Friday, March 13, 2026

Two birds on the tree πŸŽ„

 NDEGE WAWILI MTINI.



Kuna ndege wawili, wapo juu ya miti,
Wana rangi  bahari, pendo limejizatiti,
Wana mbawa  johari, macho madini ya bati,
Ndani kwenye viota, wametulia tuli.


 
Tuli tuli tuli tuli, maji mtungini.
Sauti zao kasuku, na wivu wao chiriku,
Wakatoka tuku tukuy, macho wameona vitu,
Chakula alacho kuku, hindi mtama mafuku.


 
Njaa haina huruma shibe mwana unikome,
Ndege wakajiparama, kuukimbia ukame,
Tumbo lipate neema, shika jembe ukalime,
Raha ukijipa mwenyewe, jipimie uridhike.


 
Raha ukijipa mwenyewe, jipimie uridhike,
Meno yakasuguliwe, tumbo jaa lkipasuke,
Watanga tanga aguliwe,. Huo mshike mshike,
Dunia mti mkavu, kiumbe siegemee.


 
Hatai! Hatari! Hata! Ooh! Msalie mtume,
Matumbo yakata kata , ni wapi wajiegemee,
Tam ufuta kashata, eh! Mola wahurumie,
Walikuwa zumbukuku, limbyukeni wa chakula.


 
Jamani dezo yaua, vilivyo bure mtego,
Ndege hawakujua, kasuku yao mipango,
Sumu meibugua, megeuka mipingo,
Wapenzi sha tokomea,kuonana majaliwa.
 
 
 


No comments:

Post a Comment

Good love

  Mapenzi Mema. πŸ’–πŸ’– Natuijenge dunia, yenye mapenzi mema, Dunia yenye ujamaa, mapenzi tuyape heshima.   Upendo uwe neema, msamaha pia rehem...