Wednesday, September 11, 2024

KUKU WA KIZUNGU


 

            Ndege ya British Air wing ilitua  katikati ya kiwanja cha kimataifa, ARUSHA INTERNATIONAL AIR PORT. Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Uingereza,  ilipotua nanga abiria waliteremka mmoja baada ya mwingine.Islama binti mrembo mwenye ngozi ya kitasha (kizungu), mrefu kiasi ni mwenye English figure Waswahili wanaiita hiyo  figure ‘Modo’, wengine wanatania kwa kuiita ‘Figa ya  mguu wa kuku.’ Aliteremka amependez kwa kutupia Suruali yake moja ya JEANS, zile jeans za miaka ya 80’s zilipendwa, ametupia kofia yake inayozuia nywele zake zisitibuliwe na vumbi au upepo. Machoni ametupia miwani mieusi, anatabasamu lake mdomoni. Islama akatembea hatua mbili tatu kuelekea mpokezi apate kukamilisha shuhuli  ya ujio wake katika Ofisi za uhamiaji.      

     Alitimiza na kukamilisha taratibu za uhamiaji, ndani ya dakika therathini Islama alitoka pale Air port akiwa na begi lake kubwa lenye nguo na vikorombwezo  vyake vingine baada ya kutoka pale Airport Islama alikodisha Tax iliyompeleka moja kwa moja Hadi Hoteli Arusha, moja ya Hoteli zenye hadhi ya nyota tano, Hoteli ya fahari kubwa na gharama pia. Hakukaa sana ndani ya ile Hoteli Islama alikuwa na malengo pamoja na  matarajio yake, amekuja Arusha akiwa na lengo kuu moja kupumzisha akili na na mwili wake mara baada ya kuchoshwa na ule upweke wa kukaa nyumbani kwao England.     

         Islama anataka kutalii anataka kutalii Afrika anataka kujionea fahari ya Tanzania na uzuri wa Safari yake Islama yupo tayari kuishi mwaka mzima ndani ya nchi aipendayo yeye binafsi Tanzania. Amechagua kujipumzisha Tanzania kwa sababu amefanya Research, na Research yake imeonesha matokeo mazuri, imeonesha kwamba anaweza kuishi ndani ya Tanzania, anaweza kuishi hata miaka Mia, kwa sababu Tanzania ni Nchi yenye amani kubwa sana Afrika ya Mashariki. Tanzania ni Nchi tulivu  inayoongozwa kidemokrasia sio hivyo tu bali pia Tanzania ni Nchi iliobarikiwa kwa kuwa na kila kitu kizuri cha kuvutia machoni: Mito na Naziwa yenye asali Mabonde na Milima mirefu Duniani, Mbuga za wanyama wazuri na wenye kuvutia, Majiji makubwa, Majumba ya fahari na kila kitu kizuri na chema  machoni hakikosekani Tanzania. Ndio maana Islama aliona wacha akajiliwaze Tanzania.           

       Siku mbili tatu za kukaa Hoteli zilimtosha, Islama alihitaji kuondoka kwenda sehemu ya mbali na mji yaani KIJIJINI Umasaini Akafurahie maisha ya huko, akajionee mapya mbele ya macho yake kama wahenga wanavyosema macho hayana pazia. Tembea uone usitegeme kuambiwa, Islama alihitaji kutembea ili akajionee maisha ya kijijini, akajionee uzuri tofauti na ule aliozoea kujionea mjini. Ikawa hivyo siku njema yaonekana asubuhi Islama akafunga Safari yake naye akafika Maasai Land (Kijiji cha Maasai) kufika huko wenyeji wake walimpokea kama Malkia, ukarimu aliokutana nao hakutegemea kama angelikutana nao, binafsi alijisikia kama ni ndoto kwake kupendwa na ugenini.  Kuku mgeni hakosi kamba mguuni, Islama aliandaliwa nyumba yake yeye binafsi, nyumba ya kulaza kichwa chake, alikwisha jieleza mbele ya Balozi wa kijiji ya kwamba atakuwepo ndani ya kijiji cha Maasai Land kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.       

         “Hapa hakuna matatizo yoyote yale, haki! Bibie utapapenda,” Mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa kijiji cha Maasai Land alimwambia Islama.

        “Nimepapenda pamenivuta na kunivutia.” Islama aliongea kwa furaha. Nyumba aliyokabidhiwa ni nyumba yenye vyumba vitatu vikubwa, sebule yenye kila kitu ndani, bafu choo, stoo, jiko pamoja na chumba kingine maalumu kwa kujisomea vitabu, Majarida na Magazeti. Amekodi nyumba nzuri sana pale kijijini, nyumba aliyokodi inatofautiana  sana na zile za Wanakijiji. Tofauti na nyumba yake, nyumba za Wanakijiji zimeezekwa kwa  nyasi, makuti na mbavu za Umbwa. Nyumba yake yeye ni nyumba special yenye vigae, umeme, maji na kila kitu muhimu ndani yake.

     “Chochote kile utakacho hitaji usisite kunieleza, nipo kwa ajili yako nitakusaidia.” Balozi ambaye ndiye mwenyeji wake aliyempokea aliongea.

     “Thanks,” Islama alijibu angali anamtizama sana yule Balozi amabye machoni alionekana kuwa na wingi wa taama za kumpata yule English figure japo Kuku mgeni hakosi kamba mguuni, wacha amuwache kwanza ayazoe mazingira na baada ya hapo siku moja traaamu atafanya kumueleza yale yote yaliyo moyoni mwake.

Islama akaingia ndani ya nyumba yake mpya Afrika, hatua ya kwanza mara baada ya kuswafi mwili wake akawapigia simu wazazi wake huko ENGLAND kuwataarifu kuwa yu salama salimini, ameipenda sana Afrika ‘Africa is beautiful and the most’  Wazazi wake walimtakia mapumziko mema. Jioni ile akaingia jikoni ajiandalie mlo wa usiku, kuku rost mayai, mbogamboga za majani tambi na maziwa aliyopewa na jirani mwema Balozi ambaye kwa sasa ndiye mwenyeji wake pale Kijijini.


 Itaendelea kesho

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...