1
Sikilizeni habari, njema iliyotakata,
Nanyi mpate ujasiri, mazuri kuyafuata,
Mila pia desituri, zenye mafuta ufuta,
Kuziona afadhali, kwa mapenzi yenye heri
2
Yule mwenye mapenzi, apendwa na wengi,
Yeye ni mkurugenzi, miliki wa Mali mingi,
Kapewa na mwenyenzi, vizuri vilivo' rangi,
Elimu pia ujuzi, ubora wenye musingi.
3
Apendwa nao wengi, Hana mfano duniani,
Hekima yake nyingi, Mufalme sulemani,
Kamwe sipate vigingi, ujazo wake amani,
Mabaya hayamzengi, mazuri huyatamani.
4.
Ana moyo wa kutoa, hatoi kusitasita,
Mwilini Ameloa, huruma zinazoita,
Si choyo wa kutoa, hutoa mengi matuta,
Ndiye uyaondoa, mabaya yalo utata,
5
Mwenye mapenzi tajiri, mengi Mema ufuata,
Ni mtu mwenye adili, hekima nyingi saburi,
Ni moyo wenye kujari, Haki umoja na kweli,
Daima huwafikiri, wale wenye hali duni.
6
Daima kuwafadhili, watu wenye hali duni,
Kuwagawia vibari, vyenye Mali zilo Shani,
Kwanini sio bahiri? Hutoa Toka moyoni.
Hatoi moyo kafiri, hutoa vinono vya mbuni,
7
Mwenye mapenzi tajiri, Mema mengi humfuata,
Taishi kwenye uzuri, fahari ilotakata,
Mwenye kupendewa mbali, jinale limetukuka,
Yenye ubora mashauri, watu daima tuyafuate.
No comments:
Post a Comment