love is all
Given and found,πΉ
love is all
Given and found,πΉ
Mapenzi Mema.
ππ
Natuijenge dunia, yenye mapenzi mema,
Dunia yenye ujamaa, mapenzi tuyape heshima.
Upendo uwe neema, msamaha pia rehema,
Pasina tumia gharama, tupendane daima.
pasina tumia gharama, tupendane daima,
Tuishi kwa kujituma, tuzipokee karama.
Mapenzi yetu yatavuma, tayabariki karima,
Matunda tutayachuma, furaha italindima,
Mioyo iwe bima, tuuzike uhasama,
Daima tukijinyima, mapenzi yawe salama,
Daima tukijinyima, mapenzi yawe salama,
Tunyime vile vya gharama, mapenzi yatalindima.
Mapenzi yajenge hema, shamba yapate kulima,
Yaipande mbegu njema, yavune Dhahabu njema,
Mapenzi yajenge boma, lidumu likadumika,
Liwe mfano wa Jua, giza litafunika,
Liwe mfano wa Jua, giza litafunika,
Mwanga utajikunjua, mabaya tutayazika,
Mwanga utajikunjua, mabaya tutayazika,
Mema tutayajua, mapenzi taimarika.
Mapenzi niliyawaza, machoni kuniangaza,
Mapenzi sijaona kiza, moyoni meng’anganiza,
Mapenzi menikimbiza, menishika menimeza,
Mapenzi yenye huruma, nimeyawaza siku zote.
Mapenzi niliyawaza, kwangu meyadunduliza,
Hakika yameshangaza, mema yameniongeza,
Mapenzi menitongoza, kwake yananiburuza,
Mapenzi menisogeza, raha yake naiwaza.
Mapenzi menitongoza, kwake yananiburuza,
Raha inaniunguza, joto la kwangu kupoza,
Nami ninayokoleza, kamwe sintayapoteza,
Kiapo changu apiza, mapenzi yanibembeleza.
chorus
Mapenzi sio utumwa, kama mnayodhania,
Mapenzi si kusukumwa, upigwe ukaumia,
Mapenzi ni ukulima, tunda nalitamania,
Mapenzi yenye heshima, hayo najimiminia.
Mengi menisaidia, mengi yamenivumia,
Mengi nimeyasikia, mengi yatanipatia,
Mengine meniwekea, hakiba isipotea,
Ndugu nitawagawia, kamwe sintawuzia.
Mapenzi meniusia, upendo kukazania,
Hilo nalitimizia, milele naliangalia,
Mvua inaamiminia, maua yalotulia,
Milele nitayawaza, milele tayatangaza.
Hukutendea haki mapenzi
πππππππππ
πππππππππ
πππππ’π₯ππ
Hukutendea haki mapenzi,
Mara uliponifukuza,
Ulisema nimekuudhi,
Moyo wako nimechukiza,
Mara ulinipigiza,
Thamnani ya langu chozi,
Lote umelikanyaga.
Hukutendea haaki mapenzi
Mara uliponitukana
Maneno yenye puuzi,
Mdomoni uliyapayuka
Siku nimekufania,
Chumbani ukibarizi,
Mwengine ukifurahia
Mwengine ukifurahia,
Zawadi njema mapenzi,
Mimi unaniuchukia,
Waniona jinamizi,
Mimi wanichukia,
Waniona kama mbuzi
Penzi ulininyimia.
Hukutendea haki mapenzi,
uliponifukuza,
Njiani nalimwaga chozi,
Dunia imeshanifunza,
Penzi lataka heshima,
Sio kwa mafarakano,
Ungelitumia hekima,
Sio kwa matukano
Chorus
Pesa zimekupa jeuri,
Zimekujengea kiburi,
Wanifanyia ukatiri,
Penzi lako kwangu ajari,
Tukae chini tujadili,
Mapenzi uombe msamaha
Kwanini ukunifikiri,
Moyoni ukanipuuza,
Hukutendea haki mapenzi,
Hukutendea haki.
SARAFINA π
Katika mji wa Soweto, Afrika ya kusini,
Binti mwenye mvuto, japo kuwa mutu duni,
Mapenzi yake vito, Dhahabu ing’aayo gizani,
Ninani huyo mrembo, Sarafina mwenye mapenzi.
Mandela angalipo jela, Amefungwa na makaburu,
Mapenzi mema yenye sera, za kuwapatia uhuru,
Afrika iwe moja dola, isiwe mwoga wa kunguru,
Kwa mtutu na amani, freedom freedom free
Sarafina mwenye mapenzi, wima akajasimama,
Kuwakusanya wanagenzi, chehe kuzitema,
Tuupinge ubaguzi,tukiepuke kiama,
Mauaji yenye majonzi,uonevu na hujuma,
Tuupinge ukandamizi, katika aridhi mama.
Free Mandela….. free Mandela, Free Mandela free at last,
Vita! Vita! Vita Afrika, Damu zikamwagika,
Na Mali zikaharibika, mateso yakaamka,
Vitisho vikatumika, hofu pamoja shaka,
Njaa isiyo na huruma, Afrika ikateseka.
Lakini twafurahi, JUHUDI MESHINDA kudura,
Afrika yaona fahari, kuachiwa kwa Mandela,
Uhuru sasa tayari, kongole nyingi hongera,
Sarafina mwenye mapenzi, ametuchangia mapenzi.
Sarafina mwenye mapenzi,mapenzi amechangia,
umekoma ubaguzi, uhuru kwa wote pia,
hakuna ukandamizi,Afrika yashangiria,
uishi maisha mema, Sarafina mwenye Mapenzi.
MAPENZI YA ZAMANI
mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa,
Bibi kumpenda babu, heshima kumtunzia,
Hakutokuwa sababu, ya babu kumwaibia,
Bibi kwa majabu, babu katulia,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa.
Mapenzi huko zamani, yalikuwa na heshima,
Nguo fupi na vimini, hakuna hizo zamani,
Ukitaka kuamini, waone wakiwa ndani,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa.
Vijana hawa wa sasa, hesima kwao jalaa,
Wakisha pata mapesa, hula mpaka kusaza,
Ukitaka kuwahasa, wanajitia waelewa,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa,,
Mke kutoka na huyu, mume kutoka na yule,
Kama tunda za ubuyu, utupwa hapa na pale,
Wanakua kama kuku, ukikosa mtama tele,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa.
Michepuko sio dili, shikeni hiyo kauli
Kwanza mvae akili, kutenda na kufikiri
Kama nyie majeuli ,wenzenu wamekithili,
Mapenzi huko zamani sio haya ya sasa
Uturi wa Zanzibari,
Hayo marashi asili,
Basi mapenzi pulizia.
Basi mapenzi pulizia,
kama maua kuvutia,
heri nazo kukujia.
Ewe mpenzi Tanzania
Kama ua wavutia,
Heri nazo kukujia.
Tena mpenzi we pendendeza,
Waone wenye kengeza,
Jinsi unavyokatiza.
Jifukizie uturi
Unukizie hu, mwili
Tena uende sanjari.
Tena uende sanjari,
Na mavazi ya Hariri,
Yenye rangi za Johari.
Yenye rangi ya Johari,
Hazichuji kama bahari
Machoni zina fahari.
Manukato ya Commoro
Mazuri yaso kasoro,
Uyapake unyoro.
Ndege watakuimbia,
Nyimbo zinazosifia,
Uzuri wako majaliwa.
Tuvuke twende ngazija,
Mapenzi kule yamejaa,
Tukaimbe kwa lahaja.
Mpenzi twende anjuani,
Mapenzi kule ni thamani,
Thamani ndani moyoni.
Penzi lako lanukia,
Wengi wannatamania,
Kamwe hawakupatia.
Basi mpenzi nukia,
Nisichoke kuangalia,
Nazo sifa kusifia.
Basi mpenzi nukia
Uvae taji dunia
Taji lake Malikia.
Taji lake Malkia,
Sasa utaabudiwa,
Mema nayo taambiwa.
Nyimbo tamu kukwimbia,
Harufu njema wasikia.
Kwako wakimbilia.
love is all Given and found,πΉ It's all around,π₯° It's hard to tell about,π Easy to show,π€© One sure thing when you feel it You kn...