Friday, October 4, 2024

KUCHEPUKA SIO dili... Sehemu ya 3




Sehemu ya tatu

ONYO.

                  Asha alikua yupo bize ana ‘typing’ mara baada ya kumuona Bwana Mawe amekuja shagalabaga, moyoni alimcheka, tai haikufungwa vema, shati lake jeupe halikufungwa vema, kifungo kimoja juu kingine chini, mkanda wa suruali uliachwa  haujakizunguka kiuno cha yule mwanaume, juu ya nywele zake kuna chanio, chanio hilo limeshikilia nywele zake.

                  “Vipi Asha bosi amefika.” Leo mdomo wa bwana Mawe ulitoa denda la ajabu.

                  “Ndio amefika, lakini mbona leo umechelewa namna hiyo? Alafu umekuja nyang’a nyang’a? Embu jitizame kwenye kioo kilicho juu ukutani.”         Asha alimwambia yule mwanaume kijana ambaye hakuweza kulijibu lile swali la kwanza kuulizwa alitii lile agizo la kujitizama kwenye kioo.

Loo! Mawe aliona aibu kwa mwonekano ule juu ya kioo, haraka haraka alikimbilia bafuni, bafu lililo nje kidogo na Ofisi yao, huko akajiswafisha swafisha kwa kuukosha mwili wake, kujipaka mafuta, kujipulizia marashi, kusafisha kinywa na kuzichana nywele zake. Mara baada ya dakika 40 alijitizama kwenye kioo kilicho ndani ya bafu lile, akajihesabia kuwa safi salama.

              “Wacha sasa niingie Ofisini kwa bosi, Bwana mawe akiwa nadhifu wa kupendeza aliongea na Secretary.

              “Samahani bwana Mawe.” Mrembo Asha aliongea.

              “Bosi yupo kuongea na mgeni.”

              Eeeh! Mfyuuuu, mawe aliubetua mdomo wake kuashiria kuwa hajapendezwa na ujio wa wageni hasubuhi na mapema.

             “Ni mgeni gani huo?” Alihoji.

             “Ni yule mwekezaji ambaye jana wlipanga wakutane Kipepeo Hoteli,”

             “Ok. Sawa…..Mmmh! akiisha toka naomba nipigie simu, unishitue ili nije kunena na bosi wangu.” Mawe aliongea wakati huo huo tayari amekwisha elekea kunako mlango wa Ofisi yake ili aendelee na kazi.

             “Poa!” Asha alijibu kimkato. Baada ya kupita masaa mawili, Asha aliuinua mkongojo wa simu ya Ofisini akimtaarifu bwana Mawe kwamba yule mgeni tayari amekwisha ondoka, Nafsi ipowazi kwa Bwana Mawe kuongea na bosi. Bwana Mawe alielekea moja kwa moja Ofisini kwa bosi wake. Bwana Viviani Vladimili ni mtu mzima mwenye umri wa miaka hamsini na ushee, ameketi ofisini kwake, anachora chora kwenye karatasi iliyopo juu ya meza yake

               “Karibu sana Bwana mawe, karibu keti kitini,” Bosi alimkaribisha Mawe.

              “Asante sana bosi, ninashukuru kwa ukaribisho,” Mawe aliketi kitini.

             “Eeh, una shida gani mawe niweze kukusaidia.” Bosi alisahau kutanguliza Salamu.

                 “Habari za tokea juzi, pole na majukumu, jana hatujaonana kabisa bosi wangu.”

                 “Nzuri sana Bwana Mawe, Nimepoa kimajukumu, lakini hata hivyo jana nilitoka nje kikazi, ndio maana Jana hatujaonana.”

                 “Ok. It’s good to hear from you,” M awe aliendelea kunena.

                 “Jana nimepokea ujumbe wako kutoka kwa Asha Secretary lakini kwa bahati mbaya sikuelewa vizui ulikua una maanisha nini bosi wangu..” Mawe alihitaji kujua.

                 “Aaah! Si wewe umeoa!?

                 “Ndio bosi wangu.”

                 “Vema, embu nieleze siku zote tunatoka kazini saa ngapi?”

                 “Saa nane bosi wangu.”

                 “Na wewe mara baada ya kutoka hapo uwa unafika nyumbani saa ngapi.?”

                 “Saa kumi  na mbili bosi wangu.”

                 “Are you sure, una hakika na unacho ongea? Bosi alikua na shaka.

                 “Nina uhakika bosi.”

                 “Haki ya Mungu!!” Bosi alitilia mkazo, Mawe alishindwa kuendelea kunena, akatizama chini kidogo, ndani ya sekunde chache alijibu.                

                 “Jana nilichelewa kutoka, sababu nilikua nikikusubiri, ili tuje tuongee suala hili.”

                 “Sawa hilo halina tatizo na pale Buzi bar, daima waenda saa ngapi?” Mawe alipigwa na butwaa asitake kuamini kama bosi wake amekuwa akimfuatilia hadi Buzi bar, Ukitegemea  Buzi bar ipo vichochoroni  na kwenye vificho, bar hiyo ni yenye hadhi ndogo kwa watu wa daraja la chini sio jambo la kawaida kumuona mtu kama bosi wake akinywa matapu tapu.

                  “Mbona haunijibu, hilo mimi nanalijua sana, daima nmekua nikikuchunguza, kila ukitoka hapa kazini, nisingelipenda ujieleze sana ila ningeliomba ujirekebishe na utimize majukumu yako wewe kama baba mwenye familia.”

                  “La..La…La…La….Lakini bo…siiii” Mawe alikamatwa na kigugumizi.

                  “Mbona umekamatwa na kigugumizi, ok. Embu nenda ukaendelee na kazi zako za kiofisi.”

                  “Sawa bosi.” Mawe alirudi ofisini kwake akiwa na mawazo chungu nzima , siku ile alifanya kazi mdogo mdogo naye akapitiwa na usingizi kisha akadozi. Alipokuja kushituka ilikwisha timu saa nane kamili, pasina kuchelewa. Mawe alifunga kazi.

                  “Duh! Ama kweli kulala  noma, yaani nimelala kwa muda mrefu haswa, wacha nifunge  kazi, kwa leo, halafu kesho niwahi mapema bwana Mawe, aliongea yeye na moyo wake,mawazo yalimzoga kichwani akajikuta anasahau ushauri aliopewa na bosi wake. Pasina kutarajia alijikuta anadondokea Buzi  bar bar ambayo Bosi wake alimwambia hapo awali kamwe asijaribu kuigusa, asipite wala asifanye mazoea ya kwenda hapo, kamwe asiendeleze tabia ya kukesha na kushinda bar.

                  Bosi aliongea hivyo kwa kumtaadharisha kwa sababu ulevi wake ulikua ni chachu ya utendaji mbovu kazini, mbovu usiotamanika, ulevi wake ulimfanya mara nyingi ashindwe kufanya kazi kwa bidii na matokeo yake sasa akawa ni mtu wa kuchelewa kufika kazini, mtu wa kulala ofisini akiwa amechoka kutokana na kukesha bar, mtu wa kuja hovyo hovyo na kumtia aibu bosi wake mbele ya wageni waliomtembelea huyo bosi.

                                 ******************* 

 


No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...