Tuesday, September 17, 2024

IS IT HOW YOU LOVE ME JESUS? ✝️





 AUKUNIPENDA MIMI?


Kwanini watapatapa? Mpenzi wangu msalabani,

Umechomwa kwa chupa, kosa lako kosa gani?

Au kunipenda mimi? Ubavuni mwako uchomwe,

Au kunipenda mimi? Muslaba wako ubebe?

 

Au kunipenda mimi Dunia ikuandame?

Au kunipenda mimi Dunia ikusakame?

Au kunipenda mimi, Dunia ikuheremee?

Au kunipenda mimi, Dunia ikundame?

 

Kibwagizo.

Ndio! Mpenzi wangu, ndio mwokozi,

Ndio! Mkombozi, ndiwe mganguzi,

Ndio! Mtatuzi, ndiwe mfariji,

Au kunipenda mimi Yote haya upitie?

Au kunipenda mimi, Ndio wanipenda yesu?

 

Umepigwa pasina kosa, umetemewa na mate,

Taji miiba wamekuposa, damu yako niifute,

Ulale kaburini sasa, nataka nikufuate,

Au kunipenda mimi, Mateso haya upitie?

 

Au kunipenda mimi, dunia ikuchukie?

Au kunipenda mimi, dunia sikutambue?

Au kunipenda mimi, dunia sikusikie?

Au kunipenda mimi,maumivu upitie?

 

Japo umenilisha, japo umenivisha

Japo umeninywesha, dunia umenionesha,

Tena umenifundisha, nijifunze kusamehe,

Au  kunipenda mimi, mema uniachie?




No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...