Sehemu ya TANO
BARAZANI.
“What!? Tunahitajika mbele ya Baraza la Wazee wa mila na desturi?” Ally alimuuliza Tunu mamaye
“Yes, kama nilivyokwambia baba kasema siku ya leo tunahitajika mbele ya baraza la Wazee, juu mlima wa kidundai, ifikapo saa saba mchana kwa pamoja tuwe Barazani.” Tunu alimweleza mwanae wa kufikia Ally.
“Ni ishu gani muhimu kwa sisi kuitwa kunako mkutano wa jadi?”Ally alimuuliza mamaye.
“Binafsi bado sijajua sababu kuu ya wazee wa mila kutuita barazani, lakini kama ujuavyo mwanangu la mgambo likilia kuna jambo yanini kuandikia mate wino ukiwepo? Tujiandae mapema siku ya leo, twende tulipoitiwa, mtu hakatai wito, mtu ukataa lile aitiwalo.” Tunu alimweleza mwanaye Ally.
“Ok. Mama, wacha niwahi kuwarejesha wanyama nyumbani, mapema kabla saa saba haijatimu tutakuwa pale.” Ally alimwambia mamae wakati huo alikua akiwalisha wanyama ndani ya msitu wa Kidundai.
######################
Uwanja wa Kidundai, juu ya kilima cha Kidundai ulifurika wazee wajuzi wa mila na desturi za wasambaa, wapogoro na wabondei, kila mzee aliyekuja nakuwasili katika kile kiwanja alijitapa na kujisifu mbele ya wazee wenziwe kuwa yeye ni bora zaidi ya wengine. Wazee wale waliketi mduara katikati kuna moto mkubwa unao waka, tayari kufanya mambo yao ya kishirikina.
Miili yao, nyuso zao na mikono yao walitupia hirizi pamoja na vitu vingine vya kishirikina, ukiwatizama huwezi kuwapenda sababu mavazi waliyo vaa yalikua nyang’a nyang’a
Ngoma zilipigwa, vijana walicheza nyama pamoja na pombe vilinyweka yapata saa kumi na mbili jioni burudani iliendelea na kuishia papo hapo. Jambo lililotegemewa liliibuliwa ili lijadiliwe na kufanyiwa maamuzi, Mzee Jamali tayari alikwisha kuwakusanya Wazee wa mila wapatao ishirini na watano, tayari alikwisha waeleza dhima ya kuwaitia barazani, ajabu iliyoje hadi wakati ule bado Ally na Tunu mamaye hawakujua sababu ya wao kuitiwa mbele ya Baraza la Wazee.
******************************
“Maneno niliyonena mbele yenu, mbele ya Baraza hili tukufu Wazee wangu ni yenye ukweli thabiti, mwanangu Ally anatembea na mke wangu bibie Tunu, mapenzi yao si kificho, yapo wazi wanayaonesha mbele ya macho yangu.” Mzee jamali aliongea, akawaachia bumbuwazi Ally na mamaye Tunu, wasilijue kosa lao katika Baraza la Wazee wachawi na washirikina. Si Ally wala si Tunu aliyepata amani ndani ya mtima wake. Mara baada ya wawili hawa kusikiliza yale madai walipigwa na mshangao mkuu ina maana madai yale yalikua ni madai kutu kutoka kwenye mdomo wa Mzee Jamali.
“Je, ni kweli iliyo thabiti kusema kuwa Ally unatembea na mamayo wa kufikia ambaye ndiye mke wa babayo?” Mzee mkuu wa mila alimuuliza Ally mwana wa Mzee Jamali.
“La, asha! Mzee wangu madai yote aliyoyatoa baba m usebele zenu hayana ukweli wowote ule ndani yake, mie napinga na tena nakataa madai kuwa ninatoka kimapenzi pamoja na mama yangu.” Ally alijitetea.
Rungu lilitua mbele ya upeo wa macho yake Tunu, alihitaji kujitetea, alihitaji kukiri au kukataa kama kuna ukweli kusema kuwa anatembea na mwanaye wa kufikia Ally.
“Kamwe siwezi kuwadanganya wazee wangu na siwezi kuwapotezea muda wenu mzuri kwa kuwakusanya pahali hapa ili kuamua hatima ya madai ninayodai. Kwa ufupi ni kwamba yote niliyoyanena mbele yenu asilimia tisini na tisa ni maneno yenye kweli tupu na hiyo moja iliyobaki mie ninawaachia nyie wazee wangu mfanye maamuzi yaliyo sahihi juu ya haya yote niliyoyanena.” Aliongea Jamali, aliongea kwa kujiamini zaidi.
Wazee walimsikiliza mtu wao na sasa hatua iliyofuata ilikua ni kutenda kwa matendo yaliyo dhabiti kama wajuavyo wao binafsi mkono mtupu haulambwi, maneno matupu hayavunji mifupa, imani bila matendo ni imani iliyo kufa. Walihitaji kuhakikisha kama maneno ayanenayo mzee Jamali yana ukweli ndani yake.
“Sisi kama Wazee wa mila za wasambaa, wabondei,wapare na wapogoro, tunao mababu zetu, tunayo Mizimu yetu tunao wazee wetu, Miungu, Mashetani, Pepo na roho waovu, tunawaheshimu sana hao wazee watupao mvua wakati wa wa ukame, watupao chakula wakati wa njaa, wanaotulindia watoto na mifugo yetu, wao ndio wanao ujua ukweli na uwongo wa mtu,na sasa tunaelekea kushusha maombi yetu mbele ya mikono yao, masikio yao pamoja na hisia zao.” Mkuu wa mila aliongea.
“Wazee wetu sio wazee wa kutumia makisio ya mambo, wao ndio wanao jua uthibitisho juu ya tendo na tukio, kuna adhabu juu ya mtu atakaye gundulika kuwa hasemi ukweli ama hawasemi ukweli, maneno yake au yao ni udanganyifu juu ya yote yaliyo kubaliwa hapa.” Mkuu wa mila aliendelea kuongea.
Wazee wetu wanaifahamu adhabu itakayo tolewa juu yenu enyi wanafamilia, adhabu itakayo tolewa na mizimu yetu, pepo na roho waovu, ipo wazi, ni adhabu ya uasherati, adhabu ya usaliti, adhabu ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa . Hatia ijapomdondokea mhusika ajihesabie kuwa ni mwenye janaba, atageuka mwili wake nao utakuwa nusu binadamu nusu mnyama wa kufugwa hiyo ndiyo adhabu impasayo huyo mja mdanganyifu na huo ndio ukweli na umadhubutu wa yale ambayo mila na desturi zetu zinapaswa kufuatwa.” Mkuu wa wale wazee aliongea.
Si mzee jamali, Ally na mamae wa kufikia Tunu aliyeingiwa na wasi wasi juu ya maneno yale yaliyotamkwa na wazee wa mila, mzee Jamali alijihaminisha moyoni akisema leo ndio leo msema kesho mwongo ni lazima wale wawili walioukeketa moyo wake wapewe adhabu yao, adhabu kari tena kari sana. Ili wapate funzo kutokana na matendo mabaya yanayo ukwaza mtima wa mzee Jamali.
Yanini mzee Jamali auhumize moyo wake ikiwa mali ni ya kwake yeye mwenyewe, mali yake inaliwa mikonono mwake? mbele ya macho yake,hapana asijeitwa ‘babu jinga inama ufikirie mali yako inaliwa.’
Ally na Tunu hawakuwa na hofu wala wasi wasi, walitoa idhini mambo ya jadi yafanyike ili harobaini za mwivi zikamatike mapema iwezekanavyo, wao binafsi hawakujiona iwapo wana hatia japokuwa ile hali ya mzee Jamali kuwaita mbele ya baraza la wazee wa mila pasina kuwaeleza kwa kinagaubaga kwamba hapendezwi na urafiki wa wawili hawa, urafiki ulio pitiliza ,walishituliwa kwa hilo, wao binafsi wanafahamu juu ya mila za jadi yao, wanajua fika kuwa mila za jadi yao ni mila korofi, wanafahamu ukorofi wa Pepo,Mizimu, Ibilisi na roho wengine waovu.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment