I miss you Lupita
Usiku wa siku ile ulipita, ulipita na kuniachia mawazo mengi Mtimani, nilikuwa nikifikiria labda nimshawishi mke wangu Lupita tukapime vipimo vya DNA, ili tupate kujua uhalisia wa yule Mtoto, wazo hili lilikuwa ni wazo jema fikirani, nami nikajiapiza kumweleza Lupita ifikapo jioni ya kesho nikirejea kazini nayeye pia akiwa free.
Asubuhi ya siku iliyofuata nilikuwa bize kuwasafirisha Raia wa kigeni ambao walikuwa wakisafiri kuelekea ZANZIBAR hivyo basi nilihapa kama nitarudi salama sina budi kumweleza Lupita juu ya wazo langu, wazo la kwenda kuchukua vipimo vya DNA, tuchunguze damu na chembe chembe za urithi ili kuthibitisha kama huyo mwana anayeleta gubu ndani ya familia ni mwana wangu au ni foto kopi.Safari yangu ilikuwa ni Safari njema, sababu mimi ni Lubani na tena ni Lubani mbobevu nina EXPERIENCE, nimefanya kazi ya ulubani kwa zaidi ya miaka saba, nimtu tumaini ndani ya Nchi ya BARA hainipi tabu kuiongoza AIR BARA kwenda Zanzibar, Tanzania na kunirudisha tena BARA, AFRIKA YA KUSINI.
Nilipokwisha kutimiza wajibu wangu, nilirudi nyumbani nikatimize wajibu wangu kama baba katika familia, Zawadi tele nilizokua nazo mkononi mwangu zilikua ni maalumu kwa wanangu wapenzi Maliki-shua na huyu mwingine aliye leta gubukatika familia, SEBA ndilo jinale
Dereva wangu alinifikisha nyumbani yapata saa kumi na mbili mida ya jioni mara baada ya kuingia nyumbani nilipitiliza moja kwa moja chumbani kwa mie na wangu Lupita, sikumkuta wala sikumuona Mtoto Seba, nilijua yawezekkana Lupita ametoka na mtoto Seba. Lakini mmmh! Ametoka na kwenda wapi Jioni ile? Maswali yalinisumbua, sikupata majibu.
“Baba, baba, baba.” Ilikuwa ni sauti ya mwanangu mpendwa wa moyo wangu Maliki-Shua aliingia chumbani na kunikuta mie juu kitandani nikiwa na mawazo tele.
“Oooh my son Sweet Love Maliki, how are you Baby?”
“ I’m good Dady.” Maliki aliniitikia maendeleo yake kitaaluma ni mazuri, ana akili nyingi sana, akili nyingi alizozochukulia na kurithi kutoka kwa mama yake Lupita.. maana kw jinsi nijuavyo Historia ya mke wangu Lupita tangu akiwa Primary School, Sekondary hadi Universty alikuwa akishika nafasi ya kwanza kwenye matokeo yake ya Mitihani.
“Thanks very much my dear Son Maliki, mama yako yuko wapi?” Nilimtua chini Maliki kutoka juu ya mikono yangu niliyomnyanyua kwa mapenzi yangu yote.
“Mama ameondoka muda si mrefu ni nusu saa, kuna gari moja zuri imekuja kumchukua, amembeba Seba akaniambia ati harudi tena, amenipatia barua hii amesema ati ukirudi nikupatie.” Maliki aliongea naye akaingiza mkono wake kwenye mifuko ya suruali yake akatoa kipande cha karatasi iliyokunjwa vizuri nami nikaipokea kutoka kwa mwanangu Seba nikaifungua na kuanza kusoma nini kilichoandikwa ndani yake.
Mpenzi mume wangu Mika,
I’m so sorry, nimeamua kuondoka nyumbani na kukuachia Jukumu zito la kumlea mwanetu Maliki-Shua,mpenzi nisamehe kwa sababu nimefanya uamuzi wa haraka, uamuzi wa kulivua pendo ulilonipenda sana maishani. Nisamehe sana mpenzi sikuwa mwaminifu kwako ndio maana hata Seba mtoto niliye mzaa miezi michache iliyopita ameleta gubu ndani ya nyumba yako.
Nisamehe mpenzi, kwa yote mabaya yatokanayo na mie kutokuwa mwaminifu kwako. Ninajua uliniamini na pia uliamini kuwa mimi ni wa kwako Forever, sikupata kukuonesha darili zozote zile kwamba ninaye mwanaume mwingine pembeni.
Mika, Seba sio mtoto wako, Seba sio damu yako, Seba ni mtoto wa mtu mkubwa sana Serikalini, mtu huyo ni mtu mwenye cheo chake, ni mtu mwenye uwezo wake, haki, hauwezi kumletea nyodo au kumfanyia chochote kile cha kumdhuru na hata hivyo ninajua fika kwa upole ulionao hauwezi kamwe kufanyia jambo lolote lile baya RAISI ANTONIO bali utabaki hivyo hivyo ukisikitika na kuhuzunika.
Mpenzi unisamehe sababu sijutii uamuzi wangu wa kuishi na Raisi Antonio, sababu ameniahidi maisha bora mazuri na yenye fahari, sio kwangu tu bali pia kwa mwanangu Seba. Raisi ameniahidi utajiri mwingi ulio ndani ya nchi ya BARA kuwa atanipa mimi na wanangu Seba. Ameahidi kunipatia vyeo na madaraka mbali mbali hapo baadaye, nami nimefurahia na kuridhia ndio maana nimesema sijutii uamuzi wangu wa kukuacha wewe na kwenda kuishi na Raisi Antonio.
Mapenzi yangu mie na raisi Antonio yalikuwa ni mapenzi yenye siri kubwa sana, Sikutaka kukuambia maana nilijua fika kuwa maji yakimwagika hayatazoleka lakini acha nikwambie, mwana sio riziki yako, ni sawa sawa na kusema kitanda kimeza haramu,damu sio yako. Baki pamoja na mwanetu Maliki –Shua nami nitakuwa naja kukutembelea wakati wowote ule nikijisikia.
Sina mengi ya zaidi labda niseme Asante sana kwa kunipenda, ile pete uliyonivisha siku ile ya harusi yetu ipo ndani ya kabati kubwa la nguo nimeivua sioni thamani ya kuivaa tena. I’m sorry, I’M sorry Mika LET ME GO ( Acha niondoke) mazuri niliyo ahidiwa siwezi kuyaacha, ndio sifa ya mwanmke, mwanmke ana moyo wa kutamani na kuyapenda mazuri ya dunia.
Wahenga walisema, bahati haiji mara mbili mbili, nikichelewa au kuikataa bahati hii ninajua fika kuwa nitajuta maishani mwangu mwote, siwezi kuiacha hii bahati nasibu.
Nisikuchoche Mume wangu wa zamani acha niishie hapa hapa, SO LET ME GO NOW ( hivyo niache niondoke sasa.)
Yours,
wa zamani
LUPITA ANTONIO.
Yallah! toba, almanusura niuanguke chini na kuzirai mara baada ya kuusoma ule ujumbe, ujumbe alioniachia mke wangu Lupita Machozi yalinijaa ndani ya macho yangu lakini hayakutaka kudondoka
Kumbe mabadiriko yale yote ambayo mke wangu Lupita alikuwa akiyaonesha kwangu hayakuwa bure. Kumbe kunichukia kwote kule alikonionesha Lupita hakukuwa bure, lo! Masikini mke wangu Lupita, nimemfanyia nini mimi hata afikie hatua ya kuniacha na kuolewa na mzee mzima mwenye umui sawa na babu yake.
Masikini! Machozi yalinidondoka mbele ya mwanangu mpenzi Maliki Shua, nilishindwa kujizuia nililia mwanangu akinishangaa kulikoni mie babaye nilie bila kupigwa, Si unajua tena watoto hujua kuwa apigwaye ndiye ulia.
Nilimchukua Malik-Shua na kumpeleka Sebuleni, nikasingizia kuwa kichwa kinaniuma, nikamfungulia Chaneli moja inayoonesha vikatuni kwenye Televisheni kisha nikamzingua kwa kumwambia mwanangu ninafika dukani mara moja kuchukua dawa ya kichwa. Nilimzingua ukweli ni kwamba nilichanganyikiwa nikafikia uamuzi wa kwenda malango ya Ikulu, ili nimfate mpenzi mke wangu Lupita.
Itaendelea
No comments:
Post a Comment