KARAMU YA MAPENZI
Leo tumeadhimu, tuiweke na karamu
Sherehe yetu ni tamu, wawili tuliodumu,
Pasipo na uhasimu, ni miaka themanini,
Penzi hili vumilivu, penzi hili tulivu,
Mwanga wake angavu,laonekana bado bivu,
Penzi hili subirivu, halina doa wala kovu,
Ni miaka themanini, miaka tuliyodumu,
Wale wenye uhasimu, penzi kwao ni hadimu
Kushiriki kama timu, kuyatatua magumu.
Penzi lenye uhakimu, ulinzi na usalama,
Pendo mekuwa mwalimu, ni mzazi bora mama,
Mahaba yenye timamu bure hayana gharama,
Leo ninaitwa bibi, mwenzangu aitwa babu,
Wajukuu mashababi, wazuri wenye adabu,
Twawaombea maombi, wawe wema matabibu.
Tumeipanda milima, tumeyaruka mabonde,
Japokuwa tulikwama,tukasonga mbele twende,
Kwa zake mola huruma, twala arua na tende.
Leo twaweka karamu,kunyweni tena kuleni,
Leo twaweka karamu,furaha tena chezeni,
Karamu yenye mapenzi upendo pia mahaba.
Karamu yenye mapenzi, upendo pia mahaba,
Watoto wetu wapenzi, zipokeeni nasaba,
na Baraka zenye enzi, muishi katika 'haba
No comments:
Post a Comment