SURA YA KWANZA
Amina kiguu na njia ni binti mwenye umri wa miaka kumi na misaba, anasoma Shule ya Sekondani Benja iliyopo Ilala Dar es Salaam, yupo kidato cha tatu sasa, lakini Amina hapendi masomo amejiingiza kwenye tabia mbaya ya kupenda penda wanaume. Familia yao Amina ni familia ya watu duni wenye kipato cha chini, hawawezi kumudu gharama mbali mbaIi za kuyaendesha maisha japo wanavumilia.
**************************
DARASANI
Jumatano ya leo Mwalimu Grace ameingia darasani, leo ni kipindi chake, anafundisha somo la Kiswahili, kwa bahati nzuri leo Mwalimu Grace hafundishi, bali anaandika Notes, wakati huo huo Amina aliyeketi na rafiki zake wawili Anna na Suzanna alianzisha maongezi.
ANNA: (Anayaanzisha maongezi). Shoga yangu jana kwenye ngoma ya SINGERI vigodoro ulienda?
AMINA KIGUU NA NJIA: Mwaya, nikose tena mie kiguu na njia, Jiji lote hili nafahamika, nenda Kimara uwaulize 'mnamfahamu Amina Kiguu na njia?' Watakujibu 'ndio tunamjua,' Nenda Ubungo, nenda Kigamboni, Nenda Gongo la Mboto, nenda Buguruni,. Kote huko mie ni mtu maarufu, najulikana kama vile Jua linavyojulikana. (Anajifanya kama anaandika Notes kumbe haandiki).
ANNA: Wacha we, si ungelitupitia hata sie wapambe wako?
AMINA: Mtanisamehe bure, lakini mwaya wacha nisikufiche, bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi, nimekutana na Jibaba huko huko kwenye ngoma za vigodoro, mwaya limenitunza mihela hiyo eeeh! Linatoa tu kama vile mashine ya ATM.
ANNA: Mmmh! Mwenzetu, mbona bahati hiyo, usiicheze, ikiondoka hiyo, kamwe haiwezi kurudi tena, hembu niambie jina la hilo jibaba.
AMINA: (Anajifanya kufikiria.) Silikumbuki vizuri shoga yangu ila nakumbuka utafikiri liliniambia linaitwa Zee la Puta puta.
ANNA: (Anashtuka kidogo). Mmmh! Hilo jina utadhani nimewahi lisikia!
AMINA: (Anapaza sauti kidogo). Wapi? Aka! Babu we, nisiibiwe mali yangu, naitunza kama vile ninavyotunza j
mboni ya jicho langu.
SUZANNA: (Suzanna aliyekuwa akiandika akaingilia kati yale maongezi yao). Jamani nyamazeni mwalimu anatoa material, si mnajua kuwa mitihani ipo karibu, tuombe Mungu tuingie kidato cha nne kwa furaha.
Anna: (Anamjibu Suzanna kwa kebehi). Huyu naye anajidai na kujiona kama ndiye msomi sana, utadhani elimu yake anasomeshwa kwa michango ya wanakijiji.
Suzanna: (Anachukizwa na maneno aliyoyatamka Anna). Sio hivyo rafiki zangu, muhimu kuzingatia masomo, muhimu kuzingatia mafunzo atoayo mwalimu. Elimu ndio ukombozi wa mtoto wa kike, hizo fedha mnazowaza zitawafikisha pabaya. (Anaongea kwa sauti ya chini).
AMINA(anabetua domo kwa hasira) Nyoo! Ati zitatupeleka pabaya, wapi hapo pabaya? Kwa kifupi elimu bila pesa hiyo sio elimu, hivyo basi pesa kwanza elimu baadaye.
ANNA: Mwambie huyo anajidai kiziwi.
SUZANNA: Kufuru tupu, mkumbuke kuwa pesa ni maua, sifa yake ni kuchanua na kusinyaa, elimu ni utajiri na urithi wa maarifa. Bila elimu hizo pesa wala zisingekuwepo.
ANNA NA AMINA: Mmmh! (Wanaguna wasipate kumjibu Suzanna ambaye anaendelea kuandika Notes).
ANNA: (Anamsonga Amina) Eeeh! Tuachane na huyo msomi Kasuku anajiona yeye ni bi safi sana hapa shuleni. Ok. Shoga yangu endelea na stori, ikawaje hilo jibaba kukumwagia mvua ya mapesa.
AMINA: Mwaya, ukisikia kulala masikini na kuamka tajiri ndio huku, zee lile limenipatia Promisi ya nguvu, eti kila siku mimi na yeye tukionana tu litafanya juu chini kuniachia shilingi laki moja na nusu ya vocha…” (Hakumaliza kuongea, Anna alidakia).
ANNA: Akupe shilingi laki moja na nusu hiyo simu unayo?
AMINA: Tena umenikumbusha (Anauchukua mfuko wake wa madaftari wenye daftari, anaitoa simu kisha anamwonesha Anna). Na hii simu lile jibaba limenipatia kama zawadi ya kuwasiliana naye.
ANNA: Waoooh! Ama kweli buzi hilo ulilolipata mbona linachunika. lichune hadi libakie mifupa. (Anafurahia, wakati huo huo mwalimu Grace anaelekea kufuta ubao).
AMINA: Hiyo laki moja na nusu ni ya kununulia vocha tu, je, nikiliomba hela ya nguo na viatu itakuwaje tena?
ANNA: Teh!Teh! Teh! Teh! Kantangazee! (Anacheka, wakaendelea na masimulizi yao, na hatimaye muda wa kile kipindi ulifikia tamati, kengere ya mapumziko iligonga, wanafunzi wote waliruhusiwa kwenda kujipumzisha kiakili, kimwili na kisaikolojia).
Amina akiwa anaramba ramba Koni, mara akapita kijana mmoja aitwaye Beni, Beni ni kijana anayekaribia kumaliza kidato cha nne, mara kwa mara amekuwa akimwangalia Amina kwa jicho la Huba, hata hivyo mdomo gundi alionao hawezi kumtamkia Amina, daima alikuwa akimumunya mumunya maneno na hatimaye ububu umpande kinywani mwake. Leo ameona heri ajikaze kiume, ayatoe yale yaliyo moyoni mwake.
BEN: (Anamsalimia Amina). Mambo vipi dada Amina.
AMINA: Poa tu kaka Beni, nashukuru sana juzi ulinilipia nauli kwenye ile
Daladala, jamani yule konda angeniua mie, yaani sijui nilipotezaje nauli yangu. (Anatoa sababu na kucheka cheka).
BEN: Kawaida mbona, tena leo nimekuletea shilingi elfu moja. (Anampatia). Itakusaidia kw matumizi yako madogo madogo.
AMINA: (Anaipokea kwa pupa utafikiri ni pesa yake). Asante sana Ben. (Amina anaugandamiza mkono wake kwenye kiganja Cha mkono wa Ben Kisha anaufinya finya Kwa dole la kati, Ben anashtuka, macho yao yanagongana, Ben anatizama chini kwa aibu, muda si mrefu, kengele ya kuingia darasani iligongwa.
AMINA: Bye bye! Kaka Ben nitakuona baadaye. (Anajaribu kuondoka).
BEN: Aaah!...aaah! Amina subiri kidogo kuna jambo nataka niongee na wewe (Anamkimbilia Amina).
AMINA: Jambo gani tena hilo kaka Ben? (Amina anamtizama Ben, wakati huo huo Mwalimu Grace alikuwa akiwatimua wanafunzi waliokuwa wakiendelea kuketi nje ya madarasa wakati wa vipindi na masomo).
BEN: (Anamung’unya mung’unya maneno).Unaj..ua..A..mi na..ku..” Hata kabla hajamaliza kuongea, mwalimu Grace alifika pale waliposimama Amina na Ben. Mwalimu amekamata stick anataka kuwacharaza Amina na Ben.
MWALIMU GRACE: Nyie wanafunzi, mnafanya nini hapa? Je,hamjui kuwa huu ni muda wa kuingia madarasani ili vipindi vianze?
AMINA: (Anatetemeka kwa woga wa kupigwa). Aah! Hamna kitu mwalimu, ndio tunaelekea darasani.
BEN: Nilikuwa namwomba kitabui cha History. (Anaangalia chini mara baada ya kugonganisha macho yake na mwalimu grace.)
MWALIMU GRACE: Haya nendeni madarasani kwenu, nisiwaone tena nje, huu ni muda wa kusoma, sio muda wa kuzunguka zunguka Canteen. Masomo yaliendelea kama kawaida, muda wa wanafunzi wote kwenda majumbani kwao ulipowadia, Beni alimngojea Amina nje ya geti la kutokea shuleni, na mara baada ya kutoka waliongozana pamoja, safari ya kwenda nyumbani kwao Manzese iliendelea, wakatembea mwendo mdogo mdogo, wakafika Ilala Boma wapate kupanda gari ziendazo Manzese.
Sijui Nini kitafuata
No comments:
Post a Comment