Monday, September 16, 2024

LA MCHONGO 🤣 sehemu ya 5 ( Mwisho)


 LA MCHONGO

Sehemu ya mwisho


         "Ninataka amani, nipeni nguo zangu, pochi langu la pesa na kapu langu la tunda mashetani wakubwa nyie."Naliwakemea Frida akanisogelea pale naliposimama.

        "Nimesema toka ndani ya nyumba hii umbwa mkubwa wewe!”

     “ Sitaki na polisi naenda.” Maneno yangu yalimwogopesha 

       “Aah unajifanya mjuzi et eeh? Akanivaa tena akaanza kunidunda mie ambaye pombe tayari kunitoweka sikulaza damu nikaanza kumdunda, tukadundana Fahari wawili. Ajabu Marcus, Mtendaji feki na Shahidi feki wakanivaa nao wakaanza kuniponda  huku wakipiga kelele 'Mwizi Mchawi, Mwizi Mchawi Mwizi Mchawi.'

         Uwiiii!! Nilirikoroga Wada mie nikaona hapa sasa yatanikuta kama ni kupona mara ya kwanza nimepona vip sasa niitwe Mwizi na Mchawi?  Baya zaidi ningali uchi wa mnyama,😳😢🤯🥶🙆 We! Mwenzangu akili za matunda zikaniambia kimbia wewe usirudi tena, Mwizi upigwa hadi kuuwawa, Mchawi uchoma moto 🔥 utajiteteaje kikaragosi weye? Embu toweka.

        Basi mie mpumbavu nikaanza kukimbia na kutoka ndani ya ile nyumba ya wapuuzi wale La mchango. Mbio mbio mbio nikatoka nje ya lango kuu la kuingilia, mbio mbio mbio bado tu masikioni nalizisikia sauti nyuma, La mchango walinipigia kelele 'Mwizi, Mwizi, Mwizi, Mchawi Mchawi, Mchawi kamata huyo Mwizi.'

      Nyie mbona niliogopa mie Wada na kujuta😢😢 Nilitoka.Mbiombio🏃‍♀️🏃‍♀️, Mbio bado tu kelele za Lamchongo ziliripuka💥 na kuwaamsha majirani pamoja na lnzi wengine wapendano unoko. 

       'kamata huyo, kamata Mwizi, Mchawi' walipigisha kelele. Jamani!! My day went bad😭 nalipatikana. Mbiombio, mbio ghafla nilishtuka natiwa Ngwala nzito iliyopelekea nianguke na kutua kichwa changu juu ya jiwe moja zito la chuma…. 'Maweeee!' Maumivu niliyopata  ni Mungu pekee mjuzi. 

Jamani nilishuhudia damu zikibubujika mdomoni mwangu baya zaidi meno ya mbele haswa yale ya juu yalitoka yote! Nyie nalikua chini Niagara gara kulia kwa uchungu wakati huo huo kundi kubwa la inzi na nyigu (Wambeya na wanoko) wenye hasira hasara lilinivaa na kuanza kunig’ata bila huruma.

       “Jamani mimi sio Mwizi!! Mimi sio Mwizi, mimi sio Mchawi!” Nilijitetea.

     "Waongo nyie, nyie ndio mnaotuharibia maendeleo ya Nchi na taifa kwa ujumla lazima uone joto ya jiwe.” lnzi wenye hasira walinikoromea.

     “Sio Mwizi jamani 😭sio Mwizi mimi😿😿 nimepatwa na majanga nipeni nafasi nijitetee.” Nililia lakini wapi lnzi wanoko hawakujali walidhamiria kuniangamiza.

 "Mdada mzuri kama wewe unaingia kwenye nyumba za watu na kufanya Ulozi?" nilikoromewa.

         “Unaacha kufanya jambo la maana ili kuleta heshima katika jamii wewe unaingia kwenye Nyumba za watu na kuanza kuroga.” Nilikemewa zaidi.

         “Wapendwa mie sio Mchawi na mwizi mie ni muuza Tunda Gongolamboto jamani!” Nilijitetea lakini Bado tu sikuaminika.

      “Leteni Tairi, Petroli na Kiberiti, Wizi na Uchawi koma Leo! Na iwe fundo kwao.” nilipigiwa kelele. Mie nguvu sina kwa kipigo, mie sauti haitokei tena kwa vile nilipondwa hadi ulimi 😛 ulikua mzito. Mdomo ukapata stroke ukatamani kunidondoka na kuniacha, Nyie😭 kweli kudanga kubaya. 

       Tairi lilileta na kwa lazima nalivishwa bila kupenda. Mafuta ya petroli yalimiminwa juu ya kichwa cha mie Wada muuza embe,Nanasi, katapela, chungwa na pela. nikainua macho yangu na kutazama huku na huko nikawaona La mchongo wakinitazama kwa jicho la dharau. Marcus alikua ameshika kigogo alichotumia kuniponda mwili huu dhaifu wa kufa akanitizama kwa dharau.

        Nyie!! Ndio yule Marcus aliyenipa offa ya chakula pale Masika bar? Ndo yule aliyenipeleka hadi ndani ya Jumba alilodai ni lake kumbe ni la mchongo? Ndo yule alinipa kilevi cha Jack DANIELI. Na mie nikamwambia kwa kudeka sikiwezi ajabu akatumia sauti yake tamu kunishawishi? Ndo yule niliyelala nae kitandani kwa zaidi ya lisaa limoja na wakati wote huo alizidi kutamania nimpende? Ajabu leo kuniponda na kutaka kuniua!

        

        Frida yule jimama La mchongo alishikia jiwe zito alililolitumia kuniponda nalo kichwani apate kuniua, mwanamke mwenzangu hana huruma zaidi ya kutaka kuniua binti nisie na hatia. MTENDAJI wa kijiji nae alishika chupa ya Bia ilovunjwa akataka kunichoma koo 😿, Mtendaji gani huyu jamani kama sio La mchongo? Kuna Mtendaji ambaye anatamani raia wapigwe na kuuwawa!? Aah, nimesahau kuwa huyu ni mtendaji feki tena La mchongo. 

Na yule shahidi La mchongo ndo' aliyeleta petroli na kiberiti mie Wada nichomwe moto na nyama yangu inukie ikaliwe na nguruwe ama nibakie mifupa na majivu. Jamani! Na BADO TU INZI WANOKO WALINITAZama kwa jicho la chuki na hasira.

          'Tiri Tori Tori toriiiii…' lilisikika Gari ya Polisi ikija kwa kasi ya upepo. Zile kelele za ile Gari zikawafanya La mchongo wote watoweke na kukimbilia nisikojua mie nilieponea chupuchupu kuwashiwa kiberiti. Inzi wanoko nao walianza kutawanyika huku na huko kuepuka ushahidi. Nakwambieni hata yule shahidi feki na mtendaji feki walikimbia kuwaogopa Polisi nikabaki pekee nimepona chupu chupu kuwaka moto.

*************

Mwenzangu mie nawashukuru mabwana Polisi wameniokoa roho iliyotakika kuteketea ndani ya tairi ya Gari iliyobaki kidogo ichomwe moto wa petroli. Ingawaje nipo HOSPITALI ninauguza majereha mwilini mwangu, lakini pia nimefungwa pingu pembeni ya kitanda nikisubiria kupandishwa Mahakamani eti kosa langu ni kukamatwa Uchawi na Wizi.

 Huo uchawi au wizi mie Wada nimeanza lini jamani? Nimemroga nani mie? Nimemuibia nani mie Wada muuza Tunda Gongolamboto?! Jamani La mchongo limeniponza.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...