Saturday, October 5, 2024

IM SORRY MR. TRUMP.

 

Nilikua namchukia
Sio kwa sura au mwonekano wake
Bali kwa matendo yake
Trump.

Nilimuona kama mtoto
Realy alikua mtoto
Tena mtoto mwenye utoto
Nilimchukia


Anipige
Anisukume
Anivute nywele
Anikemee
Bila sababu
Nilimchoka👿

Siku Moja
Mimi Agi, Dolla na Linda
Marafiki zangu
Tukipata mlo
Akajipitisha
Aliponiona
Akafanya madoidoi yake
Makusudi tu, akaibonyeza meza
Yetu ya chakula
Chakula Cha bei gharama
Kikamwagika

Nilimchukia
Sio hivyo tu
Mtu wa hovyo Trump
Darasani nilikosa furaha
Raha na amani
Sababu ya matendo yake
Ya hovyo.
Si mnamuona?
Anaburuta nywele zangu
Kwa furaha na kejeli
Kama haoni maumivu yangu.
Shit!
Anafanya kunipiga juu kichwani
Nahisi maumivu
Nyota nyota machoni
Nilikasirika
Hapana, uvumilivu una kikomo chake
Nimemvumiliavya kutosha
Sasa lazima nimfunde
Kwa vitendo.

"Kula kofi hilo, mavi ya kuku wewe"

Puuu
Puuu
Puuu

Nilimpigia juu ya kichwan chake
Aliumia
Akatimka
Mwendawazimu yule

Safi sana
Wavulana lazima wawaheshimu wasichana
Wajue sisi pia tuna hisi na hisia na maumivu

Mshenzi yule!
Tuone kama atarudia tena
Leo Bahati yake.

Mungu baba!
Nimeshituliwa na habari hizi mtandaoni
Siku ya Leo, siku mbaya.. Bad day!
Habari zinasema
Trump yupo Hospitali
Amepasuliwa juu ya kichwan... Opereshen🙆‍♀️
Ubongoni

Eti damu imevujia ubongoni
Jesus!!
Mtume!!


Si ni mimi ndie niliempiga kichwani!!
Hizi habari au ndoto!
Wamemnyoa nywele na kumshona kichwan
Uwii!
Nimeogopa mimi Agi.
Siku zilivyozidi kwenda
Taarifa zikamininika kutoka Hospitali
Trump Yu hoi, taabani, mahututi

Nilichanganyikiwa
Nikajiona labda mm ni mkosaji
Maana kwa hasira nilimponda kichwani
Ni mm ndie niliesababisha kichwa chake kivilie na kivuje damu
Jamani!
Habari zikavuma
Trump yule Mkorofi wangu
Hatunaye tena Duniani
Uwiii😭😭
Machozi yakanibubujika
Huzuni ikaniparamia
Kifo kiogope
Mkorofi wangu akazikwa
Akalala pekee
Kwenye giza
Huzuni na upweke.
Mimi nikiendelea kulia
Na kupiga kelele
Juu ya kaburi lake

I'm sorry Trump😭
I'm sorry Trump😭
Please forgive me😭
Sikudhamiria
Sikujua kama itatokea hivi
Sikujua Mkorofi wangu

Mungu akulaze pazuri pema.


Najiona mkosaji

😭😭😭😢🙆‍♀️

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...