama wadamke pale kitandani walipolala.
Nikalia masikini mimi Debo
Nikalia upendo huu wa Wazazi wangu,
Unconditional love, upendo usiopungua
Wamejitoa muhanga Ili Mimi niishi
Wamejiharibu Ili Mimi niishi
Na bado tu NATAKA kuwakimbia
ππππ
Hapana, Sintakimbia
Wala sintaobdoka
nawapenda wazazi wangu
NATAKA kuishi pamoja nao.
No comments:
Post a Comment