MBOSSO
"Nenda kaoge baba kijacho wangu.” Diva alimtania Mbosso.
“Nataka twende tukaoge wote mama Mbosso Juniour.”
“Tangulia my Love, si unajua kwamba natakiwa kufua mashuka yawe safi?”
“Ok. Love, sijui leo tutakula nini Baby?” MBOSSO alimuuliza Diva.
“Wewe unapenda tule nini Love?”
“Upendacho wewe Diva.”
“Ok. Mie natamani wangu wa mapenzi ndio uanze kunena.” Diva aliongea.
“Ok. Ungependa twende Hoteli?”
“ La, hasha! Sipendi. Mkeo nipo kwa ajiri yako, nitakwenda soko kununua Samaki, mchele, matunda na viungo kidogo.” Diva aliongea wakati huo Mbosso tayari kashavua nguo zake naye anaelekea bafu kusafisha mwili wake.
Tuendelee LEO
****
Nyumbani kwao Diva pakawa hapakaliki, mama na babaye Diva tayari walikwisha kumtafutia mume mwana wao Diva. Kijana mmoja sio mwizi kama Mbosso, kijana moja mpole, mstaarabu, mtulivu na uzuri wake ni mtumishi wa Benki ya CRDB. Ana kazi yake, ana elimu yake, mpole huyu bado yupo single boy. alipoambiwa kwamba kuna mdada mrefu mzuri anatafutiwa mchumba, basi huyu kijana kama mwendawazimu akalainika na kushika njia mfano wa Ng’ombe aendaye machinjioni.
Mapenzi umfanya msomi ampende chizi, Msomi amkatae Msomi mwenzie, lakini pia muhimu kufahamu kwamba macho hutazamia mali, vyeo, nafasi ya mtu katika jamii au sifa za mtu katika jamii. Lakini mapenzi ya kweli hayatazamii hivyo, mapenzi ya kweli yanajali, yanathamini na yanapenda pale panapopendeka. Kama wazazi wake Diva wangelijua kwamba mapenzi ya kweli yana uwezo wa kutembea hakika wasingelihangaika kumtafutia Diva mume wa kumuoa. Kama wazazi wa Diva wangelijua kuwa mapenzi ya kweli yana upofu, Wallah! Wasingehangaika kumchagulia mume wa kumposa mwana wao mpenzi Diva.
Mume sio kama nguo ya mtumba, walijue hilo, mume sio kama picha za sinema walijue hilo, mume sio mchezo wa sandakalawe. Suala la wao kumtafutia Diva mume ati kwa sababu ya kutopendezwa na penzi la Mbosso yawezekana wamekosea lakini pia mawazo yao muhimu yaheshimiwe hata wao muhimu waziheshimu hisia za mwana wao mpenzi Diva.
######
“Diva mwenetu mpenzi, huyu kijana unayemwona mbele yako anaitwa Samsoni au kwa kifupi upendelee kumuita Sam mzuri.” Babaye Diva alimtambulisha mgeni aliyeletwa hapo nyumbani siku nzuri ya leo, Jumapili.
“Ninashukuru kufahamiana nawe, karibu sana mgeni wetu, jisikie hupo nyumbani.“ Diva alimkaribisha yule mgeni kijana mmoja mtanashati, mzuri wa sura, umbo na haiba. Mtu mwenye heshima zake, hayupo rafu rafu, kama vile Mbosso alivyo, yeye ni mtu mwenye heshima zake japokuwa bado yungali singo hilo nalo halimtii wasi wasi anajua kwamba wanawake wapo na uzuri mmoja wa hao wanawake si mwingine bali ni huyu mrembo aitwaye Diva.
Jambo ambalo kidogo huyu kijana aitwaye Samson analifurahia, anafurahia kuwa na mwanamke msomi wa elimu ya juu, msomi wa Sheria. Waoooh! Hadi raha, mke msomi, mume msomi na watoto watakuwa wasomi, ndizo fikra za Sam mzuri wakati Diva hafikirii hivyo. Fikra za Diva zipo kwa huyu kijana Jambazi, mwizi aliyeuteka moyo wake, mwizi aliyeiba mtima wake. Mara baada ya salamu na utambulisho mamaye Diva akaongea.
“Mwanetu, huyu kijana umwonaye hapa mbele ndio chaguo letu, mumeo mtarajiwa tuliyependezwa naye, Baraka zetu na heri zetu zipo juu ya huyu mume bora aliyependezwa na wazazi wako.
“What?” Diva alipigwa domo wazi, akiyashangaa maneno yale aliyoyanena mamaye mpenzi. Babaye akafungua kinywa na kunena.
“Usishangae mwanetu, sisi wazazi wako tunakupenda ndio maana tunafanya hivyo. Tizama tumekusomesha, tumekupatia vyote unavyovitaka, hatujakunyima kitu chochote maishani mwako, tumekufurahisha kwa kadri ya uwezo wetu. Basi mwanetu mpenzi ujue sisi wazazi wako hatuhitaji kitu chochote kutoka kwako bali tunahitaji umpokee huyu kijana Samson awe mchumba wako na baadaye mjapozoeana mtapanga mambo yenu ya ndoa, kama ujuavyo tena mambo mazuri hayataki haraka.” Baba aliongea.
“Mwanetu Diva, sisi wazazi wako tunakupenda sana, wazazi wako hatupo tayari kukuona unapata shida, unateseka au kutaabika, ndio maana tunafanya kila jambo ambalo tunaweza ili uwe na furaha. Yanini kuona mwanetu msomi mwenye Degree yake, Degree ya Sheria anakubali kutembea na chizi kichaa aitwaye Mbosso? Chizi ambaye hakuna asiyemjua hapa Dar es Salaam. Ni chizi anayetafutwa na vyombo vya Dolla kila ikiwa leo. Mpenzi, jihadhari kabla haijakufika hatari, usidharau mwiba utakuchoma, usicheke jema baya litakuita.” Mama aliongea kwa kirefu.
“Ninakupenda sana Diva, wazazi wako wamenieleza kila kitu kuhusu wewe, nimekubaliana nao, na mimi nipo radhi kushiriki katika kukufanya ujisikie hupo tofauti na zamani.” Sam mzuri aliongea kwa kifupi, Diva angali yupo kimya hana neno la kuongea.
“Mwanetu, narudia tena kusema.” Mamaye Diva alihitaji kuongea.
“Wewe ni msomi, unapaswa kuolewa na msomi mwenzio, kumbuka kwamba hata mimi mama yako ni msomi, ndio maana nimeolewa na baba yako aliye msomi zaidi, tangu nimeolewa na baba yako sijawahi juta bali nafurahia maisha, riziki njema atupayo Mwenyezi Mungu, yanini wewe binti wa kisomi umpende yule chizi, taka taka, Jaha na debe la uchafu? Muache huyo chizi akawapende machizi wenzie bali wewe uwepo na Samsoni wako ukiwa na furaha, raha na amani.” Mama aliongea, Diva angali yupo kimya.
“Ok. Baba na mama, nimewaelewa, basi nipeni muda mzuri nikae chini na kutafakari yale yote mliyoyanena kwangu, nijapopata jibu sahihi nitawaambia na hata kama sijapata jibu sahihi nitafikiria zaidi na zaidi.”Diva aliongea maneno ambayo wazazi wake walianza kuingiwa na matumaini wakiamini kwamba sasa mwana wao ameanza kuelewa nini maana ya maisha mazuri yenye ufahari.
*****
KUTOROKA.
Jumatatu asubuhi Diva aliamka akiwa ni mwingi wa mawazo, mwingi wa fikra zilizouchanganya changanya mtima wake kwa jinsi alivyokuwa anawaza moyo wake ulimwambia, wazazi wake watakuwa wanamuonea kwa kumchagulia mwanaume ambaye yeye Diva hamtaki. Diva alihisi kwamba yawezekana wazazi wake bado wapo katika zile zama za ‘uprimitive’ zama za uzee, zama ambazo wazee katika koo au familia walikuwa na hamu kubwa ya kumchagulia kijana wa kiume mwanamke wa kumuoa, tena kijana mwenyewe ni yule ambaye wazazi wa huyo binti wamependezwa naye.
“Ni lazima nitoroke ni lazima niondoke hapa nyumbani, wacha nimfuate Mbosso wacha niende kwa yule ambaye moyo wangu umemchagua, mapenzi hayalazimishwi kihivyo, mapenzi hayaangalii status ya mtu na mtu katika jamii, iwapo mtu na mtu wanayatizamia mapenzi ati kwa sababu ya sifa za muhusika basi hao watakuwa wamepotoka, wamepotoshwa na pia hawaelewi maana ya halisia ya mapenzi.” Diva aliwaza.
Wakati huo Diva tayari alikwisha kukusanya kusanya mavazi yake, tayari Diva alikwisha kuzoazoa vikorokoro vyake, tayari Diva alikwishabeba kila alichoona kinafaa kwa ajiri ya kutoroka. Uzuri wake wazazi wake Diva tayari walikwisha kumfungulia Account ya hakiba, hakuwa na shida, alipitia Benki ya CRDB Lumumba naye akachota kiasi cha pesa ambazo aliona zinatosha kwa ajiri ya kuanzisha maisha mapya na huyu ampendaye Mbosso.
#####
“Umesema umetoroka nyumbani kwenu?” Mbosso alimuuliza Diva, wakiwa ndani ya Geto analoishi Mbosso.
“Yes, sidhani kama nitarejea tena nyumbani, wazazi wananilazimisha niolewe na mtu nisiyempenda wakati mie ninaye Mbosso wangu.”
“Duh! Sio mbaya lakini je, wazazi wako wakikutafuta itakuwaje sasa?” Mbosso aliongea kwa wasi wasi.
“Hilo halina shida, wanitafute au wasinitafute watajijua ilihali nimekwisha waachia ujumbe mezani kwamba wasinitafute, mimi nipo tena nipo popote duniani.” Diva aliongea kwa kujiamini.
“Sio mbaya, mimi ninakupenda kama unavyonipenda wewe.” Kwa mara ya kwanza Mbosso alimtamkia Diva juu ya mapenzi yaliyo moyoni mwake, ukitegemea siku zote ni Diva pekee ndiye aliyetanguliza mapenzi yake kwaMbosso, hakika moyo wake Diva ulimhitaji Mbosso kwa hali na mali.
“Je, umekwisha urudisha ule mkoba uliouiba Kariakoo?” Diva alimkumbusha mpenziwe juu ya ule mkoba ulio na fedha pamoja na vito vya dhahabu.
“Bado sijaurudisha, ungali upo vile vile.” Mbosso aliongea, wakati huo alichukua pisi ya bangi yake au dawa kama wanavyoita wao wenyewe, naye kaiwasha na kuanza kuivuta.
“Unajua sipendi.” Diva alimpokonya Mbosso ile pisi ya bangi kisha akaitupa chini na kuikanyaga.
“Sipendi unavyoendeleza tabia hiyo ya kuvuta moshi.”Diva aliongea, wakati huo huo Mbosso alinywea kimya kama mtoto aliyetandikwa bakora na mamaye.
“Ok. Ni hivi Mbosso, mimi na wewe tunahitaji kuondoka hapa Kigogo haraka sana iwezekanavyo.” Diva aliongea.“
"Kuondoka! Kwenda wapi?” Mbosso aliuliza.“Tutande popote pale duniani ilimradi tu huko tuendako kuwe tofauti na Mjini yaani Kijijini.
"Kwanini tuondoke? Kwanini tusiendelee kuishi mjini? Twafata nini kijijini?” Mbosso alidadisi.
Tukutane kesho
No comments:
Post a Comment