Mapenzi Mema.
ππ
Natuijenge dunia, yenye mapenzi mema,
Dunia yenye ujamaa, mapenzi tuyape heshima.
Upendo uwe neema, msamaha pia rehema,
Pasina tumia gharama, tupendane daima.
pasina tumia gharama, tupendane daima,
Tuishi kwa kujituma, tuzipokee karama.
Mapenzi yetu yatavuma, tayabariki karima,
Matunda tutayachuma, furaha italindima,
Mioyo iwe bima, tuuzike uhasama,
Daima tukijinyima, mapenzi yawe salama,
Daima tukijinyima, mapenzi yawe salama,
Tunyime vile vya gharama, mapenzi yatalindima.
Mapenzi yajenge hema, shamba yapate kulima,
Yaipande mbegu njema, yavune Dhahabu njema,
Mapenzi yajenge boma, lidumu likadumika,
Liwe mfano wa Jua, giza litafunika,
Liwe mfano wa Jua, giza litafunika,
Mwanga utajikunjua, mabaya tutayazika,
Mwanga utajikunjua, mabaya tutayazika,
Mema tutayajua, mapenzi taimarika.

No comments:
Post a Comment