Wednesday, April 9, 2025

INFIDELITY





 MUME WANGU ALIMTIMUA🏃 NYUMBANI🏠 MAMA YANGU MZAZI MWENYE CHANGAMOTO YA AKILI🤪 MARA BAADA YA MAMA KUMFUMANIA AKIGONOKA NA CHANGUDOA. 💏


      Baada ya sherehe ya Noel na Mwaka mpya kufika ukingoni wanangu wawili Rashford na Josea 👩‍👧‍👦walihitaji kurudi shule,🏫🎒👨‍🏫 shule ya boarding, 🛌shule Binafsi ya kulipia.💰llikua ni kawaida ya my Husband kuwapeleka skuli 🚖Kila ifikapo January mosi. Mie nilibaki na mama yangu mwenye changamoto ya akili🧠 yaani kuna wakati akili zake ukimbia anakua kama sio yeye naye atafanya Kila kituko cha kuudhi 🤯au kuchukiza, utoto mwingi hadi tutamchoka. Atavua nguo zake, atapiga kelele, atavunjavunja vyombo na kuharibu pia baada ya muda akili zake zingerudi na kuwa sawa, hapo angelitulia tuli kama maji mtungini.🚰🏺.


    Uzuri wa changamoto ya kupoteza ufahamu🤯 pale inapofika ukomo mama yangu urejea katika hali yake ya kawaida. Hali ya kujutia matendo yake ya utoto, 🥹hali ya kujionya kutorudia tena matendo haribifu,😮‍💨 hali ya utulivu, amani na furaha🫡. Ajabu changamoto yake ingelirejea tena.😵‍💫


       Basi mume wangu Dionice aliniambia kwa mwaka huu 2024 January niwapeleke watoto warejee kusoma nje ya Mkoa yaani Tanga mjini sikupinga Wala kukataa nilimuomba anitunzie mama yangu mwenye changamoto ya ufahamu, kwa moyo❣️ mkunjufu Dionice alikubali Ombi langu. Safari yangu mie Gigyfriday na wanangu Rashford na Josea ilipamba moto.


"""""""""""""""""""""""


"Hallow! Gigy"☎️ Siku ya tatu baada ya kuingia Tanga mjini mume wangu alinipigia simu.


"Hallow! Daring😘"Nilimwitikia wakati huo nipo ndani ya Moja ya hoteli 🏨🏩za kifahari.


"Kuna tatizo kubwa limetokea nyumbani" 🏡Toba!😶 Dionice alinishitua kidogo.  


"Tatizo!?"🤭 Niliuliza kwa mshangao kidogo Wine yangu niliyokua nikiinywa imwagike.


     "Ndio tatizo my wife, ni tatizo kubwa" Aliongea


     "Tatizo gani? Tafadhali nieleze." Nilikaa mkao wa kula kuisikiliza ile changamoto.


     "Bibi mama mkewe ametoweka nyumbani nisijue ni wapi alipoelekea. Safari hii ile grass 🍷🍾ilinidondoka chini puuuu ikadondoka na kuvunjika. Maana nilipata mshituko.


     "Ametoweka! 🏃‍♀️Ametowekea wapi na lini ametoweka?" Maswali mfululizo yalinitoka, hofu na wasiwasi juu ya Mamangu mwenye changamoto ilinivamia.


      "Ametoweka leo🏃‍♀️,sijui ni wapi alipotowekea!? Ningali ninamtafuta." Dionice alinijibu.


     "Vipi ushaenda Police👮‍♂️🚓 kutoa taarifa?" Nilimuuliza, jibu alilonipa lilinivunja maini.


    "Bado nakusubiri wewe uje tuangaike pamoja kumtafuta." Sikutaka kuendelea kuongea kwenye simu,📱nikakurupuka kuondoka ndani ya ile Hoteli 🛋️nikiwa nimeacha Kila kitu changu chenye thamani💰 na kisicho na thamani. Nikashuka ngazi za ile Horofa haraka haraka nikakimbilia uwanja wa Ndege🛫 ilikuwai Ndege ✈️itakayoondoka siku ya Leo kwenda Dar es saalam🌇.


      Niliingia Tanga nikiwa na Gari yetu lakini baada ya kusikia habari juu ya tatizo lililompata Mama ilibidi niiache Gari yetu pale pale Airport, nikapanda Ndege iliyokua inaelekea Dar es saalam. Moyoni nikijilaumu kwanini niliruhusu Dionice amtunze Mama yangu mwenye changamoto? Ni heri na ni bora kama ningelibaki kumtunza mimi mwenyewe.


   "Labda alimuachia ufunguo wa Geti kuu?⛩️" Nilijiuliza, nikiwa nimepagawa yote kwa sababu nilimpenda sana mama yangu na kuumia moyo ilikua lazima.


    "Mama umekwenda wapi rudi tafadhali." Nilisali kimoyomoyo 🛐📿


    "Ninakupenda Mama yangu, ninakupenda Dear." Nililia pekee yangu ndani ya ile Ndege. Safari yangu haikua ndefu sababu kutoka Tanga kwenda Dar ni masaa ⏰machache baada ya kuingia Dar nikafanya pupa pupa kukodi Uber🚖 ilonikimbiza moja kwa moja hadi nyumbani kwangu nilikomkuta mume wangu amekula pozi sebuleni macho kodo kwenye Tv📺 anafuatilia Tamthilia ya Juakali.🌞


     "Daring badala ya kuangaika mitaani kumtafuta Mama yangu wewe umepiga pozi namba nne kwenye Video📺 unatizama Tamthilia" Nililalamika mara baada ya kuingia pale sebuleni.

      

     "Gigyfriday, unastahiri kupumzika kwanza ndipo nikupe taarifa kamili." Alinipokea Kisha akanitaka nipumzike sofani🛋️ akafanya hima kuniletea maji baridi Jokofuni 🧊lakini wapi! Hayakupita kooni. 


     "Muda huu unaoingia ndo' na mimi ni naingia, mwenzio nimekesha🌗 nikimtafuta Bibi Mama mkwe nisimpate." Aliongea. 


     "Ushaenda 🏃Polisi?👮, Polisi nao wanasemaje?" Maswali yalinitoka. 

    

     "Nimeenda, nao wameahidi kutusaidia watampata tu." Alinipooza. 


    "Tatizo nini hadi Mama akimbie nyumbani?" Nilihoji. 


    "Gigyfriday si unajua changamoto inayomsumbua Bibi Mama mkwe?" 


    "Duh! Mola wangu amwepushie mabaya Mama yangu" Niliropokwa. 


    "Amka basi twende tukaendelee kumtafuta." Ninavyompenda Mama yangu nilikua tayari kufanya jambo lolote ilimradi apatikane.


       "Gigy my Daring Nimechoka please." Alidekadeka. 


     "We! Mwanaume wa wapi? Embu Amka hapo tukaangaike." Nilimpigia kelele haraka haraka. Ttulichangamka kumtafuta. Tulimtafuta sana Mama yangu, tulimtafuta ndani ya majalala ya takataka🗑️🚮 tukidhani labda amekwenda huko, tulizunguka mtaa kwa mtaa tukiuliza na kuwapigia simu ndugu, jamaa, marafiki 👥na majirani lakini wapi! Ma. Hakupatikana. Hatukukata tamaa tuliendelea kumtafuta Mama.


       ::::::::::::::::::::::::


Siku ya tatu tulijisikia kuchoka sana maana tulikua tunapumzika na kulala popote pale ili tubahatike kumpata Mama. Tuliamua kuelekea nyumbani kwenda kukoga na kubadili nguo maana kwa zaidi ya siku tatu hizi hatukubadili nguo Wala kugusa maji mwilini.


    "Kwanini tusiende kulitangaza🔊🔉 jambo letu kwenye Mablogu.📃 Televisheni 📺na Radion!📻📡"Nilitoa ushauri.


     "Wazo zuri" alinijibu kwa ufupi.


    "Tutangaze donge nono💰 kwa mtu au watu watakao mpata Mama." Nilitoa wazo.


     "Unamaanisha pesa, 💶💸 , kiasi Gani? "Dionice aliniuliza.


    "Nipo tayari kutoa Million Tano 💳💸kwa mtu atakayebahatika kumpata Mama yangu."Nilimjibu Dionice.


    "Gigy pesa zote hizo? Pesa za kufanyia jambo la maana." Alinijibu kama vile hakupendezwa na wazo langu.


     "Najua Dion, lakini pia Mama yangu ni mtu wa maana." Nilimziba mdomo.🤫 Tukasikia muungurumo wa gari ikiingia uwanjani kwetu, ilikua ni Gari ya Polisi. Sie tulikodoa macho kodo kwenye Dirisha ili kujua kuna Nini? Nikaingiwa na furaha baada ya kumuona Mama yangu akiteremshwa kutoka kwenye ile Gari ya Polisi. Polisi walifanya kazi nzito ya kumsaka hadi kumpata Mama yangu.


     "Twende tukampokee." Nilimwambia Dionice kwa furaha.


    "We, nenda tu ukampokee!" Mume wangu hakuonesha furaha. Nikatoka kwenda kumlaki Mama yangu kwa furaha na kumkuta akiwa mzima mwenye afya, pasina makovu au ubaya mwilini mwake. Nikampokea na kumkaribisha tena Nyumbani kwetu. Aliingia sebuleni na mimi pia niliingia, Mabwana Polisi nao waliingia. Ile tunaingia tu, Mama aliponwona mume wangu alianza kupiga kelele kama amemwona Pepo mchafu.🦹‍♀️👿


      "Mkamateni huyu fedhuli ☠️na firauni mjaa laana." Alimnyoshea dole mume wangu, aliyeanza kuogopa.


      "Kwani amefanya nini Mama!?" Nilimuuliza kwa mshangao⁉️


     "Huyu fedhuli ndio sababu ya mimi kuondoka hapa nyumbani." Nilimsikiliza, Askari walimsikiliza pia.


    "Tatizo nini!? Embu tueleze."Askari mmoja alimtaka mama yangu afungue kinywa ayatoe yaliyofichama moyoni. Mama akaanza kueleza.


     "Gigyfriday huyu mumeo ni shetani👹 asiye na huruma."Alimnyoshea mkono👉 mume wangu aliyeketi sofani kimya akisikiliza.


      "Ulipoondoka kwenda Tanga kuwapeleka wajukuu zangu Shule usiku mmoja nilikua nimelala chumbani kwangu lakini nikaja kuamshwa na milio ya chaga za kitanda 🛏️chumbani kwenu. Mbali na sauti za chaga niliskia mili ya sauti za mahaba, mwanzo nilivumilia moyoni nilijisemea sauti hizi na vilio hivi vikuu vya mahaba sijazoea kuvisikia ndani ya nyumba hii." Mama aliongea wote tulimsikiliza.


     "Nikajiwa na wazo kwamba labda Binti yangu Gigyfriday amerejea kutoka Safarini, lakini kwanini arejee pasina kuniambia sembuse kuja chumbani kwangu kunitakia hali? Basi mie nikateremka ngazi za Horofa na kuelekea chini kule sauti za chaga na mahaba zikiendelea kulindima. Bahati nzuri au mbaya mlango wa chumba chenu ulikua umeachwa wazi." Mama alipumzika kidogo kuongea🙇


   "Nikausukuma ule mlango, taa zilikua zinawaka💡. Salale! Macho yangu yalitua kitandani nikamuona Mkwe wangu Dionice akifanya zinaa na mwanamke mwingine."Mama alitoboa Siri.


     "Bibi Mama mkewe ni mwongo👺" Dionice alimpinga Mama yangu.


      "Kama mimi ni mwongo yule mwanamke ni nani haswa pale kitandani unapopaswa kulala na mkeo Gigy?" Mama alimuuliza Dionice.


     "Mwanamke aliyelala kitandani alikua ni Ombaomba niliyemuokota mitaani nikampa maji, 💦chakula🥪 na pahali pa kulala🛌 kama hifadhi. Dionice alijitetea sie twalimsikiliza.


    "Na ile sketi kimini👗, kitopu,👙 wigi🦰 la bei gharama, mkoba mwekundu👜, viatu virefu vya mchuchumio 👠 baya zaidi amepakaza mdomo wake lips nyekundu💋💄 wote mlikuwa mmelewa bwiiiii 🍻🍺msitamanike." Maneno yaliyomtoka Mama yalitushangaza 😂😶‍🌫️


    "Dionice ni kweli ayaongeayo Mama!?"Nilimuuliza. 


    "La! Hasha, Bibi Mama mkewe anadanganya. Lakini Gigy si unajua kwamba Mama ana changamoto ya kuvurugwa akili? Yamkini akili zake zilihama ndio maana anaongea wendawazimu." Dionice aliongea mikono yake na miguu ikipata kitetemeshi.


     "Mume wangu lakini si ni wewe ndiye unayedai kuwa ulimleta Ombaomba ndani ya chumba chetu Sasa yawezekana vipi Ombaomba akalala chumbani kwetu wakati vyumba vya wageni vimejaa tele na baya zaidi wote wawili mlilewa?" 🍺🥂Nilimuuliza kwa hasira.👿


       "Alafu tangu Mama ametoweka mbona hukuniambia kama ulimleta Ombaomba chumbani kwetu?" Nilimuuliza.❓


    "Kumbe mimi ninawapeleka watoto shule wewe unafanya ngono na Malaya unaowaita Ombaomba? Hakunijibu zaidi ya kuangalia chini kwa aibu. Mama yangu akaendelea kunena:


    "Nilipomuuliza mkwe wangu kwanini unafanya ngono na Malaya chumba ulalacho na Binti yangu mkwe akanijibu jeuri na kuniambia 'hii ni nyumba yake, ana haki ya kufanya kitu chochote kile.' " Toba! Nilishituka yaani nyumba niijenge mie alafu mwanaume amjibu kunya 💩 Mama yangu.


      "Mkwe wangu akaniambia niondoke haraka ndani ya hii nyumba sababu hii nyumba ni yake, mimi na mwanangu Gigy hatuna chetu hapa." Mama alianza kulia.🥹 Mimi pia chozi lilinitoka 


     "Hii ni nyumba yako 🏡Dion? Ulijenga wewe?" Nilimuuliza, hakunijibu.


      "llibidi niondoke Gigyfriday, niliondoka akinitazama wakati huohuo amemkumbatia Malaya." Mama aliongea kwa uchungu.


     "Nisamehe Gigy, nisamehe Daring....💞 Pombe zilinidanganya " Aliongea.


     "Siwezi kukusamehe, umemvunjia heshima Mama yangu." Nilianza kulia chozi.😭😢


      "Mama kwa sababu sisi hatulioni kosa alilolitenda huyu Bwana Dionice pia hili jambo ni la kifamilia tungependa tuwaachie hii kesi muimalize nyie wenyewe." Bwana Askari aliongea Kisha wakaondoka na kutuacha sie twalumbana na kupigiana kelele ndani ya nyumba.


     "Beba Kila kilicho chako 🧳na uondoke ndani ya Nyumba yangu, muuaji mkubwa wewe."Nilimpigia kelele.


    "Nisamehe Gigyfriday, nisame sweetie. Ibilisi😈👹 alinipitia." Alijitetea


     "Na wewe kampitie huyo lbilisi. Mkeo sikutoshi hadi ufikie hatua ya kutembea na Malaya!? Eeh!? Baya zaidi unalala nae kitanda ninacholala na wewe." Nilimfokea.


       "Nisamehe Daringi 🙇‍♂️please." Sikujali Wala sikumsikiliza.


       "Nasema beba vigagula vyako uondoke. Nilitilia mkazo, akaingia chumbani na kusomba vilago vyake safari ya kuondoka ilifuata.


     "Barua ya Taraka utaipata kwa Mwanasheria ⚖️ infidelity mkubwa wewe." Nilimkemea kwa hasira😡😤


    "I'm Sorry Gigy lm sorry please."Alibembeleza sana


     "I don't care please leave my house now." Nilifoka, Aliondoka akiwa mnyonge na mwenye huzuni



***************

(Embu nishaurini wenyewe, nimsamehe au nimbwage kwa Mwanasheria !? Ningali katika machozi na kuvurugwa 🥲) 


***************


TCHAO 😢🥹😭🤯


""""""""""""""""'""'''''''''''




     


    




   

      

No comments:

Post a Comment

I promise you

   I PROMISE YOU. (NINAKUAHIDI.) SURA  YA KWANZA. UBAYA WA POMBE. “Umenizingua job, umenizingua kwa muda mrefu sana mpenzi wangu…….kwanini l...