MAPENZI YA ZAMANI
mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa,
Bibi kumpenda babu, heshima kumtunzia,
Hakutokuwa sababu, ya babu kumwaibia,
Bibi kwa majabu, babu katulia,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa.
Mapenzi huko zamani, yalikuwa na heshima,
Nguo fupi na vimini, hakuna hizo zamani,
Ukitaka kuamini, waone wakiwa ndani,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa.
Vijana hawa wa sasa, hesima kwao jalaa,
Wakisha pata mapesa, hula mpaka kusaza,
Ukitaka kuwahasa, wanajitia waelewa,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa,,
Mke kutoka na huyu, mume kutoka na yule,
Kama tunda za ubuyu, utupwa hapa na pale,
Wanakua kama kuku, ukikosa mtama tele,
Mapenzi huko zamani, sio haya ya sasa.
Michepuko sio dili, shikeni hiyo kauli
Kwanza mvae akili, kutenda na kufikiri
Kama nyie majeuli ,wenzenu wamekithili,
Mapenzi huko zamani sio haya ya sasa

No comments:
Post a Comment