OMBI LA KINGA.
SURA YA PILI
OMBI LA KIJINGA.
Ilipita miezi miwili, miezi ya ndoa yao, Happy aliukamata ujauzito, moyoni alikuwa na wingi wa furaha na raha tele, mumewe aliporejea nyumbani kutoka kazini akafanya hima hima kumweleza juu ya furaha iliyo moyoni mwake. Ilikuwa ni jioni moja tulivu, wawili hawa walikua na maongezi yao mara baada ya chakula Happness alianzisha maongezi.
“Mume wangu mpenzi leo nina taarifa njema ajabu.” Happy aliongea kwa furaha, akicheka cheka na kuichezea mikono ya mumewe.
“Taarifa gani hiyo mama.”Furaha alidadisi.
“Ndoa yetu imejibu, ningali nina ujauzito wa miezi miwili sasa.” Happy alitarajia mumewe angelionesha uso wa furaha lakini bila matarajio alishangazwa na mabadiliko aliyoyaonesha mumewe mpenzi. Sura yake ilijikunja, macho ya mumewe yakawa makali kama pilipili.
“What?!........ Nini?” Furaha aliuliza kwa ukali, happness alishangazwa na muitiko wa mumewe.
“ Mume wangu mbona unashanga au haujapendezwa na ujio wa taarifa hii njema?” Happy alimuuliza mumewe. Furaha aliyekuwa ametulia juu ya moja ya masofa mazuri ndani ya nyumba yao akanena:
“Sina maana hiyo, lakini mke wangu mbona mie sijajipanga kuitwa baba.” Furaha aliongea jibu lililomshangaza mkewe.
“Mume wangu haujajipanga kivipi wakati sie tuna kila kitu ndani na nje ya familia yetu!!?” Happness alimuuliza mumewe kwa mshangao mkuu.
“Mke wangu umri huu nilionao, umri wa miaka ishirini na minane ni umri ambao bado mimi ninapaswa kutafuta mali zaidi, tukiharakia kuwa na mtoto huyo mtoto atatusumbua.”
“kwa hiyo wewe unataka tufanye nini sasa? Wakati mie ninaujauzito wa miezi miwili.” Happness aliongea.
“Utanisamehe sana mke wangu kwa haya machache ninayotaka kuongea ninaomba ombi moja kwako, enenda ukautoe huo ujauzito.”
“What? Nikautoe ujauzito wangu? Hivi mume wangu una akili timamu wewe?”
“Utanisamehe mke wangu, sina nia au dhamira mbaya, kama ujuavyo tena hilo ni ombi langu.” Furaha aliongea, Happness alichukia. Zilipita siku tatu wawili hawa hawakuongea pamoja hawakula, hawakunywa wala kulala pamoja. Wakati furaha akimsistizia mkewe akautoe huo ujauzito kwa madai ati ajajipanga kumpokea Malaika mtarajiwa, Happness alitia mkazo hakutaka kuusikia upuuzi huo.
Ghafla upepo ukabadirika, Happness alibadiri nia, Ibilisi wa kutoa ujauzito alimwingia, aliona kuwa maombi ya mumewe ni bora zaidi kama ajuavyo yeye Binafsi ameolewa na bada ya kuolewa alipaswa kuheshimu mawazo ya mumewe. Alimpenda sana mumewe japo alisita sita kufanya kitendo kile kiovu, afanye nini jamani? Hana la kufanya roho yake ilimlazimu akubali na baada ya kukubali alimwambia mumewe yupo tayari kuutoa ule ujauzito.
Mume kusikia mkewe amekubali kuutoa ujauzito alifurahi sana, furaha iso na kifani, akamchukua mkewe ndani yamoja ya magari yake ya kifahari haraka akampeleka mkewe kwenye moja ya hosptali kubwa ndani ya jiji la Dar es saalam.
“Salamu Bwana Dakta, habari za kazi?” Furaha alimsabahi Dakta aliyemhitaji.
“Salamu bwana mdogo kazi yangu yaenda Vema, sijui nikusaidie nini?” Dakta alimuuliza Boss Furaha. Wakati huo wawili wale yaani Furaha na Happness walikuwa wapo ndani ya Ofisi ya Dakta. Dakta alikuwa na kiasi cha furaha usoni kwake, sababu alimjua vema Bwana furaha, ni miongoni mwa matajiri vijana ndani ya jiji la Dar e saalam. Basi Bwana Dakta alijiweka tayari kwa lolote lile jema la kumfaidisha.
“Bwana Dakta tumekuja mbele zako tuna tatizo, ni tatizo dogo sana, nina hitaji umflash mke wangu…..” Furaha hakumaliza sentensi yake. Alichukulia tendo la kutoa mimba kama jambo la kawaida sana.
“Una maanisha nimtoe Mimba?”
“Ndio bwana Dakta au mpaka sasa haujanielewa?”
“Ah! Hapana mkuu, lakini mkuu si unajua fika kuwa serikali inapiga vita utoaji mimba kwa wanawake na iwapo nikitenda hilo tendo ovu nitahatarisha ajira yangu, “ Dakta aliongea kwa miguno na wasi wasi.
“Sikiliza Dakta ninahitaji utende tendo hili uwezavyo, nitayaboresha maisha yako ukinisaidia.” Furaha alimshawishi Dakta.
“Lakini…………!” Dakta alionesha wasi wasi wake.
“Lakini nini bwana Dakta, embu tizama iwapo utanisaidia nitayaboresha maisha yako na wa kuyaboresha hayo maisha si mwingiune ni mimi.”
Dakta hakuwa na jinsi aliamua kula mlungula, alipokea rushwa ya pesa mingi, alikubali kutenda tendo la utoaji mimba, alikubali kumtoa mimba mwanamke yule, na baada ya kumtoa ujauzito alipewa chake, pesa mingi kweli, maisha yake yakawa bora na kuboreka.
Itaendelea sehemu ya 3
No comments:
Post a Comment