Thursday, September 19, 2024

I love my Elders

 NINA WAPENDA WAZEE






Ninawapenda wazee ,hilo ni jukumu langu ,

Wengi nitegemeo katika maisha yangu,

Lazima  niwatetee , huo ni wajibu wangu ,

Wazee ndio chimbuko, chanzo cha maisha yangu,


Wanazo nyingi hekima, katika kumbukumbu zao ,

Hutamka kwa heshima, kwa hayo maneno yao,

Haki kweli ndo uzima , kwakila zuri lao ,

Wazee ndio chimbuko , chanzo chamaisha yangu,




Matatizo hutatua, ni moja ya kazi yangu

Maovu kuzifichua, zote nitabia zangu ,

Akil kuzifumbua, nalo ni jukumu langu,

Wazee ndiochimbuko, chanzo cha maisha yangu,


Chanzo cha historia, wazee ndio chimbuko,

Chimbuko lakuanzia, kwao ndio maendeleo,

Kwa kweli wajivunia, wazee kuwatangaza,

Wazee ndio chimbuko chanzo cha maisha yangu,


Wao ndio walezi wangu , sio wa jana  sio wa leo,

Tangu utotoni mwangu, wamekuwa kichocheo,

Kwa matamu na machungu, wao ndio tegemeo,

Wazee ndio chimbuko, chanzo chamaisha yangu,



Kweli maisha machungu, bila kuwa na wazee,

Ntakuwa changamfu, na mema ni watendee,

Hata matatizo yangu, niwaelezee,

Wazee ndio chimbuko , chanzochamaisha yangu,


Wao ni wazalendo, kwa manufaa ya nchi,

Kwa yetu haya matendo, hili halina ubishi,

Mawazo yao vitendo, si mawazo tatanishi,

Wazee ndio chimbuko, chanzo cha maisha yangu,







No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...