KUKU WA KIZUNGU
Sehemu ya 3
Tulipoishia.
“Pita Balozi Ole, lango lipo wazi nimelirejesha tu.” Balozi Ole aliingia amebeba kifurushi kidogo kilichofungashwa na kuzibwa kwa kitambaa kizuri cha kimaasai nyuma yake ameambatana na kijana amabaye Islama alipomwona tu, we! Mapigo yake ya moyo yakamwenda kasi kama Roketi juu ya mawingu, asitake kuamini kama kweli yule kijana aliyekuwa akimuwazia muda si mrefu leo hii ameambatana na Balozi
Ni kijana aliyemuona jana, kijana anayeufanya moyo wake uende mapigo mazito, kijana anayemfanya Islama kupumua pumzi ndefu na nene nzito ajabu, yeye binafsi amekiri kwa kusema ‘HAJAWAHI KUPENDA NDIO MARA YAKE YA KWANZA KUFANYA HIVYO”
Sasa endelea
Ile anagonganisha macho yake na huyu kijana mzuri wa kiafrika, si mnene bali ni mwembamba, mweusi tii mrefu kama Twiga, haki! Islama alihisi kama vile ameiona nyota njema ikizaliwa, na iyo nyota imezaliwa jana alipo toka Out pamoja na Balozi, wakaangaze angaze macho yao Hapo Maasai Land.
“Good morning, Miss Beautiful?” Balozi alimsalimu Islama ambaye bado angali macho pima kama mjusi aliyebanwa mlangoni, akimtizama huyu kijana anayeufanya moyo wake uwashe unahitaji mkunaji.
“Good morning, u hali gani Bwana Balozi?” “ Mie bukheri, shaka kwako, heri uzima kuliko upweke.” Balozi alimtania yule mrembo wakati wote huo mikono yao imeshikana kwa mtindo wa salamu.
“Nimelala vema, labda wewe?” Islama alijibu kwa furaha.
“Sijalala Miss, mawazo mengi juu yako, naitamani sana na kuisubiria siku moja ambayo utakuja kunipa offa ya kuwa karibu na wewe.” Balozi aliongea bila aibu, Islama alitabasamu kwa furaha. Ndivyo inavyotakiwa ugenini ukichukizwa uruhusu moyo wako uoneshe furaha, haijalishi kama unapendezwa au haupendezwi na hali uionayo, ingawaje kama umeona mambo hayajakupendeza usiyaweke moyoni muhimu kuyaweka wazi.
“Ninaona umenijia na mgeni siku ya leo, ni kijana mzuri na mpole,” Islama alimsifu huyu kijana anayeupendeza moyo wake kijana ambaye hapo baadaye alikuja kuligundua jina lake anaitwa LAIZER, Kijana mwenye umri wa miaka 26 hivi.
“Nikijana mzuri na mpole kama nilivyo kuahidi jana, nilikwambia nitafanya juu chini nikutafutie mtumi, tizama leo nimetimiza ahadi yangu, kama wahenga wetu wanavyosema ‘ahadi ni deni, timiza ahadi yako’”
“ Wee! Haki! Balozi una mambo ya kizungu weye.” Islama aliongea, tayari amewakaribisha wageni wake ndani, Juisi ya Zabibu midomoni mwao, wanaifurahia kwa kutafuna tafuna kwa karanga zilizochanyanywa rojo ya mayai.
“Mgeni kwetu Malkia.” Balozi alizidi kuchombeza,vicheko viliwatoka wote watatu. Wakati huo bado macho ya Islama yametua kwa yule kijana mwenye mvuto kwake, macho ya Islama yamejaa matamanio. Ua alilolikamata mkononi mwake, lile Ua jekundu anatamani kama angelimpatia yule kijana anayemtamani lakini aibu nayo imemtawala, asifanye upuuzi wacha avumilie, haraka haraka itamnyima Baraka. “Anaitwa Laizer" Balozi alimgusa yule kijana mabegani, akamtizama na kisha akayageuza macho yake kwa Islama
“Ni kijana mchapakazi sana, atafanya kazi nyumbani kwako, kazi zote utakazo wewe afanye atafanya……. Kwetu huyu kijana tunamwita MWANAUME MASHINE, yupo kama mashine, kwa kazi nzito hajambo,” Balozi alitania Islama akatabasamu wakati huo yule kijana pia akatabasamu.
“ Bwana Laizer” Balozi alimgeukia yule kijana “Huyu ni Bibie Islama, Bibi niliyekueleza kuwa ametokea Euorope (Ulaya), siku mbili tatu zilizopita, anahitaji mtumishi na mimi niliona heri na vizuri nikuumganishe naye, Karibu sana.” “ Shukrani na Asante,” Laizer aliitikia, akatabasamu, tabasamu lake liliyaonesha mapengo, meno yake mawili ya mbele, yameng’olewa, ndio utamadunini wao, sijui kwanini Maasai wanapenda kung’oa meno mawili makubwa ya ufizi wa juu?
“Karibu sana Bwana Laizer,” Islama alimkaribisha Laizer
“ Asante nimekaribia.”
“ Ni hivi bibie Islama,” Balozi Ole aliendelea kuongea
“Huyu bwana ameoa mke na pia ana mtoto mmoja,” Kawivu kakamwingia Islama mara baada ya kusikia kuwa Laizer ameoa na pia ana mtoto. Ile amemwona tu japo bado hajamjua vizuri, Islama alidhani labda Laizer yupo Single hana mtu, kumbe hisia hazijengi,wacha asikilize, sikio husikia, mdomo huongea, macho huona na akili hufanya kazi.
“Nimeafikiana naye jambo moja kwamba, atakuwa anakuja kufanya kazi hapa nyumbani kwako, kuanzia asubuhi mapema, kabla Jua halijachomoza, kwisha kumaliza kazi zote za nyumbani ifikapo saa moja jioni yampasa arudi nyumbani kwa mkewe.” Balozi alipumzika kidogo kuongea, sasa kidogo moyo wake Islama ulipoa, sababu wivu mwingine ni wivu wa kijinga jinga yeye binafsi anajua kuhusu hilo.
“Hivyo ndivyo nilivyo afikiana na huyu kijana, binafsi amekubali, amekubali kwa moyo mmoja anahitaji sana kufanya kazi. Je, Islama umeridhia kuhusu hilo?” Balozi alimeza mafunda mawili matatu ya ile Juisi yake Juisi ya Zabibu, akisubiria jibu kutoka kwa yule Bibie mrembo mwenye figure ya kizungu.
“Yes, sina pingamizi nimefurahi kuambiwa hivyo, pia ninamkaribisha sana nyumbani kwangu.” Islama aliongea kwa furaha, furaha yake ilionekana mbele ya wale wanaume wawili waliomtembelea, maongezi yao yakapamba moto na hatimaye Balozi alihitaji kuondoka, Laizer alibaki pale nyumbani awe karibu karibu na bosi wake. Asubuhi ile ilitosha kwa Islama kufanya kazi ya kumtembeza tembeza Laizer hapa na pale ndani ya nyumba yake ili Laizer apate kuyajua na kuyafahamu vizuri mazingira amabayo ni mageni kwake. ###############################
“ Ameoa?!”Islama aliwaza moyoni, yupo ndani pembeni ya kioo cha nyumba yake anatazama tazama nje akimwangalia Laizer amabaye siku ya leo anajibidisha ndani ya bustani ya Islama. Ile bustani ya Maua, anakata kata majani yaliyomea ndani ya Bustani (Anayapunguza na kuyapurunya)
“ Oooosh! Ana uzuri wa sura, Black handsome!” Mawazo yalimchanganya na kumtibua Islama, anatembeza tembeza macho yake nje ya mwili wa Laizer, mapaja makubwa meusi ya yule Maasai yapo wazi, amechuchumaa ndani ya ile Bustani, anaihudumia kiutaalamu.”
“Sijui nimwambie? Mmmh! sijui nimsubirie au?” Islama amelikamata Ua aina ya Jasmini ananusa nusa harufu nzuri ya lile Ua, Ua lile linamvutia , mapenzi yanamjaa na kuujaza mtima wake
“Mimi ni mwanamke, mwanamke ana haki ya kupenda na kupendwa. I’m English Lady, mwanamke wa kizungu, tofauti na mwanamke wa kiafrika, sie wazungu daima hatuna aibu, tukipenda tumependa, muhimu tulipopenda papendeke.” Mawazo yalimtibua Islama pembeni yake kuna Bottle yenye Juisi ya Zabibu, akaitwaa ile juisi na kuimimina kwenye glass kisha akameza funda moja, ili kutuliza mapigo ya moyo wake.Mapigo ya moyo wake yanamwenda kwa kasi zaidi mara ile amwangaliapo huyu kijana ampendaye, apendezaye moyo wake, ni mzuri kuliko David, boy wake aliyemwacha England, amepitiliza uzuri kwa jinsi anavyomwona yeye binafsi na kwa mtazamo wake yeye binafsi.
“Laizer” Islama alimwita Laizer, ametoka ndani ya nyumba yake, ameelekea kwenye Ile bustani ya Ua lake, bustani ambayo Laizer anaihudumia.
“Yeah, Madame” Laizer aliitikia , Islama hakupendezwa na lile jina Madame alitamani angelimsikia Laizer akiyatamka yale majina matamu ya kimapenzi, “Swet heart, Lovery Quuen, My love,Dear, Amour……Mmmh!”
“Can I help you,” Islama aliongea akitamani kumsaidia Laizer shuhuli ile ya kupalilia Bustani
“No, Madame ninakaribia kuimaliza.”
“Alright, ninahitaji tutoke pamoja twende Market,” Islama aliongea amelichuma Ua zuri la Jasmine, ajabu mara baada ya kulichuma lile Ua akampatia Laizer mkononi mwake, Laizer akalipokea kwa shukrani.
“No, problem twaweza kutoka Madame,” Laizer alikuwa tayari kutoka na kwenda Sokoni pamoja na Islama, Islama akaiendea Gari yake aina ya Tax iliyo wazi juu, Gari hii ameletewa majuzi, kutoka Shirika la utalii Tanzania, ameazima kwa muda wote ambao atakuwepo Afrika, popote pale anapotaka kwenda, Gari ipo kwa ajili yake.
“Unapenda kuendesha?” Islama akamtega Laizer kwa swali la Uchokozi, wakati huo Gari yao ipo barabarani, kuna vumbi kiasi, uzuri wake majira haya ni majira ya mvua ambayo itaanza kunya muda si mrefu, basi hilo vumbi zito kama ugolo wa kimaasai halina nafasi kipindi hiki kizuri cha mvua.
“Hata sijui” Laizer alimjibu Boss wake.
“Nikufundishe,” Islama aliukamata Mkono wa Laizer
“Naogopa,”Laizer alijitetea.
“Unaogopa nini wakati mie ninajua kuwa weye ni mwanaume Mashine? Sifa kubwa ya mwanaume mashine ni kwamba haogopi,”
“Duh!” Laizer alicheka kidogo na kuguna, Islama aliisimamisha ile Tax iliyo wazi juu ya bodi, akateremka ule upande alioketi, akamwambia Laizer Keti upande wa Dereva, Laizer alibaki bumbuwazi kwa amri ya Boss wake. Kwa pupa Laizer alieleka kuketi, Islama akazunguka na kueleka kuketi ile nafasi iliyoachwa wazi na Laizer.
“ Washa funguo ya Gari,” Laizer alitii amri gari ilianza kulia ‘Kanyenyenyenyenyeeee njiiiim, Laizer alitetemeka kidogo, woga na hofu, ndio mara yake ya kwanza anatolewa ushamba sasa.
“ Ikanyage hiyo Gia mguu wako wa kulia,” Islama aliongea akimtizama yule Maasai kwa matamanio kibao,hamu ya kulala na yule kijana imemkamata vilivyo, mmmh! Yetu sie macho.Laizer akatii amri mguu wake aliovaa Makurubasi na vikuukuu vyenye shanga za kimasai ilikanyaga Stata.
“Ninataka unapo unyonga nyonga huu mstering uwe unatazama mbele ya kioo ni muhimu sana usipuuze kwa sababu Dereva ni macho na macho ni Dereva,” Islama aliongea, Laizer alitii maagizo Gari ikaanza kutembea taratibu kama vile inavutwa na Tembo, vicheko na tabasamu viliupamba uso wa Islama, alicheka na pia alitabasamu kuona jinsi gani yule kijana ampendaye akilikokota Gari.
“ Mwanzo mgumu,” Islama aliongea
“ Mwisho utakuwa mchonga gogo,” Islama alimpooza yule kijana ambaye siku ya leo alijisikia fahari
“ Nitafurahi zaidi,” Laizer aliongea “Utafurahi sana,” Islama alizidisha maneno, safari yao iliendelea Islama hakuacha kumuelekeza yule kijana nini anapaswa kufanya wakati wa kuliendesha gari.
##############################
Tukutane sehemu ya 4
Kama hujaisoma sehemu ya 1, 2 na 3
Binya link hapo utakutana na maandishi meusi "kuku wa KIZUNGU" binya hapo Kuna mwendelezo
Wakaribishe wengine pia
No comments:
Post a Comment