Friday, April 25, 2025

OMBI LA KIJINGA.

 

OMBI 🤲 LA KIJINGA.

 


 

 

 

 

SEHEMU YA KWANZA

WANAKUTANA.

           Bwana Masumbuko pamoja na bibi Mwema waliishi ndani ya jiji la Dar es saalam,🌃 Mbezi beach kwenye makazi yao, wana mjengo wa fahari bonge la jumba 🏘️na uzuri wa kujenga nyumba yao katika mazingira yale kuna utulivu mwingi pia kuna hali nzuri ya hewa. Wawili hawa hawakuwa ni watu wa daraja  la chini bali wawili hawa ni watu wa daraja la kati (middle class) yaani watu ambao wanajiweza kiasi fulani hawana shida sana💰💸, kama ni chakula basi chakula 🥪🍕kipo tele nyumbani kwao, kama ni manywaji 🍻🍷🥂basi manywaji yapo tele nyumbani  kwao, kama ni pesa hawana shida wanazo pesa nyingi na za kutosha.

               Mungu akuwatupa bali mungu aliwajaria kuwa na mtoto mzuri wa kiume 👼waliyekuja kumpa jina la Furaha, wakiwa na wingi wa furaha ya kumpata mtoto mwenye siha na afya tele. Kwa ujumla mtoto Furaha alizidi kukua na kuwapendeza wazazi  wake, kwa vile mtoto Furaha alilelewa katika maadili mema, alisoma   📚vema  kwa bahati nzuri Furaha aliweza kuhitimu elimu ya chuo kikuu, kwisha kumaliza masomo yake ya chuo kikuu, furaha alipata kazi nzuri ya Ukurugenzi, akaketi Afisini, 📝akijizungurusha zungurusha juu ya kiti chake💺, kwa wingi wa furaha, raha na mapozi, hana shida tena, yeye ni mtu wa kuandika🖋️✍️ andika Afisini, yeye ni mtu wa kutia tia saini mikataba mbali mbali, akiwalipa watumishi wa kampuni aliyoajiriwa na kufanya kazi nyinginezo nyingi na muhimu kwake.


                Furaha hana shida tena, mshahara wake ni mkubwa wa kumtosha kununua Gari🚘 au kujenga nyumba na uzuri waa maarifa ya Furaha tayari amekwisha jenga nyumba na kununua gari zuri la fahari anapesa mingi ana raha tele, ametunzwa kimaadili ndio maana ana juhudi kazini kwake ana bidii pia.


                  Basi siku moja yapata juma tatu asubuhi Furaha alitembelewa na mgeni ambaye alikua ni binti👩 mmoja mzuri sana, anavutia kama Malaika ni mwema machoni na pia mzuri moyoni. Wakati yule binti anaingia ndani ya Afisi ya Furaha Furaha alijiweka bize akiandika andika mambo yake ya kiafisi. Akamkodolea macho yule binti mzuri kama uaridi, 🌹mkononi kwake alikua ameshikirilia bahasha ambayo kwa fikra za haraka ungelisema ni barua ameileta maalumu ajiri ya Bosi.


                 “Karibu sana Dadangu, ingia usiogope keti kunako hicho kiti” 🪑Furaha aliongea akimwelekeza mgeni aketi kunako moja ya viti vya pale Afisini.


                “Asante sana Bwana mkubwa. Habari za kazi, pole na majukumu.” yule binti mrembo aliongea maneno mazuri ya kutia moyo na faraja.


                “Kazi ziko poa, namshukuru sana Mungu pamoja na faraja zako.” Furaha alimjibu yule mgeni.


                 “Kwa jina ninaitwa Happness Magessa, mimi ni mzaliwa wa Musoma, hapa Dar es saalam ninaishi Kinondoni, kwa mara yangu ya kwanza nimejitokeza kuja kuomba nafs ya kazi kwenye kampuni yako.” Happness aliongea kwa ufasaha zaidi.


                   “Oooh! Karibu sana, mimi ninaitwa Bwana Furaha, nimefurahi sana kukufahamu Happness Magessa.” Furaha Aliongea


                  “Jambo jema ninalofurahia ni kwamba maana za majina yetu zinafanana, mimi ndiye Mkurugenzi mkuu wa kampuni hii.”


                 “Nimefurahi pia kukufahamu,” Happness Magessa aliongea naye akaendelea kunena.


                 “Bahasha hii ina CV zangu.” Akamkabidhi Furaha ile bahasha yenye Barua ya kuomba maombi ya kazi.


                  “Ok. Ok no problem, naomba uniache niipitie pitie, uje kesho kuchukua majibu ya maombi yako, uje muda wa saa tano nitakuwa tayari nimepata jibu sahihi.” Furaha aliongea maneno mazuri yenye kumpa yule binti matumaini.


                   “Asante🙏 ninashukuru, kazi njema.” Happness aliinuka pale alipoketi, apate kuondoka.


                    “Uwe na siku njema, 👋have a nice day.” Furaha alimuaga mgeni wake.


                    “Nawe pia, have a nice day too.”👋 Happness alirejesha majibu. Akatoka ndani ya ile Afisi akaelekea ilipo lift iliyomteremsha hadi Horofa ya chini .


Mara baada ya Happness kutoka ndani ya ile Afisi, Furaha akaifungua Bahasha aliyokabidhiwa na Happness, akaifungua kwa pupa pupa, alimradi apate jua nini kimeandikwa ndani.


                    “Waaoooooo!” ☺️Furaha alijikuta akiongea kwa furaha kuu, akiyashangaa shanga yale makaratasi yaliyokuwa ndani ya ile bahasha iliyoletwa kwa mikono ya Hapness mtimani akajisemea. “Duh! Kumbe huyu binti mrembo amesoma Oxford university? Mashallah! Vyeti na wadhifa uliopo humu unafaa kwa mtu huyu kufanya kazi hapa.” Furaha amejaa tabasamu, aliendelea kuongea.

                  “Lazima nimpe nafsi ya kazi ndani ya kampuni hii.” Furaha alihitimisha kwa furaha.

                                      ##########################

Yapata saa nne na robo asubuhi, Happness alikuwa tayari yupo Afisni, amewahi mapema ili asikilize majibu juu ya nafsi ya kazi aliyoitafuta, alimkuta secretary  wa ile Afisi ametulia tuli anakunywa chai ya maziwa na chapati, hana shida Binti yule analipwa vizuri ndio maana anazidi kunawili na kupendeza.

                  “Samahani ndugu Secretary  je nimemkuta Mkurugenzi?” Happness alimuuliza huyu binti ambaye hapo baadaye alikuja kugudua kuwa anaitwa Amina.

                   “Yeah! Umemkuta, utasubiri kidogo sababu ana maongezi na mgeni wake.”

                   “Ooooh! Sawa sawa  sio vibaya nitamsubiria.” Happness aliongea kwa matumaini.

                    “Waweza keti katika kiti hicho dada.” Amina alimweleza Happness mahali pa kuketi, Happness aliketi pale alipo elekezwa.

                     “Eliza!” Amina alimwita kwa sauti mmoja wa watumishi wa pale Afisini.

                      “Abee.” Eliza aliitikia na kuja pale alipoketi Amina.

                      “Embu mletee Dada supu aendelee kunywa wakati anamsubiria Mkurugenzi.” Amina alimtuma Eliza alete supu Happness apate kunywa. Happness aliona aibu kuikataa ile ofa alijikuta anakunywa kwa moyo mmoja. Akainywa ile supu iliyoletwa na Eliza na baada ya dakika kama 45 kupita alimwona mtu akitoka ndani ya Afisi ya bwana Furaha.


                      “Dada sasa unaweza kuingia, mgeni tayari amekwisha kuondoka.” Amina alimpatia ruhusa Happness apate kuingia Afisini kwa Bosi Furaha.


                       “Oooh! Thanks so much.” Happness alishukuru akainuka pale alipoketi akaingia Afisini kwa Boss Furaha. Happness alikuwa amependeza sana, ananukia marashi na manukato, wakati huo tayari Happness alikwisha kuinywa ile supu tamu iliyoandaliwa kwa wingi wa chapati.


                      “Oooh! Verly good, ni wewe Happness karibu sana, karibu uketi.” Aliongea Mkurugenzi mkuu, aliongea kwa bashasha hali ambayo ilimshangaza sana Happness ambaye hakutarajia kama angelipokelewa kwa wingi wa furaha ile.


                 “Asante sana bwana Furaha,” Happness aliketi kwenye kiti chake, wakatizamana uso kwa uso yeye na Bosi Furaha. Wakati huo Bwana Furaha alionekana kuwa ni mwingi wa tabasamu.


                   “Habari za toka jana?”🤝 Furaha alimsabahi Happy.


                   “ Nzuri,👍 ninamshukuru Mungu, je wewe una endeleaje Bosi?”


                   “Nami ninamshukuru Mungu.”


                  “Uliniambia nije leo baada ya jana kukuachia Bahasha ile yenye barua yangu ya kuomba kazi!”


                  “Ndio ninakumbuka vema, nimeisoma Barua yako na pia nimetizama wasifu wako, nimeona kumbe unafaa kufanya kazi pamoja nami.” Furaha aliongea maneno mazuri kwa Happness.


                  “Ooooh!” ☺️Happness alipumua kwa furaha.


                  “Asante sana Jehova.” Alimshukuru mungu kwa mazuri aliyomtendea. Basi kuanzia siku ile Happness alifanikiwa kufanya kazi katika kampuni ambayo Furaha alikuwa Mkurugenzi mkuu. Happy na Furaha walifanya kazi kwa pamoja kwa muda wa miezi saba, ndani ya muda huo walipata faida kubwa sana ukilinganisha na muda uliopita kabla Happy hajaajiriwa.




,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,




Furaha alipendezwa na uchapakazi aliouonesha Happy, Furaha alipenda Happy aje kuwa mke wake siku moja, mke wa ndoa, ukitegemea Furaha alikuwa angali bado hajaoa na pia Happy alikua hajaolewa. Furaha akamueleza Happy Hisia zake, hisia za mapenzi, pasina kuficha neno kumbe Happy naye alikuwa akimpenda Furaha, labda tuseme aliogopa kumwambia kwa hofu ya kuona kibarua chake kikiota nyasi. Wawili hawa wakapendana na kupatana kwenda kwa wazazi kujitambulisha


                   Uzuri wa kujitambulisha kwa wazazi wao waliwapokea kwa shangwe nderemo, vifijo na chereko, halikuwepo pingamizi juu ya hawa wawili waliopendana, kwa Baraka za wazazi wao walikubaliwa.


 Kama alivyofurahi Furaha ndivyo Happness alivyofurahi pia, awali alikuwa na hofu, hofu waliyo nayo wanawake wengi, wanaopelekwa nyumbani kwa wakwe zao, alitia hofu yawezekana wazazi wa mchumba wake wakamkataa mwanamke huyo, kwa madai kwamba wamemtafutia Furaha mchumba wa kumuoa. Mungu yu mwema kwa Happnes haikuwahivyo.


 Hatua iliyofuata ilikua ni kufunga ndoa, karamu kubwa ilifanyika, ilikua ni bonge la karamu, karamu ya kifalme. Baada ya kumaliza fungate maisha ya ndoa yalianzia hapo. Wakaishi kwa kujitegemea, uzuri wa maisha yao wawili hawa walikwisha kujijenga kiuchumi, wangali wana mali nyingi pamoja na vitenga uchumi kibao. Kwa kifupi hawakuwa na shida.

 Itaendelea sehemu ya pili. 


No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...