Friday, October 4, 2024

KUCHEPUKA SIO dili. ...5



Sehemu ya tano

 ANAMWAGA UNGA.

                   “Mambo vipi Asha Secretary wangu.” Mawe alimsabahi asha

                   “Poa tu bwana mawe, habari za huko utokako?”

                   “Asubuhi mashallah kwetu wagonile, hawajambo, ni  bukheri wa afya,” mawe alijiandaa kuingia ofisini kwake.

                   “Samahani bwana mawe” Asha alinyanyuka pale alipoketi ameshika bahasha mkononi.

                   “Bila samahani bibie.”

“Bosi amenipatia huu mzigo ameniambia nikukabidhi.” Asha alimkabidhi Mawe ile bahasha kubwa yenye rangi ya kaki.

                   “Tena bosi ameniambia urudi nyumbani kwako, asingelipenda kukuona tena ukiwepo maeneo haya.” Asha alimpasha Bwana mawe.

                   “kuna nini tena mbona ni kama vile sielewi elewi bibie”

                   “Mie binafsi sijui kinacho endelea.”  Asha alimjibu bwana Mawe kwa ufupi. Mawe alitii lile agizo, alitoka nje ya ofisi akaenda kuketi nje kunako  mti mkubwa wa mnazi, mawazo yalimfunika moyoni.

                    “Nimefanya nini mim jamani hata niambiwe sitakiwi tena  ofisini siku ya leo, kosa langu nini jamani?” Aliwaza bwana mawe wala asipate jibu. Ya mawazo yake mara ile aliinuka pale alipoketi naye akaelekea nyumbani kwake kama kawaida alipoingia chumbani kwake alifunga mlango naye akaifungua barua aliyopewa na secretary Asha.

                    Barua ile ilimtaka asirejee tena kazini wala asiguse tena ofisini, machozi yalianza kumbubujika bwana Mawe, Keisha timuliwa kazini, kazi nzuri yenye mshahara mnono looh! Ataishije yeye na familia yake? Ukitegemea kazi ni maisha bila kazi maisha yake yangekuwa mashakani. Alilia sana bwana Mawe. mkewe aliingia chumbani na kumkuta mumewe ni mwingi wa majonzi machozi na masikitiko.

                    “Eeeh! Mume wangu una nini leo mbona unalia.” Alimuuliza mumewe kwa mshangao, sababu wahenga walisema ukimuona mtu mzima anamwaga chozi juna jambo limemgusa.

                    “Embu niache huko.” Mawe alimjibu mkewe kwa hasira, Mkewe hakufa moyo alihitaji kulijua tatizo linalomsumbua mumewe.

                    “Mume wangu una nini siku hizi? Mbona umebadirika sana laazizi? Siku hizi haunisikilizi kama awali, siku hizi hauoneshi mapenzi yeyote kwa wanao, umegeuka mbogo, haungalii ni wapi unapokose, nijapokuambiua haunisikilizi, kwanini mume wangu? Baya zaidi nimepata habari kuwa una Vingasti, unavipa hela huko bar, umekuwa mzinifu, haueleweki eleweki kama mtu na familia yake.”

                    Maneno yale yalimwingia bwana Mawe kichwani mwake, kwa upole na kwa unyonge alianza kumuomba mkewe msamaha.

                    “Nisamehe mke wngu.”

                    “Nikusamehe kwa lipi jambo?”

                    “Nimefanya maovu mengi ya kukusaliti wewe mpenzi, kutokana na  usaliti huo kibarua changu kimeota nyasi……” Mkewe alishituka kidogo kisha akanena.

                    “Una maanisha nini mume wangu?”

                    “Nimemwaga unga mke wangu, nimefukuzwa kazini,  kuanzia leo mimi sio mfanyakazi wa ile kampuni.”

                    Mkewe angali amepigwa butwaa. Tama shavuni, akasema kwa majonzi              “Mungu wangu we! Mume wangu sasa sisi tutaishije, ukitegemea kazi yangu hii ya kuuza mboga mboga na matunda ni kazi ya kubahatisha bahatisha, pesa yenyewe ndio hiyo tena mlo mmoja kwa siku.”

                    “Dah! Mke wangu, majuto ni mjukuu, fuja mali kufa kwaja, yatupasa tuanze kupambana na hali zetu, nitakuongeza mtaji kwenye biahara yako nami nitaendelea kutafuta kazi ya kutusaidia kuboresha maisha yetu.”

                    “Sawa mume wangu.”mkewe Mawe aliitikia moyoni mwake akijisemea mwana umleavyo ndivyo akuavyo, mtegemea nduguye ufa masikini,tamaa mbele mauti nyuma, mwenzio akinyolewa zako tia maji, mfaa maji haeshi kutapa tapa, shika mawili moja litakupokonyoka.”

                    “Eeeeh! Na vipi kuhusu hivyo Ving’asti vyako “

                    “Ndo maana nilianza kukuomba msamaha mke wangu, Ibilisi alinipitia ninakuahidi sintarudia, nami nitabadirika mabadiriko makuu.”

                    “Sawa mume wangu, ninaomba haya yasijirudie tena, achana na hao vimada wanakulia pesa, hawakupi faida zaidi ya hasara tupu jambo muhimu ni kuipenda na kuijali familia yako jua kwamba mimi ninakupenda sana mume wangu.

Wawili wale waliongea kwa muda mrefu sana na baada ya maongezi yao Mawe alimpatia mkewe kitita cha kuendeleza biashara ya mboga mboga, nyanya vitunguu na matunda hata hivyo maisha yao yaliendelea kuwa magumu kila uchao. Mawe amekonda na kudhoofika amekuwa ni mwingi wa kujilaumu, anawaza maisha bora aliyokuwa nayo zamani, zama zile alizokuwa na mshahara mnono. Ubaya wake amefuja mali kifo kimemgoja anasikitika akijisemea  ama kweli kuchepuka sio dili.

         *******************************

                       MWISHO.

                                                                          


No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...