NILIUHARIBU UHUSIANO💕💔 WA MUME WANGU NA
GIRLFRIEND 👩❤️💋👨 WAKE BAADA YA VIFO ⚰️☠️ VYAO
NILlSHANGAA NALETEWA MTOTO WAO 👧 NIMLEE.
Ninakumbuka ilikua ni mwaka 2010 nilienda 🚶 kutembelea kaburi la Mume wangu Dylan aliyenitoka baada ya kupata ajari ya Gari na kuaga Dunia. Siku hiyo nilikwenda kuweka shada la Maua juu ya kaburi lake. Machozi mengi yalinibubujika.😢 nikiwa katikati ya maombi kumuombea🛐🤲 Dylan Mume wangu nilihisi kuguswa bega la mashoto, ubaridi ulipenya mwilini mwangu nikatetema.
Nilipogeuka nikakutana na uso wa mwanamke mzee mwenye kadirio la miaka themanini akiwa👵 amemkumbatia mtoto ambaye kama sikosei alikua na umri wa mwaka mmoja.👩🍼
"Tafadhali mchukue huyu Binti ni Binti aliyemuacha Mume wako." Pasina salamu aliongea yule Bibi kizee. Nilimtazama Kwa sekunde chache nami ⏲️nikahisi yawezekana ni Mwendawazimu."
"Bibi chunga kauli yako, Mume wangu tangu amefariki imepita miezi sita sasa hatukuwa na mtoto Wala hatukujaliwa mtoto." Nilimjibu
"Huyu ni mwanaye na Mimi ni Bibi kizee unataka nimpeleke wapi kama sio kwako wewe kumchukua." Aliongea.
"Usiniharibie siku wewe Bibi kizee nimekwambia mimi na Mume wangu hatukuwa na mtoto, huyo mtoto mpeleke pahali popote pale hata kama ni kituo Cha kulelea watoto yatima." Nilimwambia Kwa hasira. Nikatoka pale Makaburini kuelekea pahali nilipoifadhi gari yangu Ili niondoke. Nilipofika kwenye Prado yangu nyeusi🚐 nikaifungua mlango upande wa Dereva. Nilipoufungua tu mlango jamani nilipigwa butwaa baada ya kumkuta mtoto yule yule ambaye Bibi kizee nisiye mfahamu alimbeba.
"Toba!🙄🧐 amemuingizaje mtoto ndani ya Gari ikiwa Gari yangu ilifungwa." Nilijiuliza.
"Huyu Bibi kizee vipi au ni mchawi? Ananifosi nimchukue mtoto ambaye simjui" Nilitizama kila pembe ya Gari yangu kuangalia kama yule Bibi yupo lakini sikumuona nikambeba yule mtoto na kurejea naye pale nilipokutana na yule Mbibi yani kule Makaburini lakini ajabu sikumkuta.🪦
"Mume wangu hakuwa mchepukaji, Mume wangu alikua ni mwanaume mtulivu na mwaminifu asingeliweza kuzaa nje ya ndoa.🤔" Niliwaza. Nikarejea ndani ya Gari yangu tayari kuiwasha moto na kuondoka. Nilimtazama yule Malaika 🧚 kusema kweli alikua ni mzuri wa kuvutia machoni. Moyoni Nikajisemea:
'Ama niende Hospital🏥 nikachukua vipimo vya DNA'
'Mmh! Dylan Mume wangu hakuwa mchepukaji, alikaa akatulia na Mimi tu👩❤️👨.'
'Wacha niende Hospital nikachukua vipimo vya DNA🧬' Nikaikimbiza Gari kuelekea Hospital, bahati nzuri nilipitia supermarket🛒 kumnunulia yule mtoto vichache vya kula, kunywa🍼🧋 na kutafuna Ili asije kunisumbua mbeleni.
'''''''''''''''''''''''''''''' '''''''''''''''''''''''''''''
"Nahitaji kumifanyia Partenity Test huyu mtoto ili nijue kama kweli ni mtoto wa marehemu Mume wangu.'' Niliongea na Dakta🥼🩺.
"Madame Doka ombi lako sio mzigo kwetu tutalifanyia kazi ila itakubidi usubirie siku mbili au tatu tutakupatia jawabu tosha."Dakta lsmael aliongea.
"Dakta nipo tayari kutoa pesa nyingi💷💰 ilimradi
ili jambo lifanyike haraka na majibu nipatiwe Leo🔬 Leo."Nilimwambia Dakta lsmael.
"Safi sana Madame kama utatoa pesa nyingi basi Leo Leo utapewa matokeo.📄" Yule Dakta mpenda pesa alikenua meno ya😁 furaha kisha akachukua Sampuli muhimu ajiri ya kumpima yule Binti nisiyemjua jinale zaidi ya kumwita Alicia.
Ikawa kusubiri matokeo forever, mtoto alipolia nilimbembeleza Kwa kumpatia maziwa, alipojisaidia haja kubwa na ndogo nilimbadilisha Pampasi, alipotaka kulala nilimbembeleza naye akalala, 🤱kazi ya malezi na kulea mwana yataka moyo. Hakuna marefu yasiyo na mwisho nikaitwa Ofisini kwa Dakta lsmael nikakabidhiwa Report na matokeo ya DNA 🧬 yalisomeka asilimia99.9 💯Mtoto Alicia ni wa Dylan Mume wangu yaani ni Copyraity
Wiki mbili kupita nikiwa na mtoto Alicia naangaika kufanya Kila kitu kuhusu kumlea na kumpatia mahitaji yake yote nilibuka na wazo zuri nilihitaji kufahamu Mama wa Alicia ili nimkabidhi mwanaye aanze kumlea na iwapo Mama yake Alicia hana uwezo kiuchumi nitajitoa kumuwezesha ili afanikiwe kupata kazi au biashara.
Mie Dorcka na Dylan hatukubahatika kupata mtoto, tumeishi wote miaka 42 ndani sio mbaya Alicia amerudisha heshima ya mume wangu Dylani basi Wacha nimsake Mama yake Alicia.
'Duh! Nitaanzia wapi? Mwanamke simjui sijui nitaanzia wapi kujua pahali anapoishi?' Nilijiuliza.
'Yule Bibi aliyenikabidhi Alicia pia sijui wapi anapoishi? Jamani mtihani huu!!' Niliwaza.
'Ok, ok 👍 yanipasa nianze kusechi sechi mtandaoni, Ofisini na nyumbani yamkini nitapata kitu.' Basi mie huyo nikaingia mitandaoni: Fb, Wasap ya mume wangu, Twitter, Reddit, YouTube, na kila mtandao alioutumia marehemu mume wangu nikisoma Kila jumbe na kuangalia kila picha lakini sikuona Darili za Dylan kunena au kupiga picha akiwa pamoja na mwanamke
Nikafanya hima kupangua pangua nguo zake kabati lote lakini wapi! Nikaingia Ofisini kwake na kuivuruga vuruga Kila kilicho Ofisini lakini wapi! Sikupata kitu. Taratibu nilianza kukata tamaa. Ghafla ninakumbuka ndani ya Gari yake alifunga kamera iliyomuongoza kujua wapi anakwendra, wapi yupo au anaongea na nani ndani ya Gari.
Nikafurahia na kufanya hima kuichunguza ile kamera iliyopachikwa ndani ya Gari. Nilichunguza Kila sehemu alizoenda lakini hakuna sehemu nilipoona akiwa na mwanamke, nilichunguza kila mwanamke aliyeongea nae ndani ya Gari lakini sikuiona picha yoyote ya mwanamke ndipo akili zangu zikapata mwanga💡 niligundua Kuna sehemu alizoea kwenda, nikafurahia na kuhapo naweza kupata kufahamu wowote kuhusu mwanamke aliyezaa na Mume wangu Dylani.
'Njia ya Pugu Sekondari Barabara ya Majohe karibu na kituo cha Mjomba Kuna Pub imeandika Paris Pub. Nyumba nambari mbili.' Nilisoma Direction ndani ya ile kamera. Hapo ndipo Dylan upendelea kwenda zaidi ya mara mia.
Nikamchukua Alicia tukapakia ndani ya Prado Gari yangu mie Bosy Lady tukatoka pale Oysterbay pahali ninapoishi nyumba yangu mwenyewe na Safari ya kwenda Gogolamboto njia ya Majohe iliwadia.Tulifika Paris Pub, nikachunguza chunguza niipate nyumba nambari tatu bahati nzuri nikaiona.
'Ngoo ngoo ngoo' Nikiwa nimembeba Alicia mgongoni nikabisha lango, halikufunguliwa na aliyefungua alikua ni yule yule Mbibi niliyekutana naye makaburini, yule Mbibi aliye to seenidhiria mtoto akamtekeleza na kupotea kama mchawi.
"Jesu!" Alishituka. Aliponiona.
"Umekuja kuniadhibu mie mwanamke mzee nisiye na nguvu za kumlea mtoto wa mpangaji aliyefariki miezi Saba iliyopita." Aliongea machozi yakimtoka.
"Mpangaji." Mpangaji aliyefariki ndie aliyezaa na Mume wangu?" Nilijikuta nauliza lakini hakunijibu ila akatamka maneno yafuatayo
"Kwanini usiondoke na huyo mtoto ukamlea jamani mie kizee nitapata wapi nguvu za kunywesha uji na maziwa, nitapata wapi nguvu za kumfulia au kumbadilisha pampasi? Miguu yangu imechoka kwenda Clinick, jamani Marehemu Zuhura kwanini unaniadhibu mimi." Alilalamika na kumwaga chozi akitazama juu mbinguni.
"Zuhura!? Zuhura Ambrose au Zuhura nani?" Nilijikuta nauliza.
"Ndio, Zuhura Ambrose. Je wamjua?" yule Bibi aliacha kulia akauliza.
"Embu tuingie ndani tuyajadili yamkini ninaweza kupata picha juu ya huyu Zuhura na Mume wangu Dylani. Nilimwomba yule kibibi tukaingia ndani na kuketu sebuleni, akaniandalia Kahawa na vipande vya karanga taratibu maongezi yakapamba moto
""""""""""""""""""
"Huyu ndiye Zuhura mpangaji wangu akiwa na mwanaume aliyezaa nae." Yule Bibi aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Cesilia alinionesha photo moja kubwa aliyopiga mume wangu pamoja na Zuhura Ambrose. Nilipoitazama almanusura nidondoke na kuzirai.
"Yupo wapi huyo Zuhura?" Nilimuuliza yule Mbibi.
"Alifariki miezi Sita iliyopita. Alifariki kwa msongo wa mawazo. Mara baada ya kupewa taarifa juu ya kifo cha hawara yake Bwana Dylan. Kuja nyumbani kwako nilibahatisha tu ila ukweli ni kwamba Zuhura na Dylan walikua ni wasiri sana. Hawakutaka habari zao mtu azijue. Bibi Cesilia aliongea.
"Naomba unieleze jinsi unavyomjua Zuhura." Bibi Cesilia aliongea. Nikayapangusa machozi yaliyonibubujika kama kisima kisha nikaanza kumsimulia Bibi kisa na mkasa kuanzia pale nilipomjua Dylan hadi siku ile nimemwaribia Shoga yangu Zuhura mipango yake
"Mume wangu Dylan alikua ni aina ya wanaume wanaojua kupenda hata mwanamke asimuache, mwanaume anayejua kubembeleza mwanamke akabembelezeka. Mcheshi, mpole,mwenye huruma." Nilianza kumsifia marehemu Mume wangu Dylan.
"Mimi na Dylan tulikutana Chuo kikuu Dar es salaam kampasi ya Mlimani. Tulipendana sana, tukitoka usiku kula Dinner, tukienda beach, kumbi za burudani kucheza dance kumbi za sinema na....." Machozi yalinitoka nilipovuta kumbukumbu.
"Tulikubaliana ndoa mara baada ya kumaliza Chuo lakini mwaka wa tatu wa masomo yetu Dylan alikuja Hosteli na kunipa Taarifa zilizouvunja💔 moyo wangu
'Dorka listen me carefully nimepata mpenzi mpya anaitwa Zuhura. Asante kwa mapenzi yako na muda wako naomba tuachane tu." Aliongea hivyo.
"What do you say... Nini?" Nilikua nafunga vifungo vya gauni langu lakini vifungo vikanikataa na gauni likanipwerepeta.
"Ndo hivyo Dorka sitaweza kuendeleza na wewe naomba penzi lifikie tamati"
"Haiwezekani Dylan, haiwezekani mimi na wewe tumekubaliana Ndoa mara baada ya kumaliza Chuo Sasa kwanini unitende hivyo?" Nililalamika kulilinda penzi langu.
"Nimempenda Zuu Ambrose, ameingia moyoni mwangu, naomba ukae kando." Aliongea kama vile hayajui mapenzi ya kuachwa yanavyoumiza.
"siwezi, tafadhali siwezi Dylan, siwezi Daring Bado ninakupenda mimi tena ninakuhitaji kivile." Nilimpigia kelele.
"Kelele zako ni kelele za kumpigia Mbuzi gitaa acheze Muziki. Nmesema penzi letu lifikie tamati. Dylan aliondoka ndani ya chumba changu Cha Hostel.
"Dylan ..... Dylan ...... Daylan....." Nilimkimbilia nikiwa uchi mtupu hata nisiogope walionitazama wakinishangaa lakini Dylan hakunisikiliza zaidi ya kuondoka kurejea kwa Zuhura Ambrose
********
Kama alivyosema haitaji kampani yangu, Dylan alimaanisha haniitaji kuanzia siku ile Dylan alianza kuambatana na Zuu wakinionesha mahaba yao hadi basi! Mie mwenzao wivu na uchungu wa kuachwa ukiniumiza sana. Nikageuka kilizi nikililia penzi lililonikataa, nikakonda na kudhoofu, masomo yalikua magumu na yasiyotamanika. Ajabu penzi la Zuu Ambrose na Dylan lilizidi kuchepua.
Kila kituko kisa na mkasa niliwafanyia ilimradi tu waachane lakini wapi! Hawakuachana, niliwai kukodisha mwanamke wa mchongo ili kumteka kihisia Dylan ili Zuu apate wivu lakini wapi! Mchogo ulibuma. Niliwakodisha na kuwalipa mashababi wenye sura safi na miili ya vyuma ili wamtongoze Zuu lakini wapi! Haikuzaa matunda.
Nikaenda kwa wanganga na wachawi ili wamroge Zuu aachane na Dylan wangu lakini wapi! Sikufua ndafu dawa za wanganga na wachawi hazikuzaa matunda. Mbona hata kwa Apostle Mwamposa kununua mafuta ya upako niliwai kwenda ili kuliombea penzi la Zuu na Dylan lianguke na kumeguka vipande vipande ili mie nirudiane na Dylan wangu ajabu kama nilikosea vile penzi lao lilizidi kustawi na kupendeza. Hatimaye pesa nyingi zilipotea, muda mwingi ulinipotea, akili na maarifa yalinikimbia.
Basi nikapata wazo, yamkini wazo langu lingenisaidia. Asubuhi Moja nilidamka Hostel kabla ya kunywa au kupiga kifungua kinywa nikaenda Domintory anayolala Dylan bahati nzuri nilimkuta akijipa zoezi🏋️♀️ la kuruka kamba ili kuuweka mwili wake fit.
"Umefuata Nini huku Dorka? Nimekwambia achana na mimi sikutaki." Alinipigia kelele.
"Sawa najua haunitaki lakini je haumtaki hata mwanao tarajiwa." Niliongea kwa tabasamu la kumvuta nyoka kutoka pangoni.
"Mwanangu!?"⁉️ Aliuliza kwa mshangao.
"Ndio mwanao, kama haumtaki si useme ili nimtoe." Nilijifanya kumtisha.
"Ina maana Dorka una mimba!!!!!?*🫥😶🌫️🤔😱 Alizidi kushangaa
"Sasa kumbe?!" Unafikiri mimi ni Binti wa hasara kama Zuu anayekuchuna pesa zako Nikalikoleza.
"Usinitanie Dorka, tafadhali sema ukweli." Niliona furaha yake usoni ikichomoza moyoni nilianza kujipongeza maana niliona Sasa mwanaume ameanza kulainika.
"Nikudanganye wewe kama nani? Ni lini nimetamka uongo kwako Dylan? Sikiliza Dylan nakupa sharti Moja kama kweli unataka kuitwa Baba tafadhali rudi kwangu tuitunze na kuilea mimba yetu mtoto azaliwe. Kama hautaki kuitwa Baba niambie nikaitoe hii mimba ili nikuachie uhuru wako wako wa kuponda starehe pamoja na mpumbavu wako Zuu." Nilibwata.
"Hapana Dorka naomba usiitoe hiyo mimba nipo tayari na pia ninatamani kuitwa Baba." Dylan akanisogelea na kunikumbata kumbato nililolimiss muda mrefu mapenzini.
"Achana na tena mfute Zuu kuanzia Leo." Nilimuonya
"Lazima niachane nae mama wa watoto wangu." Alinikumbata zaidi.
"Vipi kuhusu mipango yetu ya ndoa." Nilimkumbusha.
"Kabla sijajifungua mtoto Ninahaitaji ndoa." Nilideka kwake.
"Ndoa ipo Daring hata kama ukihitaji Leo nipo tayari kumwita
Padre atufungashe ndoa." Alipoa na kulainika kama barafu Juani.
""""""""""""
Zuu Ambrose aliposikia ati mie na Dylan tumerudiana Alifura kwa mahasira hasara, alimwaga chozi na kupoteza tumaini la kumpatia Dylan wangu. Msongo wa mawazo ulimkamata alitamani kujiua kwa kujinyonga (Mie huku na mimba yangu bandia tukicheka kwa furaha.😆😂.) Wazazi wake Zuu wakaingia hofu na wasiwasi juu ya Binti yao kipenzi haraka wakafanya kuhamia Nairobi Kenya huko Zuu akatulia na kiyashikilia masomo.
""""""""""
Mie na Sweet Dylan tukafunga ndoa yetu ndani ya kabisa la mtakatifu Cuthbert mahaba yakarejea tena. Basi kila siku asubuhi Dorka mie nikawa mtu wa kujifanya natapika ovyo ovyo, nalilia kula embe mbichi na ndimu, nalala lala makusudi, nabagua vyakula na kudeka kwa sana Deko ambazo Dylan mpenzi wangu alizikoreza zikakorea na kwa jinsi anavyoyajua na kuyaweza mapenzi eeh!😅🥰 Nijimiminie mie.
Waswahili wanasema mimba haifichiki na kitanda hakizai haramu, wengine wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha .Hofu ya kugundulika kuwa ninadanganya ulinisumbua yaani ipo siku yakimwagika hayazileki,io siku mwenye mtoto wa bandia akija kugundua kuwa Sina mimba napachika matambaa tumboni basi nitumbuka mie.😅😅
Nikamuaga mpenzi Dylan 'Babu ninakwea Hospitali' nilipofika Hospitali nikampanga Dakta wangu, pesa sabuni ya roho, 💰Dakta akapokea sabuni ya roho mate yakimwagika kama Zombie mpango wetu ukatick. Dylan akapigiwa simu 'Please, haraka njoo Hospital,' Akafanya hima akanikuta nimelazwa juu ya kitanda Cha Hospital, damu na maji naongezewa.
"Pole sana bwana Dylan mimba ya mkeo imechoropoka kabla ya wakati wake ni kwa sababu alianguka pindi anapanda ngazi za kupandia Hospital." Dakta Mpenda pesa aliongea.
"Duh! Pole sana mke wangu Dorka, Mungu amepanga iwe hivyo na Mola atapanga mema yatufuate."Mume wangu aliongea chozi likitamani kuanguka.
"Asante sana Mume wangu nilitamani sana kumleta mwanetu afurahi pamoja na sisi lakini imekua hivyo tena" Nililazimisha kulia machozi ya kinafik yalinitoka.
"Usilie Daring ninakupenda sana Docka wangu." Mume wangu alinifuta machozi, uongo na mchongo ulifauru. Tukarudi Hostel kuendeleza masomo hata baada ya masomo tulipata ajira. Miaka nenda miaka rudi sikubahatika kushika mimba lakini Bado Dylan alinipenda sana hakuonesha Darili za kunicheat au kupenda mwanamke mwingine zaidi ya mimi.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Nikamaliza kumsimulia Bibi Cesilia ile simulizi ya wivu wa mapenzi. Bibi alishangaa kukisikia kile kisa hata yeye poa hakujus vip Dylan na Zuhura walivyokutana zaidi ya kumuona Dylan akija mara kwa mara pahali anapoishi Zuhura.
Niliondoka nyumbani kwa Bibi Cesilia nikarejea Oysterbay nyumbani kwangu nikiwa na Alicia mwanangu ambaye nilijiapia kumtunza, kumlea na kumpatia mahitaji yake yote.
Moyoni nilijiona Nina majuto na hatia kwanza nililiharibu penzi la Dylan na Zuhura waliopendana sababu mie sikupendwa pia sikujua mipango yake Mola juu ya maisha yangu. Pili, katika miaka yote niliyoishi na Dylani sikupata kushika mimba sembuse kulea mtoto wa kusingizia kutokana na uongo wangu nimeponzeka.😢
Dylan amekufa kwa sababu ya ajari na Zuhura kutokana na msongo wa mawazo ya kumpenda Dylan baya zaidi nimeachiwa mtoto yatima wajibu wangu kumlea kama mwanangu. Nina imani Zuhura atanisamehe huko aliko.
MIAKA KUMI NA SABA BAADAE
Alicia mwanangu akawa ni mtu mzima Sasa, mtu mzima mwenye kumi na nane zake. Siku moja nilimwita sebuleni nikamweleza kisa chote na mkasa juu ya maisha yangu, Mamaye Zuhura na marehemu Dylan mume wangu. Mwanangu Alicia hakuumia Wala kusikitika alipojua kuwa mie sio mama yake, alichonena yeye alisema:
Ananipenda mimi kama mama yake mzazi haijalishi hata kama mie kwake ni Godmother kamwe hatoniacha zaidi ya kunipenda.
"Mama yangu umeitunza, umenilea na kunipatia kila kitu kwa upendo na mapenzi yako mimi nimekula vizuri, nimelala pazuri, nimedeka na kudekezwa. Ninakupenda sana na nitakupenda milele." Akanikumbatia na kunipiga mabusu shavuni mie nilikua huku ninalia kwa uchungu.😭
********
TCHAO
💞💕
********
No comments:
Post a Comment