Monday, September 16, 2024

ZAWADI

 


1

ZAWADI YANGU YA MAPENZI,



ZAWADI YANGU POKEA,

YANA MWANGA WA MAPENZI,

MAUA YANAYOMEA,

KWAKO NINAKULETEA,

JICHO KODO KUPERUZI.


2

MAUA YAKIKUVUTIA,

YAKUTAKATISHE NGOZI,

PALE YAKIJIKUNJUA,

MOYO UNATAKA DOZI,

HOMA ITAKUISHIA,

'MEPATA TABIBU.




3

Basi mpenzi sikia,

Tuyatunze Maua,

Kwa maji kumwagilia,

Na kuyatia mbolea,

Mpenzi tutajichumia,

Maua yaliyomea.




4

Mpenzi tutajichumia,

Matunda yaliyomea,

Kwa wingi tutajilia,

Mazuri ya kutegemea,

Njia njema kupitia,

Heshima kutupatia.




5

Kwa wingi tutajivunia,

Mazuri kututopea,

Njia njema ni kupitia,

Hekima kutumendea,

Zawadi nakupatia,

Basi Mpenzi pokea. 



No comments:

Post a Comment

ZEE LA ZAMANI

  SEHEMU YA KWANZA. HOTELINI Ndani ya Hoteli Paradiso katikati ya Jiji la Mzizima (Dar es salaam) ZEE LAZAMANI akiwa na Mwanagenzi wake JAN...