Sunday, September 15, 2024

LA MCHONGO...sehemu ya 4

 

MCHONGO

Sehemu ya nne

Tulipoishia

Marcus, nimekuvumilia sana mume wangu, nimekuvumilia kila neno niambiwalo na majirani kwamba unachepuka unaingiza wanawake wengine ndani kila nisafilipo Sasa leo nitamfunda huyu kahaba wakoNA na wewe pia ntakufunda.” Mwanamama aliyeniparamia Pale chini aliponibwaga aliongea na Marcus ambaye sasa tabasamu na ulevi wake ulianza kuchuja.

    "Nisamehe mke wangu, nisamehe tafadhali ni shetani alinipitia.” Nilimsikia MARCUS akiomba msamaha tena safari hii kapinga goti chini kwa aibu anatubu.Puuu PUUU PUUU pooo pooo mie nilietupwa pale sakafuni nilianza kuchezea kichapo.

Sasa endelea sehemu ya 4

      “Embu niwache mpuuzi weye, Nilimpigia kelele yule Jimama.

     B "Marcus aliniambia hajaoa kwaiyo kanileta hapa sio kimakosa” Nilimpigia kelele Jimama tipwatipwa lililonikwida kanga yangu limenikalia miguuni kwangu linaniponda kimya kimya.

        “Nikuachie wewe kama nani? Hivi hujui mume wa mtu sumu? Sasa leo nataka ujue na tena ujuwe sio kila akutongozaye weye waregea na kumkumbatia” Mwanama aliongea kwa hasira machoni wakati huo bado anaendelea kunipa kichapo. Ajabu yule aliyemtambulisha kama mtendaji na yule shahidi walikua kimya wakinitazama mwenzao napewa kichapo.

       “Mke wangu utamua binti wa watu, naomba samehe na umuache tukae chini tuongee na kuyamaliza,”Marcus alijitetea bado Jimama liliendelea kunipiga mie ambaye mwili haukuwa na nguvu sababu ya kulewa na kuwa hoi, damu zikinivuja puani na mdomoni.

      "Na bado wewe mpuuzi nikimmaliza huyu malaya nakumaliza wewe pia.” Jimama aliwaka akaendelea kunivuruga.

      “Nitakushitaki nakuambia, nitakushitaki kwa kunijeruhi mie nisie na hatia. Nishakwambia Marcus alisema hana mke yupo singo na mie nimemkubali kiroho safi.” Binti nisiyejua kujitetea nilipiga kelele sio kwa maumivu yale ya kupondwa kama Ng’ombe wa kikurya.

      "Nenda popote ukanishitaki ili uone kuwa pesa zangu zinanguvu kuliko maneno yako we malaya muuza tunda” aliongea kama vile ananifahamu na kanichunguza vilivyo. Ilinibidi niikamate ile mikono yake ya chuma wakati huo huo Marcus naye alisimama pale alipopiga goti akafanya kumtoa Jimama yule mwilini mwangu ajabu ya wale wanaojiita mtendaji na shahidi kimya wamesimama utadhani Mabodigadi.

     "Utaua mke wangu! utaua tafadhali, utaua binti wa watu.” Marcus alijitetea.

     “Acha niue, acha niue, uchungu wa ndoa yangu ninaujua mie mwenyewe,.” Jimama alitamka kwa makasiriko kadri alivyozidi kuondolewa mwilini mwangu ndo' na mie nilipata upenyo wa kutoka na baada ya kufanikiwa kutoka mwilini mwa yule jimama Mwenzangu! Mbona nilianza kumkimbia kama Roketi 🚀 ya Eloni Musc😅 pombe yote iliyeyuka ubongoni mbio mbio nilitoka ndani ya chumba cha Marcus nikapata upenyo na kuchoropoka nje nikapita lango kuu la uani tena sielewi Mlinzi alikuwa wapi maana lango lenyewe lilikuwa wazi. 

Wada mie nywele tipwa tipwa, mwili umevurugwa kwa mikucha ya yule mwanamke mwenye ngumi za shoka, damu zanichuruza puani na mdomoni. Nyie mbona nilionja joto ya jiwe.

     Salale! Kumbe Wada mie nalikua nakimbia uchi, uchi wa mnyama😭..

 baya zaidi nguo zangu naliziacha ndani ya nyumba ya mpuuzi Marcus kapu langu la matunda naliliacha huko na baya zaidi pochi yangu iliyokua na kiasi cha shilingi laki moja naliziacha sebuleni. Nyie! Pombe shikamoo😂 Pombe iliniponza, kujirahisisha kwa Marcus kuliniponza pia. Nikasimama pahali ningali uchi wa mnyama bahati nzuri pahali aishipo Marcus pametulia watu, vibosile wamejiketisha majumbani hawana haja ya kuchakula miguu yao vumbini. 

Mtima ukaniambia: 'Rudi ukachukue viwalo vyako, kapu lako la matunda na pesa zako juu ya Meza pale sebuleni.' 'Roho nyingine ilinionya: 'Mwana ukome! Hujashiba kipigo ilichopewa wataka nini kingine? Majuto??' Mmh! Nalikua njia panda. 'Mfaa maji haeshi kutapa tapa' Nalijiambia mie Wada nikaona heri nusu Shari kuliko shari kamili. Hima hima nikarudi kule nalikopewa kipigo, Kule nalikoacha nguo zangu pochi yenye pesa na kapu la matunda.

Liwalo na liwe lazima nijiongeze nikajibebeshe kilicho changu hata kwa lazima kuliko kukimbia uchi kama mchawi, chupi mkononi 😂😂😹🤭.(Nacheka kama mazuri). Nalitoka mbio za mkizi, Lango kuu bado lilikuwa wazi, nikalifungua kwa pupa na tahadhari moja kwa moja nilidhamiria kupitiliza sebuleni lakini mwenzenu nalipofika lango la sebuleni nilichosikia kabla ya kuingia. Ndani kilinifanya nipoteze nguvu, Almanusra nianguke na kuzirai.

    'Teh teh teh teh teh😹😹😹 ' nilisikia vicheko vya kishambenga 👌, Marcus alikua akicheka, Jimama lililodai ni mkewe nalo lilicheka kwa shangwe, yule aliyejiita Mtendaji wa kijiji akicheka na Shahidi wa uongo alicheka pia. Vicheko viliendelea vikakoma.

      “Kalichuna Buzi, kulila limemshinda.👌” Nilisikia jimama likichamba kishangingi.

      “Tuendelee hivyo hivyo, 'LA MCHONGO' linalipa.” Marcus alisikika akicheka tena 

     “Dada Frida mbinu ya kujifanya mke wa Marcus umeiweza” Mtendaji feki aliongea.

      “kusaka pesa Mtendaji, pesa utafutwa hata ukijifanya Mzimu wa Msyuka ulofufuka utapata tu pesa” Nilisikia Jimama like lenye sura mbaya kama ugali wa kimakonde, Lile lenye bichwa upaa kama mng'arao unga.

Akajibu mtendaji wa MCHONGO “Ungempa cha moto ungempa Cha kumzima kabisa” Aliongea kumaanisha mie ningelipigwa hadi kifo.

      “Kumuua tena, kumuua kesi Babu!  Tukiua twaenda Jela kuolewa na Manyampara 😹👌 Na la Mchongo hatulipati tena.” Jimama niliyemtambua kwa jina la Frida aliongea akakoleza tena maneno.

        “Na mie zamu yangu kesho kuna Kigogo kizito wa TRA la Mchango lazima. Ninaimani tutatoka na laki mbilimbili kila mmoja.

      "La Mchongo lazima.” Marcus alipalilia maneno“ Embu tugawane pesa za yule Malaya muuza Tunda, pochi yake ina shilingi laki moja kila mmoja atabeba elf ishirini na nne kwa kazi nzito.” Marcus aliongea.

    “Marcus na wewe, ah! Yaani unaacha kubeba Majimama yanayofanya kazi Benki unakuja kutuletea wauza matunda….. wana pesa gani wale zaidi ya kunuka shombo la kwapa na vundo la domo.” Mtendaji alilalama.

     "Tisa kumi tugawane pesa kila mmoja asepe zake si mnajua hata hii nyumba tuliyokutana ni La Mchongo.” Yule Shahidi wa bandia alihitaji wahitimishe. 

Basi mie kusikia wanataka kugawana pesa zangu roho iliniuma sikutaka kukubali upuuzi ule, niuze tunda kwa shida alafu La Mchongo wanilie haki yangu? Kupigwa nipigwe kumbe Mwanamke anayejifanya ni mmiliki wa lile Jumba ni mwanamke La Mchango ajabu hata Jumba lenyewe, Magari yao na kazi zao feki ni La Mchongo😭😢😿. We! Sikubalii👿. 

Nikafungua lango kwa hasira na kuingia ndani, kwanza wote walishituka pili wote wakaanza kujipanga wanirukie tena na kulisababisha, tatu hawakujua kuwa nshazinyaka mbaya zao.

      "Marcus umenidanganya kuwa huyu ni mkeo kumbe uongo ni bibi feki La Mchongo.” Nilibwata.

     “Wewe, wewe! Usitake kuniharibia ndoa yangu, kipigo ulichoonja hakijakutosha? Kuponea chupu chupi kwote huko bado tu unafuata hasara nyingine?” Marcus alinikemea akiwa ameninyoshea madole.

     “Unaongea ujinga Marcus kumbe ndo' michezo yenu kuwalaghai watu kwa lengo la kupata faida? Umepata faida gani kwangu mie muuza tunda.” Sikuona aibu kubwata  niliziziba kwa mkono sehemu zangu nyeti.

      “Toka, toka ndani ya nyumba hii haraka kabla hayajamwagika ambayo hayawezi kuzoleka.Marck alinifukuza kama Jibwa Koko.

        "Ninataka amani, nipeni nguo zangu, pochi yangu ya pesa na kapu langu la Tunda.....


Itaendelea kesho.

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...