MIPASHO YA MAMSAPU
WATABAKI NA LABDA
Sehemu ya pili.
“kaolewa?”👰💍 Yes, Kaolewa,kawekwa ndani akiwa na mtoto mmoja wa KUPANDIKIZWA, yaani mwaya mtoto aliyenaye Mariamu sio wa huyoo mumewe anayedunda naye, shauri ya umalaya na ufuska ndo’ maana kamsaliti mumewe na ubaya wa yule mwanamke mumewe hana habari kwamba huyo binti mtoto aliyezaliwa kwake sio mwanaye bali ni mwana wa JIBABA lingine lisilojulikana.
Shoga, embu nikuulizeni :” Sasa kama Mariamu ana wa kwake mume, inakuaje anamfuatilia roho wangu Pompo? Ama labda anataka NIMKWIDE 🧨blauzi yake,nimtwage makofi, nimjazie watu NYOMI, nimwaibishe mbele ya KADAMNASI, NIMPAKE MATOPE achafuke, ‘teeh teeh teeh’🤣😅 uwezo huo ninao, niko fiti najiweza, nishindwe nini na huyo KIMBURUKUTU tamaa, kwanza yeye bado kwangu ni mtoto dogo dogo , MCHELE MCHELE, haniwezi kwa lolote lile, ‘ ‘mfyuuuuu’ (Namfyonya, afyonyeke)
Dunia 🌍🗺️ishakuwa kijiji kuna mengi ya kujifunza na kukumbuka mengine ovyo ovyo tu, kama alivyo Mariamu, yupo Ovyo ovyo LAFU LAFU. Ndo’ kafanya KUMMENDEA mume wangu Pompo n’shasema Dunia ishakuwa kijiji hakuna siri tena, Ulifichalo ⚫gizani litaonekana💡 mwangani,ulifichalo mwangani litaonekanagizani, kwanza mapenzi sio kulazimisha Mariamu kamtaka Pompo Moyo wangu kwa lazima, ajabu Pompo kamkataa na ubaya wa huyu bibi MCHEPUKO angali analazimisha.
Nyonyo embu niulizeni, “ Ni kwanini Mariamu amekuwa king’ang’anizi? Ni kwanini Mariamu ana mg’ang’ania Pompo roho wangu?” ipo sababu nitawajibu shoga zangu, nitawajibu ni kwasababu wangu anauwezo, wangu sio mtu wa kukanyaga vumbi bali ni mtu mwenye hadhi 💰🏧yake, ana gari zake za kubadili badili, biashara zake zinaenda good, ni mtu anayejielewa na pia anaelewa maisha yanataka nini. Kwasasa tayari tume kwisha wekeza kwenye nyumba zetu tatu, moja ipo MBEZI BEACH, ya pili ipo KIMARA TEMBONI ya tatu ndo’ hii yenye HOROFA TATU tunayoishi hapa KiGAMBONI.
Jamani niachwe niishi, niachwe nijilie matunda yangu, niachwe nipumue na Pompo roho wangu. Kama ni kupanda tushapanda mie na Pompo, kama ni kuvuna sioni aibu kusema ninavuna na roho wangu Pompo, kula lazima nile na roho wangu Pompo, ai! Babu we, mambo baaaaaadro.
Kama ni dhiki basi hiyo dhiki ikupate wewe mwenyewe Mariamu, mie sinaga njaa kamwe, sinaga shida, NIMETULIA TULI KAMA MAJI MTUNGINI, sioni raha ya KUDANGA kama ewe bibi MDANGAJI, huchoki KUTANGA TANGA KAMA KUKU, KUTWA KUCHWA KIGUU NA NJIA, lo! Jamani ushayamaliz Malapa kwa kunyunda aridhi, ushavikomaza visigino kwa kutanga tanga kama kuku, lo! Wewe ni KAUKA NIKUVAE huna mbele huna nyuma, bado upo upo tu kama kichaa mwendawazimu.
‘Teeh teeh teeh🤤😆 (Nacheka mie) bibie haridhiki au labda haridhishwi ndo sababu haeshi kumsema mumewe kitaani ati mumewe ana KIBAMIA, na kibamia chenyewe KIMEDODA, KIMEBUMA na KUCHACHA kama vile MAHARAGWE YA MBEYA maji mara moja tu tayari yashaiva. Mmmh! Yangu mie macho mwenye masikio asikie.
Amepungukiwa nini Mariamu, mbona hajitumi? Hajui kuwa yeye ndiye mwenye jukummu kubwa la kumjenga Mzee baba (mumewe), amjenge kwanza kwa vyakula bora vinavyotia NGUVU na MAFUTA,amjenge mumewe kwa MAZOEZI ya mara kwa marra, muhimu amjenge, yeye binafsi anajua fika kuwa NDOA HAIJENGWI KWA TOFALI, sawa anapaswa kumjenga mumewe kwa kutumia hekima, busara, saburi , uvumilivu, stara na mengi mengine yajayo yanafurahisha.
Amjenge babu kisaikolojia, amwandae kwa kumkanda kanda kando la maandazi (massage) amgeuze geuze kama chapati (ampagawishe kimahaba) amfanyie maaandalizi yote hata yale ambayo babu yupo mgeni machoni kuyatazama
Ndo’ maana nimewauliza waungwana enyi wajuzi wa KUTWANGA NA KUPETA, enyi wajuzi wa SITA KWA SITA, enyi wataalamu wamastyle kama yote kitandani:
“kapungukiwa nini Mariamu?”
“ANAFELI WAPI?”
“MBONA HAJITUMI?”
Bibi ngoja nikwambieni, siku zote kwenye mapenzi babu hupenda kudekezwa chumbani, babu hupenda kubembelezwa chumbani, lishike hilo shoga, lishike hilo neno, usije ukaachwa solemba, usije ukaliwa kasumba, shanga zote zitakupwerepweta, si weye mwanakwetu kutwa kuchwa walilia babu akubembeleze na pia babu akudekeze, shauri yako sie wakina mama wa kitanga tutakuibieni, maana sie wa kitanga kwa kubembeleza mume na kumdekeza, hatujambo👌, hapo ndo petu, patamu hapo, na ujue kwanini hatuachwi wala hatuachiki mapema kama nyie mabibi wenye macho ya kutegemea mume akaufanyie kila kitu nyumbani. Eeenyooo, aibu shoga.👌
Niambienini mwaya, kapungukiwa nini Mariamu hata afanye kumfuatilia pompo roho wangu?
Kapungukiwa nini hata asidumu ndoani? Kutwa kuchwa anamtega wangu wa moyoni Pompo?
Nyoooo, ATABAKI NA LABDA, Labda aende kwa sangoma apewe dawa ya kumteka kimahaba yule aliye wangu wa moyoni, labda aniroge ili nimteme Pompo lakini hapa neva, hawezi, ajue tu kuwa mie ni toto la kitanga N’SHAFUNDWA N’KAFUNDIKA, Mapenzi ninayaweza, riziki nina jirizikia.
Ndo’ hivyo Jamoni nisiwafiche mie Mamsapu Mama la kitanga, nikamvaa Mariamu nikampa VIDONGE VYAKE, akimeza akitema shauri yake, dawa ilimwingia kwa vijembe na kwa kejeli, Leo hii Mariamu akipita mitaani ananiogopa, ananipa heshima yangu tena ananisalimu kwa stara.
LISHAMUUMA Anajua sasa, anajua fika kuwa MUME WA MTU SUMU. Pompo ni wangu na wangu KEISHANIPENDA MWENYEWE. Nasemaje Mariamu akirudia , akijikoroga koroga Haki mie namgea NGEU namjazia watu NYOMI, nd'o ajue fika kuwa mie SIO TYPE YAKE , atoke zake, atoke huko hana haya mwanamke huyu.
Lina muuma hata leo hii lina muuma na kumchoma mfano wa yule KIMBURUKUTU mwenzie SOPHIA. Soph, alijitakia yeye mwenyewe KARIKOROGA na kulinywa kalinywa bila kupenda, Nakwambie shoga jamii kama lote inamwona Sophia kama KIDUDU MTU.
Mashoga na Maanti EMBU NGOJA NIWAAMBIENI, Sophia anaye mume, na mumewe lazima apate raha, lazima mume apewe matunzo yote asilimia mia, lakini ubaya wake Sophia jamoni walimtibua hao mashogaze, wasomtakia heri na fahari, wakamsonga na kumgea ushawishi kumwambia kuwa sasa ni wakati wake, wakati wa yeye kuwa BENETI na mumewe. Wivu shosti wivu ni jipu la kutumbuka na jipu likitumbuka utamwagika usaha mwaya, vundo hilo, vumba hilo, shombo sio shombo! La kubunda limekosa ubani.
Sophia akawasikiliza shogaze wakimwambia ati mumewe ISSA hampendi, hampi mapenzi na nafasi ya kuwa karibu karibu nayeye kwa muda na kwa wakati wa mapenzi, yote kwa sababu Issa ANAJIWEKA BIZE, iwe usiku iwe mchana yupo ‘JOB’ kazini, iwe juma mosi iwe juma pili Issa hapati nafasi ya KUPETIWA PETIWA na Sophia. Ikawa hivyo basi Shoga, Sophia kiguu na njia, anakichakaza kisigino chake hadi huko kwenye Milima na Mapori ya MASANGOMA wajuzi na wataalamu wa miti shamaba.
Wajuzi na wataalamu wa miti shamba hawakumwacha, walimuhudumia kwa kadri ya yeye binafsi alivyotaka, pesa sabuni ya moyo, pesa tamaa ya moyo, pesa tamu na uzuri wa pesa chema lazima kijiuze kibaya kitembeze, Sophia akaikoroga dawa na dawa ikakarogeka, ikawa tepe tepe mfano wa uji uji wa bamia na mrenda. Teeh teeh teeh (Nacheka mie🤣😅) Mpuuzi huyu, alikwisha kusahau kuwa TAARIFA NYINGI ZINAFIRISI.
Loe hii mumewe Sophia yupo yupo HOME LAND haendi kazini wala hataki kwenda kazini hadi pale Sophia ajapomtaka afanye kwenda. Basi shogangu nakwambieni ukitaka kwenda nyumbani kwa Sophia Usishangae nyonyo ukimkuta Issa yule Bosi wa ofisini Leo hii anakosha vyombo anapuguta deki, anafua nguo, anaenda sokoni kununua hiki na kile tena sio kwa mabembelezo bali ni kwa amri za mkewe. Lo! Kwa mtindo huo Issa Keisha kamuliwa kama tambala la deki. Ndio madhara ya hilo dude linalo itwa LIMBWATA.
Issa sio tena yule Issa kidume mchapakazi. Basi leo ukienda nyumbani kwa Sophia Mwaya tegemea kukutana na wanawake wawili wanaoishi nyumba moja. Na hao wanawake si wengine bali ni Issa na Sophia. Jamoni sio aibu hiyo, mmh! Nigune mie, mbona n’shapewa taarifa ati hilo limdawa la limbwata lishamwathiri Issa mumewe Mariamu naambiwa ati hicho kibamia chake Issa hakiendi walah! Hakirudi KIMEDODA, KIMEREGEA na ajabu HAKILIKI. Jamoni mwanamke mbaya Sophia. Teeh teeh teeh, atabaki na labda, kayataka yeye mwenyewe na saa Keisha yapata. Ama! alisahau yale maneno ya WATASHA waliposema “TOO MUCH IS HARMFUL.” Teeh teeh teeh 😄😃😁(nacheka mie) ATABAKI NA LABDA.
:::::::::::::::::::::
Mwaya, nyonyo wangu naomba tuvumiliane next time tukutane hapa hapa, nikupe ubuyu uongeze tarehe za kuliona Jua. Huna baya kipenzi, uishi miaka ya Kobe, ukifa usioze maana hujarogwa my wangu.
Nakupenda.💖💞
No comments:
Post a Comment