Sunday, September 8, 2024

HADITHI: WAMEZIDI sehemu ya tatu



Waziri Beni alipandwa hasira akaendelea kumwaga mate 🤤 "Sawa miaka miwili iliyopita niliitia hasara Serikali kwa kufanya uamuzi wa kwenda nje ya nchi kuomba msaada wa Neti za kujifunika usiku ili kukabiliana na makali ya umbu, wananchi wasiteswe na makali ya ugonjwa wa Maralia . Ninakubali kuwa safari yangu iligharimu shilingi za kitanzania millioni mia nane na mimi nilipewa msaada wa Neti za millioni mia nne."Waziri alipumzika kumwaga mate Kisha akaendelea tena.

"Wananchi wengi sana walihoji kuhusu ile Safari yenye hasara lakini Mimi kama Waziri wa Fedha sikujali, mtimani nilijisemea 'waache wanene🌞 mchana usiku 🌖watalala.' Hatimaye wakanyamaza kama vyura 🐸waliotibuliwa kisimani."

"Sikiliza mume wangu wananchi sio watu wajinga Kuna Mshairi mmoja aliwai ghani Shairi lake akisema 'Siafu wakikazana nyoka utoka shimoni'  waogope Wananchi kwa umoja walionao ni kama siafu wanaomg'ata adui nyoka ili atoke kwenye makazi Yao . Wananchi ni kama siafu ambao watakuondoa madarakani." Mke wa Waziri aliongea 

"Wananchi hawana nguvu ya kuniondoa madarakani, wao hawakuniteua niwe Waziri bali Raisi ndiye aliyeniteua  na ndiye mwenye haki ya kuniondoa."

"Jiangalie mume wangu, marafiki wanaweza kuwa wanafki sifa yao kuu ni kwamba katika kipindi Cha furaha watakuwa bega kwa bega kusheherekea furaha lakini katika kipindi Cha huzuni watakutema na kukukimbia kama nguruwe pori."🐗🐖

"Uongo mtupu👺, siyaamini maneno Yako, Mimi ni mtu wa watu na watu hawataniacha kamwe." Kwa hasira Beni alinyanyuka juu ya sofa aliloketi akaenda chumbani kwake kujilaza kitandani.

.................

Uzuri wa ile Safari ya kwenda Ulaya walifika salama ndani ya hoteli kubwa ya kifahari... Ndani ya hiyo hoteli Kila kitu kizuri kilionekana: Swimming pool, viwanja vya michezo kama Basket ball, net ball na football, kumbi za sinema, kamari na anasa nyinginezo. 

Nje ya mahandhari  ya ile hoteli walihitaji kwenda kutembelea Jiji la Manchester wakatizame tizame uzuri wa hilo Jiji, fahari ya hilo Jiji kumbi za burudani na kadhalika. Kitu kingine kilichowaleta Ulaya ni pesa na pesa hizo zipo mikononi mwa Waziri Beni, akiombwa anatoa sio tu anatoa bali anazichezea kwa kuwarushia wapambe wake pale anapokua bwiii 🍺🍾 amelewa chakari. Ni mlevi asikuambie binadamu hata ndani ya Bunge yeye uingia amelewa. Uzuri wa pombe yake anajielewa, anaelewa anapaswa kufanya Nini akiwa kazini, anaicontrol pombe ili asigundulike mapema... Maana waswahili wanasema pombe sio chai na chai sio pombe🤣.

Asije akaumwaga unga bure, kisije kibarua chake kuota unyasi, Laaulah!😶  Ataenda wapi Waziri Beni, angali Bado hajajenga nyumba yake Binafsi sababu anaitegemea hiyohiyo aliyopewa na Serikali akae kwa muda wote wa utumishi wake. Mmh!🤔 Atafanya Nini Beni iwapo atamwaga Ubufu (unga) hajajiwekeza popote pale, hajajiongeza Wala Nini! Au watoto wake watatu Mika, Benson na Dianna watamfadhili?. Sijui kama watamfadhili🚶🚶‍♀️🚶‍♂️maana nao wanamtegemea baba Yao aliye Serikalini, awalishe, awanyweshe, awavishe na awasomeshe huko Mexico, New York na India wanakochukulia Madgree Yao.

Beni ana usemi wake unaomuongoza Kila siku katika starehe na anasa za Dunia : 'Life is short, maisha ni mafupi.. Wacha niponde Raha na starehe... Hakuna faida Wala maana ya maisha'  Huu ni usemi unaomuongoza. Anajali sana kazi lakini hayajali maisha yake Binafsi. Hataki kuongozwa na mkewe👩‍🦯 anataka Wapambe 👪👩‍👩‍👦‍👦 wamuongoze ndio maana Kila litokalo mdomoni mwa Wapambe analitilia maanani, analiterekeza haraka ipasavyo, yupo mstari wa mbele kuunga mkono.

............

Ni siku ya tatu Leo Beni anaponda Raha yeye na kampani yake. Max na Rose wametoka kidogo kwenda pahali, hawajamuaga Beni, wamemtoroka hapo ufukwe wa bahari ya mediterania wameenda ndani ya Moja ya hoteli zilizopo ndani ya Jiji la Manchester, hawana wazo lingine zaidi ya kuivunja amri ya sita ya Mwenyenzi Mungu. Beni amekunywa pombe hadi kuelewa wakati huo Mimi Viva, Dino, na Joe wanampooza kwa vicheko na  mbwembwembe za kujifanya wapo pamoja nae.

#####

Itaendelea sehemu ya 4.

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...