Friday, March 13, 2026

NELIA

 NELIA




Furaha hya mapenzi, awepo umpendaye,

akupae usingizi, presha yako itulie,

huyo ndiye mtetezi,shida zote zilile,

nawe uwe mkimbizi, matatizo atatue.


 

Nelia aliolewa, na Mume mwenye mapenzi,

Kazi akatafutiwa fundi wa kushona mavazi,

Na watoto wakajaliwa, na wakike na wakiume,

Maisha yakawa murua,wakiwa kwao Zimbabwe.


 

Furaha ya mapenzi, Nelia ilimsafisha,

Furaha ya Mapenzi, Nelia ilimtakatisha,

Mume aliye ujuzi, kwa yeye akajikesha,

Mapenzi yalivyo matamu, utamu usio kwisha.


 

Wealisema wahenga mapenzi upepo,

Walinena hekima, mapenzi maua,

Walisema busara, mapenzi sabuni,

Ndipo yakatimia, mapenzi kizungumkuti.


 

Ajari yenye simanzi, Nedlia akawa mpweke,

Mumewe ametwaliwa, kamuacha pekee nyake,

Urithi alojivunia, shemejiye akampoka,

Watoto alowalilia, Nelia anasikitika.


 

Shemejiye akampoka, mashamba ya kilimo,

Biashara iliyoboreka, mifugo itupayo nyama,

Nyumba aloisimika,watoto ni wake mama.

Hakiba aliyoiweka, mali walizochuma

Shemeji akamtaka Nelia awe mke mwema.


 

Nelia hana raha, ameachwa mjane,

dhuruma pia mzaha, matusi atukanwe,

uonevu katika haki, moyo ukamtuma,

kuizika hiyo chuki, yenye wingi wa hujuma.


 

Mahakama akafika, kesi ikanguruma,

Haki ikatendeka, mama kapewa chema,

Mali alizopokwa, Nelia akarejeshwa,

Sheria ndio


msumeno, makali makali kuwili.


No comments:

Post a Comment

Good love

  Mapenzi Mema. πŸ’–πŸ’– Natuijenge dunia, yenye mapenzi mema, Dunia yenye ujamaa, mapenzi tuyape heshima.   Upendo uwe neema, msamaha pia rehem...