Kuku wa kizungu
Sehemu ya nane
Yiaro alifika nyumbani kwaLaizer, muda ule Laizer alikuwa akimhudumia mbuzi wake aliyetoka kujifungua muda si mrefu, mkewe Laizer Swinje alitoka asubuhi ile yupo Porini kusaka kuni na matunda. Duka lao leo hii sio Duka tena, limefirisiwa kwa hila na kwa chuki zake Balozi ambaye kwa wivu alionao alihakikisha kuwa Laizer anaugeukia Umasikini aliokuwa nao miaka mingi iliyopita kabla hajawa mtumi wa Islama.
“Karibu Yiaro, karibu Mtumi wa Balozi.”Laizer alimkaribisha Yiaro.
“Asante bwana mkubwa, pole na majukumu yote? Ninaona mbuzi wako wanazidi kuongezeka.” Yiaro alitania.
“Ah! Wapi waongezeke hawa na njaa hii ya mifugo hapa Maasai land, wafugaji wanapigana na wakulima, mmh! Sidhani kama kwa ukame huu mifugo itaongezeka.” Laizer alimjibu Yiaro Mtumi wa Balozi “Ndivyo ilivyo Maasai Land, Wamaasai sikuzote hawapendi kujishughulisha na kilimo zaidi ya ufugaji, unajua kama na sisi tungelima tungelikuwa na akiba ya chakula cha Mifugo.” Yiaro aliongea.
“Najua kuhusu hilo.” Laizer alijibu.
“Sio mbaya, kuna barua yako, inasema Imetoka England, hii hapa ikamate.” Yiaro Mtumi a Balozi alimkabidhi Laizer ile Barua,Laizer aliposikia Barua imetoka England. Moyo wake ukamwenda kasi mapigo. Akaipokea. “Fungua basi, mbona waishangaa.”Yiaro alitaka kujua kilichoandikwa ndani ya Ile Barua.
“Oh! Usijari nitaisoma baadaye, kwa sasa nipo bize,”Laizer aliongea akaelekea ndani, amemuacha Yiaro amechukizwa kwa tendo la kushindwa kuujua umbea ulioandikwa ndani ya ile Barua. Muda si punde Yiaro akaondoka. Laizer akaingia ndani akaiwasha Karabai Faster faster akiwa pekee yake akaifungua ile Barua.
Kitu cha kwanza kukutana nacho ndani ya ule mfuko wa kaki ni Karatasi moja nyeupe imechorezwa Maua na mnuko mzuri wa Marashi ya Pemba na Unguja. Akaifungua ile Barua akaanza kuisoma.
ISLAMA.
ENGLAND.
20/05/2008
ARMOUR WANGU LAIZER.
Laizer wa moyo wangu, baba yake Tino. Tumaini langu haujambo? Ni miaka saba sasa kipindi kirefu cha muda tangu nimeondoka Afrika, nilikuahidi nitarejea na sasa ninataka kurejea tena.
Love ninajua kuwa nilikuweka katika wakati mgumu sana, mgumu wa kipindi. Ulinimiss Baba Tino, Ulimmiss Tino mwanetu, anasumbua anataka aje Afrika, aje akuone Baba wa damu yake.
Damu nzito kuliko maji. Love acha mwanao aje Afrika kumuona baba yake. Basi mpenzi katika msafara wetu nitaongozana na DAVIDI Mpenzi wangu wa zamani, PAMERA Shoga yangu pamoja na TINO mwanetu. Mpenzi utuandalie Makao mema. Hizo million tano zitumie kama mahitaji yako wewe pamoja na mkeo mpenzi Swinje, mie nitakapokuja na Campany yangu gharama zote tuachie nitazigharamia.
Wasaalam akupendayeISLAMA (MAMA TINO).
“Waooo!” Kila mstari wa ile Barua ulimtia Presha na mapigo ya moyo Laizer, moyo mapigo yalimwenda kwa fujo lo! Ujio wa yule aliyempenda zamani. Aki! Milima haikutani binadamu wanakutana. Kweli damu ya mtu haipotei hivi hivi.
Tabasamu pana lahaja lililipuka mdomoni kwa Laizer akaingiza mkono ndani ya ule mfuko wa kaki, akatoka na mabunda matano ya pesa, kuhesabu haraka haraka ni milioni tano Cash. Furaha, furaha na raha alijikuta Mori ya furaha imempanda anaruka juu kama mwendawazimu, anaruka ndani ya nyumba yake yenye kofia refu la bati.
###############################
Yiaro alirejea nyumbani kwa bwana wake Balozi, alipofika tu Balozi alimuuliza Yiaro.
“Ile barua ya Laizer ilisomeka kuwa inatoka wapi na wapi hapa Tanzania?”
“Ile barua haikutoka sehemu yoyote Tanzania bali ilisomeka kuwa inatoka England kwa wazungu.” Yiaro alijibu kwa ufasaha.
“What?” Balozi aliuliza macho pima kama mjusi aliyebanwa mlangoni.
“”Ndio Balozi, ile Barua imetoka Euorope.”
“England!?” mmh! Laizer hana ndugu England, atakauwa ni nani aliyemtumia?”
“ Nisijue mie, maana nilipoileta ile barua nilikwambia Customs yetu ni kuifungua barua na kuisoma au kucheki kilichomo ndani, ajabu wewe ulipiga kelele tusiifungue.” Yiaro kijana wa 22 Age mrefu, mwembanba Keisha baleghe tayari alimjibu Balozi Bwana wake.
“Oh! My GOD!! Ulipofika kwa Laizer ulimwona Laizer akiifungua?” Balozi aliongea amejaa wasi wasi. Bahati nzuri wakati huu hakuwa karibu karibu na eneo walipo wakeze, alijiketisha mbali na nyumbani, kama angeliketi Nyumbani basi Bi. Mkubwa angelimshambulia kwa maneno ya misuto.
“Ah! No, hakuifungua alidai ataifungua baadaye.”
“ God have Mercy! Una maanisha Laizer hajaifungua ile Barua.” Balozi alitilia mkazo swali lake, Yiaro asijue nini kinamfanya Bwana wake awe mkali namna ile.
“Sure, kitu kama hicho, alikuwa bize akitoa huduma kwa mbuzi wake aliye zaa muda si punde.”
“Yiaro Mtumi wangu, embu niache nikamsabahi Laizer.” Balozi Ole aliongea, akaingia ndani ametoka na mayai kumi ya kuku wa kienyeji pamoja na buyu la asali zawadi maalumu kwa ajili ya Laizer adui yake.
###
Balozi alifika nyumbani kwa Laizer kuna umbali kidogo na pahali anapoishi yeye na wakeze wawili. Alipofika akabisha hodi mara mbili tatu lakini bila tarajio hakuna mtu aliyekuja kumfungulia mlango sababu muda kidogo Laizer alitoka ana kwenda Benk Arusha mjini kutunza Pesa alizopewa na Islama.Amebadilika sana, siku hizi amekuwa mtu aliyeelimika tofauti na miaka saba iliyopita. Ole akaingia ndani ya geti kubwa nyumbani kwa Laizer.
“Ma’ Yoyo!” Balozi aliita asijibiwe. sababu Mama Yoyo mkewe Laizer hakuwepo nyumbani yupo kisimani kuteka maji pia amepita Porini kukata kuni.
“Laizer!” Balozi alimwita Laizer ajabu Laizer hakuitika sababu hayupo ametoka ni mwenye furaha tele ya kupata bahati nasibu kama ile.
“Wapi tena wenyeji wa nyumba hii? Ukimnya kama Pango la Ibilisi.” Balozi akaufungua mlango na kwa bahati nzuri mlango uliegeshwa ovyo akapata nafasi ya kuingia na kuutafuta ule mfuko wa kaki wenye Barua aliyotumiwa Baba Yoyo.
“Mmmh! Kiza totoro.” Akawasha Karabai iliyotelekezwa juu ya meza. Iliwaka pasina kupoteza muda Balozi alianza kuinama chini ya Mavungu ya Meza, viti na kuparanganyua masufuria na vyungu akiitafuta Barua iliyotumwa kwa Laizer. Bahati iliyoje akauona mfuko wa kaki, Furaha iliyoje akaketi juu ya Viti vya Laizer tabasamu jingi usoni akaaanza kusoma nje ya bahasha moyo mapigo yakamwenda kasi alikutana na jina Islama likiwa limeandikwa nyuma ya ule mfuko wa kaki. mbele ya ile Bahasha aliuona muhuri amabao kwa uhakika alijua ni muhuri kutoka England. mapigo ya moyo yakamwenda kasi haraka akachungulia ndani ya ile Bahasha kuona kama kuna Barua ataipata hakuipata zaidi aliambulia kuiona Dollar moja mpya inanukia vizuri, haraka haraka akaichukua ile Dolar moja akaificha ndani ya mfuko wa Serewili yake.
“Iwapi Barua kutoka England?” Alijihoji asipate jibu
“Yamkini imehifadhiwa chumbani.” Alijijibu fikirani. akaeleka chumba alalacho Laizer na Swinje mkewe. akapapasa kitasa cha lango la chumba cha Laizer na mkewe, hakupendezwa maana ulikuwa umekokomewa kwa ufunguo ulipitishwa ndani ya kile kitasa.
“Si haba! Chale zanicheza yawezekana Islama atakuja Maasai land.” Alijiaminisha.
Teh teh teh teh. Alicheka kidogo.
“Ni furaha kwangu ni amani Moyoni mwangu Islama anakuja na ujio wake lazima nimpokee, lazima niwe karibu nayeye tena.” Furaha ilimjia Balozi.
“Zubaa zubaa mwana umkose! Nimempenda Islama. Je, nimkose? haiwezekani kwa sasa nimekwisha boreka, nimekuwa mzuri zaidi, nimekuwa kijana tofauti na zamani.” Akajitizama tizama mwili wake ulivyo akajiona yeye bado ni mali ya kupendwa na mabinti kisha akaurejea mlango wa kutokea nje akaufunga vizuri ile Bahasha ya kaki akairejesha pahali pake naye akafanya kuondoka kurejea nyumbani kwake mwingi wa furaha na matumaini.
Itaendelea.

No comments:
Post a Comment