MIPASHO YA MAMSAPU
WATABAKI NA LABDA
Sehemu ya kwanza
“Teeh teeh teeh,๐๐ ai babu we!”๐ Nacheka mie, nacheka vizuri, nacheka kwa furaha, nacheka tena narudia kucheka, ‘teeh the teeh,’ ๐คฃ๐basi shoga nakwambieni hadi raha, raha nijipe mie mwenyewe si walisemaga wahenga “ MWENYE WIVU AJINYONGE” basi na mie ninasema “WENYE GERE WASAGE CHUPA, WENYE KIJICHO WAKAJITOSE BAHARINI,”๐๐♂️ maisha haya ni yangu mie Mamsapu na mume wangu Pompo, kiwaumacho nini? Kinachowauma kiwaume tu, tena mlie nyie mabibi wenye sura mkomavu, hata podali inawakataa, ndo’ iwe Rosheni, teeh teeh ๐คฃ mlie tena mliage, hamna haya nyie, kutwa kuchwa kunisakama kwa maneno ya umbea na ushambea, nawambieni “MTABAKI NA LABDA!”
Washazoea na sasa ninawakanya mtoto wa mwenzenu na mie ninae mama kamwe mama yangu hakukwama kanilea kwa hekima, saburi na busara, hadi hapa nilipofika ni mkono wa mama yangu๐คฑ, tuone sasa tuone kama mtaja kufikia levo zangu, levo za majuu JUU KAMA MAWINGU.๐ช️๐ค️๐ Niwaambie tena niwaambie HIZI NI ANGA ZANGU, ANGA ZA MWENYEWE, anga zangu mie Mamsapu mama la kitanga kule mapenzi na mahaba yalipozaliwa, si nyie KIGOMA MWISHO WA RELI, teeh teeh (nacheka mie) mshakuwa KATERERO michepuko nyie, VITONGA nyie, nyie ni miteremko WATU WA OOOOVYO.๐
Kutwa kuchwa kunijazia list ya maneno ya USHILAWADU (umbea) na kwa huo ushilawadu wao kamwe siwapi posho, wenyewe wanajua fika kuwa UMBEA HAUNAGA POSHO, Nyoooooo….. walie tu, kuzifikia levo zangu mbona watangoja, tee teeh teeh (nacheka mie) watangoja hadi yesu✝️ arudi tena kuwachukua kondoo, ๐teeh teeh teeh teeh nicheke mie tena nacheeeeka kwa dharau, maringo na kebehi
Kucheka haki! Tena haki yangu au sio Shoga? Kucheka kwaniongezea kalenda za kuliona jua, maisha ya Kobe, marefu kama vocha, sifi siozi Wala Sina baya. Enyoooo eti Mwaya kwanini nisiwacheke maboya hawa? Maboya ambao mie najua fika kuwa MIDOMONI MARAFIKI LAKINI KUMBE MIOYONI MAADUI, aku! ๐Babu we, waniteme na tena wanitapikie mbali, waniache jamani, waniache mie nina HAMSINI ZANGU sijala cha mtu, sidaiwi na mtu na kwa kifupi mie mama wa kebehi niawaambia hivi “ KULA๐ฎ๐๐ HAMLI MTAISHIA KUNAWA,” washa sahau fika kuwa MWENYE NYUMBA ๐กHAKIMBII UVAMIZI WA SIAFU, Umbwa hawa, UMBWA KOKO midomo ๐คtu yawasumbua.
Mie Mamsapu sio MDOGO DOGO, kama wao wanaojifunza maisha kwa kukopi na kuigiliza, nasemaje NISHAFUNDWA tena NIKAFUNDIKA nimepitia UNYAGONI sasa mie ni KUNGWI, NAFSI HIYO NINAYO,NGUVU NINAZO, UWEZO NINAO NA FURSA HII KWANGU HAINIPITI, inanitafuta kila kona ya dunia ai! Waooo, MWENZENU N’SHAPENDWA, natambua fika kuwa maisha yetu ni wakati na wakati ni mida, mida inaniruhusu NIWASUTE, NIWACHAMBUE CHAMBUE KAMA KARANGA Mabedui ๐ฟ๐นna mahayawani hawa, YA KWAO YAMEWASHINDA SIJUI YA KWANGU WATAYAWEZA?
Mmmh! (Naguna mie) Hawana ishu za maana hata wakijiweka bize ili kuyapeleleza ya moyo wangu nasema hivi hawatakamilisha ripoti zao chafu chafukoge, nishatulia na wangu wa moyoni Pompo๐๐ฉ❤️๐๐ฉ ni mtu mzima anaye jielewa, anayaelewa maisha yakoje na maisha yanataka nini? Sio nyie MAZUMBUKUKU hamyawezi MARUDI, yamewapiku marudi ndio mbaki kujuta majuto ya mjukuu ‘teeh teeh teeh’ nacheka mie, au sio shosti HUU MCHEZO HAUITAJI HASIRA upole ni nafsi yake. Mie natoka TATU BILA ⚽⛹️ati wananilazimisha NGOMA DROO, Neva! HAFIKI MBALI KIPINGU HATA AKENDA MBINGUNI .
Na leo nayamwaga ๐ฆtuone sasa kama watayazoa, YAMEWAFIKA SHINGONI wangali wanatapatapa, yangu mie macho,๐ hivi ninavyo ongea mbona kila mtu huko kitaani anawa NYANYAPAA kama vile wana ugonjwa wa UKOMA. Nishasikia maneno kibao jamii inawasuta kwa kuwaambia shoga zao, WAOGOPENI WATU HAWA, washalaaniwa MBELE HAWANA NYUMA HAWANA, hawaeleweki wapi mwanzo wapi mwisho” Teeh teeh teeh, ๐คค๐n’cheke mie.
WIVU KIDONDA, WAKISHIRIKI WATAKONDA, nishawasoma zamaani wanajua fika kuwa mie ninae mwandani, laazizi wa moyo๐๐ wangu, sioni haja ya kuirudia hiyo sentensi bali ukweli wajue kuwa mie Mamsapu na Pompo ni wawili tulofungamana, asiwepo wa kutufungua zaidi ya Mola muweza, kwanza YA MUNGU NI MENGI YA WANADAMU MACHACHE , sioni mfadhaiko kusema ukweli kwa kutumia mifano iso na mafumbo, wao binafsi walijua fika kuwa itakuwa simpo kumpata wangu wa moyoni pompo.
HATA WAKISUGUA BENCHI mara milioni zaidi lakini kamwe hawawezi kifikia LEVO HII nipo kwenye anga zangu, wacha nijilie vyangu, vyangu ni VINONO vilo NONOKA, vilo TONONOKA si kama vyao vya kutapika na kutia kinyaa na kichefu chefu Mmmh! Shoga unajua fika kuwa vya kwao ni matapishi? Na matapiko hayo wakayatupe jahani sio ati wanijazie Inzi kwenye SITA KWA SITA zangu, enyoooo WALIE TU.
Acha basi Nyoyo nikupe mfano mdogo mdogo wa huyu bibie mwenye kijicho na kidudu mtu aitwaye MARIAMU jinale zuri lenye wingi wa Baraka lakini ubaya wake ni kwamba Baraka alizopewa hawezi kuzitumia, MAMBO HAYAWEZI, MAPENZI HAYAJUI, MARUDI YAMEMPIKU NA KUMSHINDA, yupo yupo tu mtoto mwenyewe ni mtoto wa jana bado MCHELE MCHELE (dogo dogo) japo uzuri ni wake, sura ni yake, mrefu sio mwembamba sana lakini kwa yale yaliyo moyoni mwake tofauti na uzuri alionao.
MWAYA KWA LEO NAKOMEA HAPA TUONANE KESHO MAJALIWA, NIKUPE UONDO UONDOKE.
“
No comments:
Post a Comment