NIFUNIKE KWA MAPENZI.
Nifunike kwa mapenzi, kama tando la buibui,
Unizike kwenye zizi, nitulize moyo tuli,
nikuone kwenye njozi, haya mapenzi sukari,
usinijaze huzuni, unipe furaha kweli .
Nifunikie udongo, mapenzi yaote mizizi,
Pembeni kwenye ukingo, maji yenye utelezi,
Udongo uzae mihongo, idumu katika mapenzi,
Usinijaze huzuni, nipe furaha kweli.
Nikingie mwamvuli, mvua sinighiribu,
Kwe' masika na vuli, penzi lako la ajabu
Gharika ikiwasili, iniepushe adhabu
Dhoruba kwenye bahari, puta puta ni aibu.
Nizike kwa mapenzi, nitulie moyo tuli,
Penzi 'silo na majo'zi,twe' nalo twende mbali,
Sitopatwa na simanzi, nitapata raha kweli,
Huzuniko na majonzi, kwangu havitawasili.
Nikuone kwenye njozi, haya mapenzi sukari,
Nyimbo pamoja tondozi, ziniongeze .jeuri,
Mengi sana majambozi, yasiyotaka tunguri,
Nitakupa mwanagenzi, omba sana usijali.
Nisikutie huzuni, nipe furaha kweli kweli
Nikupende abadani, wewe kwangu ni wakili,
Penzi hilo la kijani, lina vito vya johari
Unizike kwa mapenzi, niridhikie mapenzi.
No comments:
Post a Comment