Thursday, September 19, 2024

IGIZO. KlGUU NA NJlA sehemu ya pili

 


Tulipoishia

MWALIMU GRACE: Haya nendeni madarasani kwenu, nisiwaone tena nje, huu ni muda wa kusoma, sio muda wa kuzunguka zunguka Canteen. (Masomo yaliendelea kama kawaida, muda wa wanafunzi wote kwenda majumbani kwao ulipowadia, Beni alimngojea Amina nje ya geti la kutokea shuleni, na mara baada ya kutoka waliongozana pamoja, safari ya kwenda nyumbani kwao Manzese iliendelea, wakatembea mwendo mdogo mdogo, wakafika Ilala Boma wapate kupanda gari ziendazo Manzese.)


AMINA: Asubuhi ya leo ulitaka kuniambia kitu gani Beni wangu? (Amina alimkumbusha Beni yale maongezi waliyoyaacha Asubuhi).

BEN: Sikumbuki vizuri, kwani nilitaka kukuambia jambo gani? (Anajifanyisha mpuuzi asiyekumbuka alichotaka kumwambia Amina Asubuhi). 

AMINA: Ben mie sikufichi, (Wanasimama karibu karibu na soko la Karume, hapo kuna mataa ya kuruhusu Gari zipite). Mie nakupenda sana, nahitaji tupendane pendo la mapendo.

 BEN: (Amejaa tabasamu pana). Unanipenda?! (Anauliza kwa Mshangao.

AMINA: Ndio, I love you so much Ben💕.

BEN: Mbona sijakuelewa, una maanisha nini Amina?

AMINA: Nakupenda kwa hisia za moyoni, nakupenda kimwili, pia ninakuhitaji. (Amina akamkumbatia Ben akampiga mabusu mazito pasina kuogopa macho ya wapitao njia, waliowatizama sana).

AMINA: Je, Ben unanipenda? (Amina alimuuliza Ben lile swali.).

BEN: Nakupenda sana Amina. (Ben aliongea kwa kumung’unya mung’unya maneno, wote waliendelea na safari yao). Amina alipofika nyumbani kwao alimkuta  Mamaye akiandaa vifuko vya ubuyu na karanga. Anafungasha fungasha ili apate kwenda  kutembeza tembeza mitaani).

AMINA: (Anamsabahi mamaye). Mamangu huyo, shikamoo, habari za mchana, pole na kazi.

MAMAYE AMINA: Marahaba mwanangu, mchana ndio hivyo tena, bora ya jana. (Amina anaelekea jikoni).

AMINA: Jamani mama, leo haujapika kitu? (Tayari amefunua vyungu na masufuria, humo hajakuta kitu).

MAMAYE AMINA: (Anaongea kwa masikitiko). Yaani mwanangu we acha tu, ndio maana nimesema heri ya jana, mie mama yako nimefulia sana, nimekauka utafikiri vipeke vya ubuyu. Heri umekuja mwanangu, uende mitaani ukanisaidie kuuza huu Ubuyu, angalau tupate shilingi mia mbili ya kununulia tembele na nyanya.

AMINA: (Ananuna) Aah! Mama naye, sijui hajui kuwa nimechoka? Kazi hizi za kuuza ubuyu na karanga sizipendi kama nini!? (Anafyonya taratibu) Fyuuuu. Mara ile anaingia babaye Amina mzee Kiputa, amevaa miwani, hajielewi wala haelewi nini kinachoendelea, anapepesuka huku na huko kama mwendawazimu).

MZEE KIPUTA: (Anamwita mama Amina)We mwanamke😨 nasikia njaa, tumbo langu halijapata mlo leo siku ya tatu sasa, hembu niandalie ugali wa nguvu, jaza mboga kwenye bakuli mie baba mwenye nyumba nile nishibe. (Anapepesuka pepesuka kuelekea ndani ya Sebule).

MAMA AMINA: Mwanaume we kama mwendawazimu, siku ya ngapi leo haujalala nyumbani, leo ni siku ya ngapi haujaacha hela ya matumizi nyumbani, yaani uje umelewa, udai chakula ukijua fika kuwa haujaacha  hela ya hicho chakula.

MZEE KIPUTA: Samahani, usinikemee, na pia usinibwatukie domo lako, hilo la kutokuja nyumbani au kutolala nyumbani halikuhusu, wewe tekeleza wajibu wako, niandalie chakula mie nile nilale. (Anaongea kwa hasira).

MAMAYE AMINA: Hicho chakula kingekuwa mana basi ningekuandalia, lakini chakula chenyewe sio mana. Baki njia kuu mwanaume wewe suruali tupu, nenda kalalale hivyo hivyo ili siku nyingine uikumbuke familia yako, ukumbuke kuwa hata sisi huku nyumbani twalala njaa yenye mashaka (Anaendelea kufungasha ubuyu na karanga kwenye vifuko).

MZEE KIPUTA: Usinitanie ewe mwanamke😨. (Anageukia kule aliko mkewe). Leo ni siku ambayo nitakufunda ili ujue kuwa mimi ni mumeo. (Anakunja ngumi na kumpiga mkewe, mkewe anakimbilia nje ya nyumba yao, anazitelekeza zile karanga na ubuyu ambao mzee Kiputa anavimwaga chini kwa hasira, chini kwenye mchanga mwingi kama wa baharini.

**********

Mchana ule Amina alibeba kapu lake lenye wingi wa mabuyu na karanga, naye akaelekea barabarani kuinadi biashara ile. Akiwa yungali njiani ni mwingi wa mawazo.

AMINA: Haya maisha ya kuketi nyumbani, kutwa kuchwa kuwatizama baba na mama wanapigana kama watoto wadogo nimeyachoka, nikimaliza shule ninahama pale nyumbani, nyumba imekaa kama vile ulingo wa mapambano. (Mara anasikia honi ya gari ikipigwa upande wake, anaigeuza shingo yake ili apate kujua ni nani huyo ampigiaye honi.

MZEE PUTAPUTA: (Anampungia mkono Amina ikiwa ni ishara ya  kumwita, pasina shaka, Amina anaelekea usawa wa gari ya Zee la putaputa). Oooh! My dear, sweet love Amina, nakuona unaelekea kwenye business zako. (Mzee putaputa aliongea kwa tabasamu pana).

AMINA: Ndio mpenzi wangu, japokuwa nimelazimishwa, lakini sina jinsi inabidi nikubali tu, liwalo na liwe, ilimradi nipate pesa za kumtunza mama yangu.

ZEE LA PUTAPUTA: Kumtunza!? Oooh! Huu sio wakati wa kumtunza mama yako bali huu ni wakati wa yeye kukutunza kwenye raha na karaha ili hapo baadaye uzeeni nawe uchukue jukumu la kumtunza yeye. (Anafungua lango la Gari yake)

AMINA: Kweli kabisa mpenzi wangu. (Anaingia ndani ya lile gari hata kabla hajakaribishwa).

ZEE LA PUTAPUTA: Unajua Amina mie biashara kama hizi za wewe kuuza ubuyu na karanga sizipendi kabisa, lakini kama utakuwa tayari kukubaliana na mimi, basi mie nitakuwa radhi kununua karanga na ubuyu wako wote kwenye hilo kapu.

AMINA: (Amejaa furaha na matumaini). Oooh!  Mpenzi nitashukuru sana, utakuwa umeniunga mkono mrefu, yaani kama vile unavyowaza wewe, hata mimi binafsi siipendi hiyo kazi ya kuzunguka, kutwa kuchwa kwenye Jua, naichukia sana, naichukia kama nini? (Amina aliongea kwa dharau).

ZEE LA PUTAPUTA: Ok, vema mtoto mzuri, sasa unaonaye mie na wewe twende Guest house tukafurahie ujana wetu, kisha nitakuachia shilingi laki mbili keshi, utajua wewe mwenyewe namna ya kuzitumia. (Aliongea huku anamtomasa tomasa Amina mapajani).

AMINA: Shaka ondoa mpenzi wangu, mie nipo kwa ajili yako, ilimradi tu usinidanganye, uniipe hiyo laki mbili, unilishe leo, si unajua tena sijala tangu asubuhi. Uninyweshe moja baridi, kisha unirudishe nyumbani kwa baba na mama nikiwa Bwiii! Nimelewa chakari. (Amina aliongea kwa kujiamini).

ZEE LA PUTAPUTA: Mie ndio Zee la Putaputa, nitafanya kila kitu unachokitaka mtoto, uwe na amani moyoni mwako, nadhani utafurahia raha nitakazokupatia, hautanisahau kamwe maishani mwako.

AMINA: (Akamshushia busu moja zito mashavuni mwake Putaputa). Asante sana my love, I love you so much.💝

ZEE LA PUTAPUTA: I love you too. 💕(Gari likatoweka, Amina na Zee la Putaputa walieleke Guest.

Itaendelea.

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...