Tuesday, September 17, 2024

๐Ÿ–ค๐Ÿ’–๐Ÿ’ž (NIGHT OF LOVE)




 USIKU WA MAPENZI

Nimpweke natetereka, baridi natetemeka,

Moyo unashituka, mwili waweseka,

Gonjwa limenishika, dawa ninaisaka,

Mapenzi nahangaika, usiku wa mapenzi.

 

Mapenzi nahangaika, usiku wa mapenzi

Tazama napepesuka,  mapenzi ninayasaka,

Mikono imekunjuka, mwili walalamika.

Walalamika mapenzi, dawa ya kuponyeka.




 

Walalamika mapenzi, usiku wa mapenzi,

Tazama napepesuka, mapenzi ninayasaka,

Mikono imekunjuka,mwili walalamika,

Walalamika mapenzi, dawa ya kuponyeka.

 

Unipe hayo mapenzi, ambayo ninayasaka,

Kwa wingi maandalizi, ndivyo ninavyotaka

yajaponitoa chozi,  mapenzi tafarijika,

asante midomoni, hiyo itanitoka.




 

Asante midomoni, hiyo itanitoika

Tamwaga shukjurani, za wingi wa Baraka,

Tuwepo wote ndotoni,watulinde malaika.

 Maua bustanini, moyoni tuje kunjuka.

 

 Maua bustani, moyoni tuje kunjuka,

Tubebane migongoni,  tupate kupumzika,

Tutiane machoni, siwe kuja toroka,

Tupendane abadani, tupone tukaponeka.



No comments:

Post a Comment

BEKA

 SURAYA TATU                        “AKIPITA ATAJIPITISHA.” Beka akawa member wa kampuni ya SIGA, akipelekwa hapa na pale kulinda mali za ma...