SEHEMU YA TATU
Keisha kuyavulia nguo na sasa ayakoge, jamoni taarifa zingine zinafirisi, sio kila biashara yazalisha faida zipo hasara pia, maneno ya shogaze yashamtia DOA, doa ambalo yeye binafsi hajui ataliondoaje Keisha zidisha maji kwenye unga, hicho KIDUDE kilicho ndani ya SEREWILI ya mumewe teeh teeh teeh 😅🤣, HAKINYANYUKI wala HAKISIMAMI, kime SINYAA balaa, yote kwa sababu Sophia kayakoroga ajabu yashamrukia usoni yana muwasha kuliko kawaida, anajuta majuto mjukuu.
Ooh! Jamani, hapo zamani za kale mumewe alikuwaga ni dume la nguvu, DUME LA SHOKA, ajabu leo mumewe hana mbele hana nyuma na baya zaidi hiyo nyumba ya Sophia hawakosekaniki wanawake wawili ambao ni Sophia na mumewe Issa.🧍♀️🧍♀️
Mmh! Bora aibu kuliko fedhea, mwaya mnakumbuka zile zama za mapenzi moto moto ambayo Sophia aliyapata kutoka kwa mumewe Issa, leo hii hata akitaka kuzrudisha kamwe hazitarudi tena, Ijulikane kwamba muda ni wakati na wakati yapaswa utunzwe vema na pia utumiwe vema. Kuishi na mume hakumaanishi ati unatakiwa uachiwe pesa mingi za matumizi bali kuishi na mume ni kwa kutumia hekima, busara na akili nyingi. Ndo’ maana hata Baibo inasema:✝️
“Enyi wanaume muishi kwa kutumia akili pamoja na wake zenu, enyi wanawake muwaheshimu waume zenu.”
Je, Sophia alimuheshimu mumewe? Kama kweli Kama kweli angelimuheshimu mumewe asingelikwenda kwa waganga wa jadi kumchimbia miti shamba ambayo leo hii mumewe amegeuka mwehu, ubaya wa kumlisha mumewe limbwata, leo hii Sophia anatanga tanga na njia KUDANGA, KUDANGARUKA na KUDANGANYIKA kageuzwa KIPORO cha hao majanaume tamaa, hana mbele hana nyuma AMEBAKI NA LABDA
Shoga, wenye hekima tunamwambiaje, afanye Juu chini kuliokoa Jahazi SIO POA atachepuka hadi lini? Wakati anajua fika kuwa MWAJABU yule jirani yake yalomkuta hawezi kuyasimulia MWAJABU alijifanyaga bibi mtukufu na mwaminifu ndoani, wakati huo huo kumbe anamtoroka mumewe anakwenda ‘GESTI RUMU’ kudanga na hao wahuni wenzie wapendao anasa za dunia ya leo ambayo hata hivyo ishageka Kijiji.
Basi babu we! Yalomkuta Mwajabu leo ashindwe kuhadithia. Mumewe alikwisha kuambiwa yote juu ya huyo bibie mdangaji. Akafanya uchunguzi wake, katika kuchunguza chunguza naye akagundua, alah! Kumbe, mkewe sio mwaminifu…………. Ukweli ndio huo sioni haja ya kuirefusha simulizi lenyewe.
Shoga njoo nyumbani Kigamboni nitakupeleka makazi anayoishi Mwajabu, yule mrembo aliyetikisa Jiji kwa kung’ang’aniwa sana na vidume mchepuko ukimwona huwezi kuamini, yaani mwaya sio yeye tena bali ni kicheko na kichekesho😆😅
“BUBU,” Nisimwite Bubu jamani, Keisha laaniwa mdomo wake.
“KIZIWI,” Mwaya, Mwajabu hasikii tena, kawa kiziwi ngoma masikio
“KIPOFU,” Huruma shoga, mdangaji kawa kipofu kwa kumwagiwa TINDIKARI na Tindikari yenyewe alimwagiwa usoni, ile amefumaniwa kule Gesti rumu
“KIWETE,” Oh! Jamani, 😭Mwajabu hana hana miguu tena. Nakwambie shoga kakatwa katwa ‘Mapangashwaaa’ yaani hana hips hana paja kabakia mifupa kama miguu ya kuku. Oneni sasa mashoga zangu hayo ndio malipo ya usaliti.
Na alie tu! Asijue kuwa aliyemtendea yote hayo ni mumewe bwana Abdul, mpole machoni, huruma mikononi lakini kumbe ABDUL ni pili pili moyoni. Haki! Tusolijua litatusumbua.
Shoga, waweza kuyateka MAWAZO ya mtu mdomoni lakini usijiaminishe ati, waweza kuuteka MOYO wake mazimaa. Teeh teeh teeh (nacheka mie), UTABAKI NA LABDA
Nilimwambia tena Sophia nilimwambia pale alipokosea aparekebishe la sivyo yatazuka yakuzuka, muda ni wakati na wakati ndio sasa, yakizuka yale ya kuzuka jamoni! Sijui kama atapona mtu hapo, sijui kama atabaki mtu hapo, vumbi si vumbi, upepo si upepo, ndugu Wataliamsha DUDE, itakuwaje jamani? Bora nusu shari kuliko shari kamili. Basi mie Mamsapu, mama wa kitanga nikampa Sophia VIDONGE VYAKE, akimeza akitema shauri yake. Japokuwa mie na Sophia HATUIVI CHUNGU KIMOJA lakini Shosti, Baibo inasema “ Adui yako mpende kama unavyojipenda wewe mwenyewe.” Duniani kuonyana sio kwa maneno matupu bali pia maonyo yaendane na mifano kuntu iliyo hai.
“Sophia mwaya nisikilize.” Nikamuweka Sophia kati nimmalize kwa mifano iliyo hai na madhubuti.
“Yote hayo uliyotenda ni MAPITO mwanamke, unapaswa kujielewa, wewe ni nani? Unakazi gani ya kufanya au hauna kazi gani muhimu ya kufanya? ISSA ni mumeo, ulimpenda sana zamani lakini kwa sasa USHAYAGEUZA, USHAYAHARIBU USHAYAKOROGA. Mmh! Sijui USHABAKI NA LABADA?”
“LABDA! LABDA! LABDA!LABDA! Teeh teeh teeh, labda ufanye nini ili kumrudisha mumewe, kwenye ‘Position’ yake, kwenye ile hali yake aliyokuwa nayo hapo awali, kwenye wajibu na jukumu lake kitandani. POLE dada, pole sana, yalokukuta ndo’ hayo, mawazo mengi hasara.”
My wangu sio poa niruhusu nikomee hapa kwa Leo
Kesho mapema tu LABDA nikipata bando nitakutafuteni
Tulinywe libeneke.
No comments:
Post a Comment