Tuesday, September 17, 2024

LOVE TILL SUN DOWN

 

NITAISHI KWA MAPENZI





Kabla kuumbwa dunia,yalikuwepo mapenzi,

Kitu cha kujivunia,alikuwepo mpenzi,

Kwa tuli ametulia,jina lake ni mwenyezi,

Kichwani afikiria,ajenge ngome mapenzi.






Baada kuumba dunia, yamekuwepo mapenzi,

Milima inavutia,watu wasio ubaguzi,

Wanyama wajizalia,wadudu wazuri kweli,

Mimea ya jikulia, kwa upendo wa mwenyezi.




Mimi nilipozaliwa,nilizaliwa kwa mapenzi,

Nikala asali maziwa,maboga pia na ndizi,

Macho mazuri ya njiwa,yakanijaza mapenzi,

Taratibu nimekua,mzuri wanye azizi.




Taratibu nimekua,mzuri mwenye azizi

Mambo yote nayajua,hayanipi pingamizi,

Dunia naitambua,mema mabaya ujuzi,

Kipi kitanisumbua,sikioni kwa mapenzi.




Hata ivyo ninaishi,ninaishi kwa mapenzi,

Hapo sileti ubishi,mapenzi yamenipa pumzi,

Kipi cha kunitetesha,nikaya mainzi?

Kipi cha kuniogopesha,mapenzi yangu mzazi.




Ije itoke vita,nitaishi kwa mapenzi,

Yaje yazuke matata,mapenzi siyageuzi,

Yote hayo yanapita,mapenzi niya mwenyezi,

Furaha itanifuata,ni dumu katika mapenzi.




Hata mwisho wa dunia,nitaishi kwa mapenzi,

Pumzi ikififia,taya kumbata mapenzi,

Mikononi yatulia,yatanijengea zizi,

Roho itafikiria, niishi kwa mapenzi.





 


No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...