Friday, March 13, 2026

I thought 'bout love πŸ’ž

 

                                                                                  

 

NILIYAWAZA MAPENZI





Mapenzi niliyawaza, machoni kuniangaza,

Mapenzi sijaona kiza, moyoni meng’anganiza,

Mapenzi menikimbiza, menishika menimeza,

Mapenzi yenye huruma, nimeyawaza siku zote.

 

Mapenzi niliyawaza, kwangu meyadunduliza,

Hakika yameshangaza, mema yameniongeza,

Mapenzi menitongoza, kwake yananiburuza,

Mapenzi menisogeza, raha yake naiwaza.

 

Mapenzi menitongoza, kwake yananiburuza,

Raha inaniunguza, joto la kwangu kupoza,

Nami ninayokoleza, kamwe sintayapoteza,

Kiapo changu apiza, mapenzi yanibembeleza.


chorus

Mapenzi sio utumwa, kama mnayodhania,

Mapenzi si kusukumwa, upigwe ukaumia,

Mapenzi ni ukulima, tunda nalitamania,

Mapenzi yenye heshima, hayo najimiminia.


 

Mengi menisaidia, mengi yamenivumia,

Mengi nimeyasikia, mengi yatanipatia,

Mengine meniwekea, hakiba isipotea,

Ndugu nitawagawia, kamwe sintawuzia.


Mapenzi meniusia, upendo kukazania,

Hilo nalitimizia, milele naliangalia,

Mvua inaamiminia, maua yalotulia,

Milele nitayawaza, milele tayatangaza.



 


No comments:

Post a Comment

Good love

  Mapenzi Mema. πŸ’–πŸ’– Natuijenge dunia, yenye mapenzi mema, Dunia yenye ujamaa, mapenzi tuyape heshima.   Upendo uwe neema, msamaha pia rehem...