BABA YANGU HAKUMPENDA MCHUMBA WANGU LAKINI SIKUJALI NILILAZIMISHA NDOA.
Nilikutana na mchumba na Mume wangu tarajiwa Jerome katika mgahawa tuliozoe kukutana kila siku. Tulifanya kuagiza kahawa na vitafuno tukaongea maneno mawili matatu.
''Mapenzi yetu yamedumu Kwa zaidi ya MIAKA SITA Sasa Shelidani Kuna jambo nahitaji kukuambia.'' Siku ya Leo mpenzi wangu Jerome hakuonesha furaha, sikufahamu kwanini? Siku zote utanguliza uchangamfu.
''Una Nini Jerome mbona Leo nakuona hauko sawa?'' Nilimuuliza
''Mbona nipo sawa Sheli,'' Alinijibu Kisha akagugumia kikombe Cha kahawa akatafuna pia vipande vya kashata.
''Nipo sawa Sheli. I'm ok'' Aliongea Tena Kisha akasema
"Ninakupenda niruhisu nikufanyie bonge la sapraizi." Aliongea akiwa na tabasamu usoni, tabasamu pana.
"Nipe mkono wako Kisha fumba macho Hadi nikuambie ufumbue." Nilitabasamu Kisha nikatii agizo lake. Aliushika mkono wangu wa mashoto akaupapasa papasa kama vile anaupakaza mafuta laini ya mtoto. Nilihisi Kuna kitu kimegota kwenye dole langu la shahada. Jerome akaniambia
"Fumbua macho MPENZI"
Waooo! Nilipofumbua macho MOYO wangu uliripuka Kwa shangwe na furaha, nikamrukia Jerome na kumkumbatia.
"I want to Marry you Sheli." Machozi ya furaha yalianza kunitoka. Muda wote wa MAPENZI yetu Leo hii Jerome wangu amenitamkia ndoa. Wacha we! Kwanini nikatae, ndoa ni TAMU Kwa wale waijuao.
"Sasa ni wakati wa kuwapa taarifa ndugu, Wazazi na jamaa juu ya harusi yetu." Baada ya kunivisha Pete Jerome alidai ndoa.
"Tuchukue miezi mitatu tu kukamilisha haya."Jerome aliitamani ndoa.
"Sawa Daring. I love you"Nilimpiga kiss Shavuni.
"I love you too Sheli."Alinipiga busu lingine shavuni na juu ya komwe langu..
Siku mbili baadaye nilikuwa nimeketi Sitting room nikiwa pamoja na wazazi wangu kuwapa taarifa juu ya nia ya MPENZI wangu Jerome kunitaka ndoa. Nikiwa na WINGI wa furaha nikapokea baraka tele kutoka Kwa mama YANGU mpenzi.
"Hongera Binti yangu, hongera MPENZI unaelekea kwenye kundi Bora la maisha" Mama alinibariki.
"Hivyo ndivyo inavyotakiwa Binti akiisha ingia ukubwani lazima aolewe na adondoke nyumbani Kwa wazazi wake akajitegemee na KUMTEGEMEA Mume au wote wakategemeane." Mama aliongea Tena.
"Nakutakia baraka Binti yangu uolewe na yule umpendae, umjuaye na yule uliyeridhika naye ambaye yeye pia unajua mtaishi milele pendo la kupendeka. Nilifurahia baraka za Mamangu. Lakini mmh! Wacha nigune Kwa upande wa babangu mambo hayakuwa sawa, niliambulia maneno yaliyonivunja MOYO furaha na matumaini.
"Uolewe na Jerome yule kapuku mtoto wa kimasikini atakupeleka wapi wewe mtoto wa Tajiri" Dady aliongea maneno Bitter yaani machungu,
"Jerome Hana uwezo wa kukulisha au kukujengea nyumba ya kuishi zaidi ya kupanga Tena hata mkijaliwa watoto hatoweza kuwasomesha Shule binafsi, Shule za kulipia." Baba alimponda mchumba wangu.
"Kuna wanaume wengi wanaotoka familia za matajiri wengine ni watoto wa marafiki zangu kwanini usiniruhusu nikutafutie mwanaume Tajiri? Baba alinishangaza kauri yake.
"Hapana Dady ninampenda Jerome na Jerome ananipenda pia. HAITAWEZEKANA KUTUTENGANISHA," NILIPIGILIA MSUMARI wazo langu.
"Basi Mimi sintakuruhusu uolewe na Jerome sitaki kusikia habari za mtoto wa Tajiri kuolewa na mtoto wa masikini." Baba aliongea maneno yaliyoniumiza.
................
Kwa sababu Dady hakutaka kusikia ninaolewa na mwanaume nimpendaye alichofanya yeye ni kukataa kushiriki mipango ya harusi yetu. Alikataa katakata kubariki Mimi kutolewa na Jerome aliyedai Hana uwezo wa kunilea au kuja kuniboreshea MAISHA. Nilimwambia Dady MAISHA Bora tutayatafuta, tutayatafuta wote wawili yaani mimi na Jerome, lakini wapi! Dady hakuwa tayari kunisikiliza. Mipango yote ya harusi yetu ilifanywa na Mimi mama na Jerome.
Jerome aligharamia kila kitu muhimu Kwa ajili ya harusi kuanzia malipo ya ukumbi, vyakula, Usafiri, mavazi na mapambo. Alifanya mambo chungu nzima Kwa hakika aliimeza akaunti yake yote ya Bank.
Siku ya harusi ilipofika nilipendeza sana mama pia alipendeza. Muda wa kuingia kanisani ulipowadia mama alinisindikiza nikaingia kanisani nikiwa mwenye furaha ingawaje Baba alikataa kuhudhuria harusi yangu mie na Jerome.
Lakini jamani nilipoingia kanisani nilipigwa butwaa kuona Jerome wangu hayupo Ndugu zake, wazazi pia hawapo.Niliogopa. Uzuri watu waliohudhuria kanisani waliniambia Jerome alikuwepo pale kanisani muda si mrefu ametoka akiwa anaongea na mtu kwenye simu.
Nikautuliza MOYO Mtima nikaketi mbele ya kanisa nikimsubiria Jerome wangu lakini Mmh! Jerome hakutokea. Kadri saa zilivyozidi kuyoyoma ndivyo Jerome hakuonekana. Toba! Nilianza kuaibika.
"Nini kimempata Jerome?"Nilijiuliza.
"Simu zake zote zinaita tu lakini hapokei."Nilishangaa.
"Wana SEMA alikuja Kisha akaondoka ina maana alikuja kuniaibisha?" Nilikosa Jibu, amachozi yalinitoka nikalia masikini. Aibu Gani hii, mwanaume ananiaminisha ndoa alafu siku ya siku anatokomea mitini. Nilimwaga chozi.
>>>>>>>>>>>>>>>
Lakini kumbe nisiandikie mate wino ukiwepo. Jerome alipowasili kanisani simu yake iliita, alikua ni mama yake ambaye alimtaka Jero haraka sana aelekee Aghakhan Hospital. Mama alimwambia Jerome Shishi mtoto wa marehemu dada yake Jerome yupo hoi taabani amelazwa ICU. Jerome alichanganyikiwa na bila kupoteza muda alitoka Kanisani na kueleka Aghakhan Hospital iliyopo Posta.
"Mtoto wa marehemu Dada YAKO yupo hoi taabani DAKTARI amesma ana uvimbe unaomsumbua kichwani" Mama Jerome aliongea akiwa na WINGI wa wasiwasi.
"Dakta amesema zinatakiwa Millioni ishirini Ili mtoto wa Dada YAKO afanyiwe Operesheni" Mama aliongea Kwa uchungu.
"Kama ujuavyo Jerome sisi ni masikini HATUNA hata senti Tano ya kuwapa Madaktari wamtibie Shishi mjomba wako. Hili ni pigo kwetu yamkini Mola anatujaribu. Mama yake Jerome alilia.
"Mama MPENZI wewe na Mimi tunampenda sana Mjomba Shishi, tatizo lake limetoke ghafla kwa bahati mbaya ninatamani sana kusaidia lakini pesa nyingi nimezitumia kwenye maandalizi ya harusi yangu. Nifanyeje mama jamani?"Jerome alihuzunika
"Sijui mwanangu, sijui tufanye Nini? Je, hauna rafiki mzuri umuazime Pesa baadaye ukifanya kazi kwa bidii utamrudishia"Mama alitoa wazo. Jerome aliinama chini kutafakari baada ya dakika nyingi kupita alimwambia mama yake.
"Nipe saa chache nijaribu maombi Kwa watu muhimu." Ikawa hivyo basi Jerome hakutokea kwenye harusi yetu.
#####
"Hallow Baba mkwe" Jerome alimpigia simu Dady.
"Hallow nani mwenzangu?"Dady hakuisave nambari ya Jerome aliitupilia mbali, alimuona Jerome kama mtu anayemchechefua.
"Ni mimi Jerome, mchumba wa Shelidani." Alijitambulisha
"Unachangamoto Gani kijana? Dady hakutaka hata kutanguliza salamu.
"Kwanza Shimamoto Baba."Alimsabahi.
"Salamu sio chakula nikala na kushiba.... Embu ongea kiutu uzima. Dady alijibu jeuri Kwa mkwewe asiyempenda.
"Ninashida Baba ninaomba msaada wako nipo chini ya miguu yako." Jerome alishindwa kujieleza.
"Huna meno, huna ulimi hauwezi kutamka? Ongea kiume."Baba alimkaripia Jerome ambaye alivumilia kauri zinaovunja MOYO.
"Mtoto wa marehemu dada yangu amelazwa Chumba Cha wagonjwa mahututi yaani ICU Hospitali ya Aghakhan, Posta. Anatakiwa kufanyiwa Operesheni ya haraka, Uvimbe unamsumbua kichwani. Ninaomba msaada wa mkopo shilingi millioni ishirini maana gharama nyingi nimezitumia kwenye maandalizi ya harusi yangu,"
'Teh teh teh' 😂😂🤣 Baba mkwe alicheka.
"Harusi YAKO inanihusu Nini Mimi?"Aliuliza Kwa kebehi.
"UNATAKA msaada wa pesa za Bure.....Aaah kijana hakuna cha bure Duniani. Embu njoo kesho asubuhi haraka sana tupige Dili," Baba alimwambia Jerome. Siku ile ilipita PASINA Jerome wangu kufika Kanisani. Aliniacha NJIA panda mie niliyechekwa na watu walionishangaa kuachwa na yule nimpendaye.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Ngrii ngriii ngriii☎️📞 simu iliita, nilishituka usingizini na kuicheki nikitegemea ni MPENZI wangu Jerome akinipigia lakini kumbe sio Jerome Bali ni Baba. Sikua na Raha Wala furaha Kwa jinsi nilivyolia usiku KUCHA juu ya Jerome liyenishangaza Kwa ahadi feki ya kunioa.
"Hallow Shelidani naomba saa SITA mchana uje Ofisini kwangu Nina maongezi na wewe." Wakati Baba akiongea ilikua ni saa mbili asubuhi.
"Sawa baba nitakuja."Moyoni nilijilaumu kwanini sikumsikiliz Dady aliponiambia Jerome sio mtu wa kunioa.
'Oh my God embu ngoja niende asubuhi hii nikamsikilize Dady" Nilipata wazo la kuondoka asubuhi hata kabla saa SITA tuliyokubaliana haijafika. Nikakurupuka kutoka kitandani na kuingia bafuni kukoga. Saa tatu asubuhi nilikua nimeshafika Ofisini kwa Dady lakini Toba! Kabla sijaingia Ofisini kwenye vioo vya Ofisi ya Dady nilimwona Jerome mchumba wangu aliyenipa Presha kanisani. Uzuri wa madirisha ya Ofisi ile yalinipa mwanya wa kusikiliza kilichokuwa kikiongelewa.
"Hizo Millioni hamsini nimekupatia Bure sitaki unirudishie kikubwa wewe tia saini huo mkataba kwenye karatasi."Dady aliongea
"Nadhani tayari ushasoma masharti yaliyopo kwenye mkataba huo. Ni marufuku kuonana au kukutana na Shelidani, kuendeleza MAPENZI au mahusiano na mwanangu Shelidani. Huna uwezo wa kumuona mwanangu Shelidani sababu wewe ni fukara masikini." Kauri za Dady zilinishitua nikiwa ningali pale dirishani.
"Utamlisha Nini Binti yangu wewe? Utamvalisha Nini? Kula YAKO na vaa YAKO imejaa mashaka. Sikiliza kijana naomba ukae mbali na Binti yangu Mimi ndiye mwenye uwezo wa kumtafutia Binti yangu mwanaume wa kumuona mwanaume ambaye ataweza kumlea na kumpenda Binti yangu," Dady alitoa mahubiri yake.
"Aya Sasa tia Saini hapo Kisha uondoke na hayo maburungutu YAKO,"Jerome alitii, akatia Saini. Sikukubali, yote yaliyoongelewa niliyasika haraka haraka nikauvamia mlango wa Ofisi ya Dady nikaingia nikiwa na hasira, Jerome alishituka aliponiona lakini Dady alitabasamu.
"Usiisaini hiyo karatasi Jerome, tafadhali," Nilipiga kelele baada ya kuingia Ofisini.
"Oh! Nitaeleza Shelidani, nitaeleza tafadhali," Jerome aliongea
"Ueleze Nini Jerome? Nimesikia kila kitu... Jero Kwa upuuzi wako hupo tayari kuyauza MAPENZI yetu Kwa sababu ya pesa?"
"Hapana Shelidani nimepata matatizo kidogo ambayo yamekuwa magumu kwangu kuyatatua zaidi ya kuomba pesa Kwa baba YAKO. Mjomba wangu Shishi amelazwa Hospitali zinahitajika pesa nyingi Ili kumtibia" Aliongea Kwa huzuni.
"Hata kama Jerome yaani UNATAKA kuniacha sababu ya pesa? Jinsi ninavyokupenda Leo hii niambiwe unaniacha na kunitenga" Machozi yalianza kunibubujika Kisha nikamgeukia Dady nikampa vidonge vyake.
"Jambo unalolifanya sio ustaarabu Dady unayaua MAPENZI niliyofunga na mtu niliyemuweka moyoni."Niliongea Kwa uchungu
"Usinipigie kelele Sheli nafanya hivi makusudi kwa faida YAKO. Huwezi kuolewa na mtu hoe hae masikini asiye na mbele Wala nyuma," Dady aliongea.
"Kama ni masikini au hoe hae Mimi ndiye niliyempenda Dady sio wewe. Umasikini au Utajiri yote ni mipango yake Mola, hatuwezi jua kesho nzuri au mbaya aliyoipanga Mola." Baada ya kusema hayo nilitoka ndani ya Ofisi ya Dady Jerome aliyekua ameshika maburungutu ya pesa pamoja na ule mkataba alinikimbilia.
"NISAMEHE Sheli sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na masharti ya huu mkataba Ili kuokoa MAISHA ya mtoto wa Dada yangu." Aliongea
"Jerome wewe ni mwenye MOYO uliojaa ubinafsi yaani unakubali kuyauza MAPENZI Kwa sababu ya Pesa. Kwanini usiwasiliane na Mimi unieleze shida hii angarau tujue wapi tungelianzia kutatua. Ubaya wako unakimbilia kuomba ushauri Kwa Dady."Niliongea machozi yakinitiririka.
"Jana nilipokuwa kanisani nikikungoja sana Sheli, nilipigwa Simu na kuelezwa tatizo la Shihi.. haukuwepo wakati huo Sasa ningelimweleza nani shida hii?
"Hata kama Jero haukupaswa kwenda Direct kumueleza Dady juu ya tatizo hili, wewe binafsi haumjui jinsi alivyo."
"NISAMEHE Sheli" MPENZI wangu alitia huruma nikamkimbilia na kumkumbatia wote tukalia machozi.
...........
Shishi alifanyiwa Operesheni kuondoka uvimbe kichwani, Operesheni ilienda vizuri akaruhisiwa kutoka Hospitali baada ya majuma kadha hali nzuri ya Shishi ilirejea SHISHI AKAPONA
NILIMSAMEHE jEROME TUKAANZA MIPANGO MIPYA YA HARUSI BAADA YA MIPANGO YOTE KUFANYIKA HARUSI YETU ndogo ilifanyika na kuhudhuria na watu wachache SEMA Dady bado aligoma kuhudhuria harusi yetu.
Bada ya harusi yetu KUFANYIKA mie na Jerome tulikubaliana kuhama Jiji la Dar es saalam tukahamia Arusha. Niliamua kukata mawasilino na Dady Tena nilifanya uamuzi wa KUACHA kufanya kazi ndani ya kampuni ya Dady, alichokifanya yeye ni kuliondoa jina langu kwenye Documentary za Urithi wa kampuni yake. Sikujali sana mana natambua kati ya upendo na pesa Upendo unanguvu sana.
Nilibahatika kupata KAZI nyingine Jerome pia alipata kazi nzuri tukajichangachanga na kununua nyumba yetu na baada ya kujichangachanga tena tulikusanya Millioni Hamsini tukamrudishia Dady pesa alizompatia Jerome Kwa matibabu ya Shishi. Dady hakutaka Tena kunisikia sembuse kunijua
Sikujali. Tuliendelea kumove on, Leo hii tuna watoto watatu na kijacho mwingine yupo njiani kuja. Sie tunapendana pendo lililoshiba pendo lisilojali Mali, pesa Utajiri au Statasi
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
MAPENZI ya KWELI hayabagui hayachagui.
Tchao
No comments:
Post a Comment