Tuesday, September 17, 2024

BLACK DEVIL (MALAIKA MWEUSI)


                 MALAIKA MWEUSI

(Alinibakaaliniua na kunifufua.)

 

SEHEMU YA KWANZA


Upepo mkali ulivuma na kutikisa tikisa paa la kijumba nyasi changu, kijumba nyasi cha udongo  wa mfinyanzi chenye paa lililoezekwa kwa kutumia mbavu za Umbwa pamoja na makuti, upepo ule ulifanya mlango mkubwa wa kijumba nyasi changu ufunguke kwa nguvu nao ukalia paaa’ nilishituka kutoka usingizini nikaamka pale mkekani nikishangaa shangaa huku na na kule kama vile mwendawazimu.

 

              Upepo ule haukukoma ulivuma tena kwa nguvu na kukitikisa tikisa kijumba nyasi changu mara ile radi kali ikapiga juu ya anga la dunia ngurumo za radi zilinitia hofu na kuniogopesha, sio kwamba sijazoea kusikia ngurumo kali za radi ile, nimezoea lakini ngurumo hizi zilinitia hofu zikayaumiza masikio yangu, zikasaga saga meno yangu, mie niliogopa.

 

              Usingizi ulikwisha nitoweka, nikaukadilia muda na wakati, nyota na mbalamwezi viliniashiria kuwa ni saa nane usiku usiku huu daima ni usiku mbaya, usiku wa kutisha na kuogopesha, usiku  ambao nalisikia mabundi yakilia juu ya paa la kijumba nyasi changu, hiyo ni ishara mbaya kwangu, ishara ambayo kwa tamaduni nyingi za kiafrika ni mkosi, naam nilijiona nipo ndani ya majanga.

 

Popo waliranda randa huku na kule, nilitishika nikaogopa sana haraka nikadamka pale juu ya mkeka wangu uliosukwa sukwa kwa nyasi kavu, nikakimbilia mlango na kuufunga sababu ulikuwa wazi umefunguliwa na upepo, nikaweka mawe pamoja na vyombo mbali mbali vikuukuu nilivyo navyo ndani ya kijumba nyasi changu. Hofu ilinitanda ukitegemea nipo ndani ya msitu mkubwa wa Roleza ningali pekee yangu, nimeishi pahali hapa miaka na miaka sitaki wala sitamani kurudi tena nyumbani kwa baba na mama yangu wa kufikia.

 

                 Mama mbaya sana, mama ninayemchukia, mama aliyenifanya niichukie dunia na wanawake wote wenye sura za ukatili na manyanyaso.

              “Ngroooooo!” Radi ilipiga tena juu ya anga, nikatia hofu kuu, sijapata kuogopa kama nilivyo ogopa sku ya leo, leo nimeogopa juu ya usalama wangu, leo nimetikiswa tikiswa juu ya usalama wangu. Upepo haukukoma miti ilitikisika tikisika mvua ilionesha dalili, matone matone hatimaye ilianza kunya kwa ghafla na kwa wingi, miezi hii ni miezi migumu kwa mwonekano wa mvua labda mwezi wa kumi na kumi na mbili au wa pili na wa tatu, hivyo ndivyo vipindi vya mvua mkoani Mbeya lakini sio huu mwezi wa saba.

 

 Upepo uliendelea kuvuma, radi na mvua vilikunya, mabundi na popo yalitanga tanga na kukizunguka kijumba nyasi changu, nilitia hofu sababu nipo mpweke ndani ya msitu mkubwa wenye giza nene la kutisha, roho yangu ikaniambia enenda dirishani ukachungulie ukione utakachokiona!” Roho nyingine ikaniambaia “La! Usiende, lala pumzika ni usiku wa manane.” Roho mbili ziliendelea kupingana hatimaye asiyekubali kushindwa si mshindani, nikatoka pale kwenye mkeka wangu nikaelekea dirishani nikachungulia nje.

 

               Mtume! Mola wangu we! Aridhi ilikuwa inapasuka pasuka vipande vipande, maji ya mvua yakaingia ndani ya  mipasuko pasuko ya ile aridhi, shimo kubwa likatokea aridhi ikadidimia chini, maji yakaendelea kuingia na kujazana ndani ya lile shimo. Niliendelea kutazama, mmmh!  Nilijihisi kama nipo ndotoni nisielewe nini kinachoendelea, mara kwa ghafla ningali bado ninaendelea kushangaa na kuogopa hali ile, hofu juu ya usalama wangu ilikuwa kubwa, nikahofia juu yaa nafsi yangu, aridhi iliendelea kupasuka pasuka, mipasuko ile ikasogea na kuelekea mbele kwenye kijumba nyasi changu.

 

                 Macho yaliendelea kutizama nje, nje kwenye mvua, radi na ngurumo, zilipita dakika tano mara baada ya aridhi kupasuka pasuka vipande vipande niliingiwa na woga mkuu, nikatetemeka sana, meno yangu yaligongana gongana, haja ndogo ilinitoka pasina mie kujua kuwa ninajikojolea, mapigo ya moyo yalinienda kasi na kusi, joto la mwili lilinipanda na kushuka, nywele zilinisisimuka, masikio yangu yaliingia baridi, tumbo liliniunguruma na kukata kata, nilihisi kuna kitu kinazunguka zunguka ndani ya tumbo langu, ni kama vile nyoka anatembea tembea tumboni.

 

              Macho hayana pazia, nikaziona pembe ndefu nzito kubwa kama pembe za ndovu zikachomoza na kutoka ndani ya lile shimo, mwanga wa radi na mbalamwezi vilinisaidia kuona  kichwa cha mwanamke mwenye ngozi nyeusi tii kama chungu mekoni.  Sikutaka kuuangalia mara mbili mbili sababu nilikua nina tetemeka tetemeka kwa hofu na kwa woga, nisijue nitapatwa na nini mie niliye pekee ndani ya ule msitu mkubwa wa kutisha.

 

Usoni alikuwa na macho makubwa yanayotoa moto, meno yake ya juu na ya chini yalikuwa ni marefu kama vidole vya mtu mzima, ulimi wake uliokuwa ukitoa damu ulikuwa ni kama ulimi wa nyoka, niliogopa nisijue kama kweli nitakuwa salama siku ile. Mikono yake ilisheeni kucha ndefu , chini miguuni alikuwa na kwato za punda, niliendelea kumtazama





Itaendelea

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...