Sunday, September 8, 2024

HADITHI: WAMEZIDi sehemu ya kwanza

 



WAMEZIDI.(Wamekua too much)

Mtunzi:Elaija-Elia.

(Sms) +255744225388.

           KAMPANI.

"Waziri Beni unahitaji KAMPANI huwezi kwenda pekee Ulaya." Secretary Rose aliongea kwa madaha mbele ya Ofisi ya Bosi wake Waziri Beni. Alimshawishi Waziri aungane na KAMPANI (wapambe) yake kwenda kuvinjari Ulaya.


"Ningependelea kusafiri Single." Beni aliongea kwa ufupi, akauzungurusha zungurusha mguu wake kunako kiti Cha magurudumu, kiti kilimtii na kumuheshimu kikajigeuza kama kando la maandazi ligeuzwavyo kikiwa na tabasamu la bashasha.


"Mkuu wangu wazo lako jema, silipingi. Itapendeza zaidi kama utanichukua mimi pia Rose Ua lako la moyo" Rose alimsumbua Bosi wake kama alivyozoea kusumbua Kila siku.

 Mjanja Sungura, Rose alihakikisha anamteka kimapenzi Bosi wake ambaye aliingia mkengeni akamezwa na penzi la huyu Bi dada aliyemlevya na kumuacha hoi. Umekula mazoea Kila hitaji analohitaji Rose hupewa kwa muda na kwa wakati yote ikiwa ni sababu ya nguvu ya penzi.


"Ooh, unatamani eeh"  kibosile yule mwenye kitambi kama mama Mjamzito aliongea kwa tabasamu la faida kwa bibie Rose.

"Zaidi ya kutamani, Bosi wangu."Rose alimjibu Bosi Beni. Midomo yake ya juu na ya chini ameikooza kwa Lipstick nyekundu zenye ishara ya mahaba nifirisi.

"Ok, very nice panga bajeti ya siku Tano, wape data 'akina Joe, Mimi, Viva, Dino na Max.... Waambie wajiandae Safari ya Ulaya ishaivaa, tukale kuku, tujimwambafai na kuinjoi life"Secretary aliingiwa na furaha iso na kipimo alipoambiwa ni wakati wa kupanga na kujipangia chochote kipendezacho Safarini. Uzuri. Beni hanaga maswali kuuliza 'kwanini twende kama kampani? Kwanini nisisafiri pekee? Nini kinachonizuia.' Hana shombo hizo. Akiambiwa ameambiwa, akielewa emeelewa ameelewa. Si mpigaji Wala  si mpingaji, sio mwenye moyo wa kusita sita. Mlaini kama chuzi la bamia, mpole kibosile huyu, asikuambie mtu, tena hanaga moyo wa kumbahiria mja anatoa tena anatoa zaidi ya moyo wake unavyomtaka atoe. Sababu hiyo rafikize wapambe kina Max, Mimi, Viva, Dino, Joe na Rose secretary haweshi kusumbua na kumtaka azidishe gharama watakazo wao.

  "Vipi kuhusu usafiri, Meli itatutosha Dear?! Kama kawaida yake Bosi humpatia nafasi mtu atoe duku duku lake bila kupingwa.

"Jamani Dear! Rose akajibebisha kideko deko,"

"Ndege itatufaa, Private Jet. Kwa usafiri huo wa haraka na hakika hatutachelewa" Alideka kimahabati .Binafsi anajua kuwa Akideka atadekezwa, akila atalizwa na lazima atafanikiwa.

"Sawa Fanya utakavyo kufanya" Beni Alihitimisha.Rose akafanya hima kutoka ndani ya Ofisi ya Waziri Beni, hima akawape taarifa wapambe wampao KAMPANI Waziri Beni. Tembea yake ya madaha ilifanya nguo yake ya chini(sketi) nyepesi iyachonjoe mapaja yake yaliyonona unono wa Nguruwe, baya zaidi nguo yake ya ndani ilijichora matakoni  ikampa wakati ngumu Waziri. Ukizidisha weupa pee wake Rose ukawa mtego kwa Waziri aliyemtazama kwa Huba la tamanio.

"Huyu Mbwege nikimnong'oneza awachane na mkewe tuishi wawili tu. He will never disagree" Mtoto Rose aliwaza kimoyo moyo, akafanya kubinyabinya nambari za Simu, akawatafuta wapambe wa Bosi Beni, akawapata naye akaongea na mmoja baada ya mwingine.

"Hallow Max,"Rose aliita

"Yes Baby, Mambo vip Rose." Max aliitikia. Hakuna Siri tena Max na Rose ni wapenzi wanaomzuga Beni ambaye hajui uhusiano wao. Kwa mtindo huuBeni ataishia kunawa kula asile.

"Fresh tu Baby." Rose alinong'ona sauti ya chini Bosi Beni asisikie tena asijue.

"Sema Love sauti ya chini, tatizo Nini?" Max aliuliza.

"No problem, hakuna matata, we jipange jipanguse tuna bonge la Safari moja traaam! Ulaya hukooo.Beni ameongea anataka KAMPANI" Rose Alideka.

"Waoo! Tukale Raha hadi Buzi libakie mufupa " Maxi alishangilia. yeye ni kijana wa 45, katika umri huo hajaoa waka hajazalisha, yeye ni starehe na starehe na yeye.

"Tukale Bata Love." Rose alichombeza

" Lini hiyo?" Max alihoji.

"Friday morning, kesho kutwa" Rose alijibu.

"Good! What next?" Max alipiga kimomboo

"Tikiti ya ndege."

"Dua!Tutapanda ndege? We huogopi"

"Unataka tupande kokoteni" Rose alitania.

"Teh teh teeeh" Max alicheka hadi ulimi na Meno vikamcheka..

"Itakua KAMPANI ya watu sita, wale wale wa siku zote." Max alijulishwa.

"Max, Viva, Mimi, Dino, Joe na wewe Rose"Max alimkumbusha Rose.Juu ya KAMPANI crew Yao.

"Yes, muhimu ni nyinyi kudeka, mdekieni huyu boya adekewe hadi adekike kama tambaa la deki"Rose alikebehi.

"Something like that, hilo ni Buzi mchuzi, lazima lichunike" Max aliongeza neno. 

"Tulichune mishipa hadi libakie mifupa"Rose aliongea kwa sauti ndogo.

"Shaabash! Wacha nijiandae, wape data hao wengine." Max alichangamka changamka.akazima Simu yake.Rose aliendelea kuwapa taarifa washirika wengine.


(Tutaendelea)

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...