SURAYA TATU
“AKIPITA ATAJIPITISHA.”Beka akawa member wa kampuni ya SIGA, akipelekwa hapa na pale kulinda mali za makampuni, mashirika na taasisi mbali mbali, anahamishwa hapa na pale ili kuywajibikia koazi zake, anafanya kazi zake usiku na mchana, amerikamata bunduki yake mkononi, amevaa magwanda yake miguuni, ametinga mkanda waqke mmoja mzito kiunoni , haivui hiyo kofia yake inayompa heshima kichwaqni.
Beka ni mzuri tena ni mzuri sana, anawavutia hao wanaoiungia na kutoka ndani ya mjengoi nwa benki, lakini hata hivyo wanshindwa kumwambia namna gani wanavyomtamani kwa kuhofia ulinzi wake, ana uzuri waq sura inayowavutia wanawake wazungu pengine waafrika. Mara ile wanapoingia na kutoka kwenye majengo ya makampuni, mashirika taasisis nakadharika.
Uchapakazi wake, juhudi zake, uwezo wake wa kufanya kazi ni baadhi ya mambo yaliyomfanya bosi wake wa kampuni ya Siga, amfanyie uhamisho, amtoe Dar es salaam naq kumpeleka Zanzibar, Unguja ndani ya mji wa Kiwenga kufika hguko Beka akawa mlinzi wa mahoteli ya watalii, makampuni, mashirika pamoja na taasisis mbali mbali, alilipwa vizuri, japokuwa maliponaliyolipwa hayakuwa makubwa sana, kiasi cha mboga, na kipindi hicho Beka hakuwa na mahali pa kuishi ‘Getto’ alilala kwenye moja ya nyumba za Bosi wake Yule mwenye kampuni ya SIGA angali bado hajaanza kujitegemea.
Hatari ya kupendwa, alipendwa na wengi, hatari ya kulia aliliwa na wengi, Haki! Macho uangaza na macho utambaza, moyo utamani na kutamania, mwili ukumbata na kukumbatia mapenzi nni hisia naq hisia hutoka moyoni, wanawake hawakukoma kumtafuta Beka, wazungu na watalii mbali mbali walipomwona Beka hawakusita kumfuata ili awapatie furaha yao ya moyo.
Uzuri wa Zanzibar ni kwamba mji huo unawavutia sana watalii wengi wanaokuja Holiday, kujipumzisha mZanzibar inakuwa ni kijiji cha watalii uhuru wa watalii ndani ya Zanzibar ni mkubwa sana, furaha yao inayoambatana na anasa ni kubwa sana, watalii hao uja na vitu vya bei gharama, watalii ununua vitu ndani ya Tanzania, kwa bei gharama, hawalalami hujuma zinazofanywa na wenyeji wao bnali wanaongeza furaha ya kuwepo Zanzibar. Zanzibar ni kisiwa cha amani kama mchanga wa bahari, Zanzibar imejaa utulivu mapenzi mahaba na upendo wa hali ya juu.
Mandhari ya Tanzania Zanzibar yana mvuto wa hali ya juu upepo mwanana unaovuma na kukifunika kisiwa cha Unguja, ndege uimba na kukisifu kisiwa kizuri kama mbingu iliyojengwa Macka. Watanzania wanaoishi Zanzibar ni wapole ajabu wema ajabu, nwakarimu na wenye huruma nyingi, sifa hizi zinaifanya Tanzania Zanzibar iwe kimbilio la wageni wengi kutoka mataifa mbali mbali.
UZURI WA Tanzania Zanzibar ni nchi iliyo na siasa safi, ulinzi na usalama wa kutosha, kuna miundo mbinu bora, kuna majengo na mahoteli yenye hadhi na heshima, huduma mbali mbali za kijamii inaifanya Tanzania Zanzibar iwe kivuto cha mataifa ya wareno,waarabu, wachina, wafilipino, wamarikani, whindi na mataifa mengine mengi.
##############################
***************************
Huyu msichana aitwaye Bella ameuteka moyo wa Beka, unajua Beka ana historia ya kupendwa,yeye binafsi hana mazoea ya kupenda bali anapendwa na kila jicho tamu la mwanamke, analiliwana na kugombaniwa, hana mazoea ya kulilia au kugombania, anajikuta anashangaa jinsi anavyofuatwa na watoto wa kike.haki! ana nyota ya bahati lakini leo anamwona huyu msichana aitwaye Bella Beka anavutiwa na huyu msichana anajaribu kuvuta picha amwambie jinsi gani anavyompenda huyu binti. Sura ya Beka ni mtaji wake,anajua hilo anajua kuwa sura alyonayo ni mvuto kw watoto wa kike Beka anajisemea moyoni “ Silazi damu, ushindi daima, akipita aatajipitisha.”
“Akipita atajipitisha.” Hii ni kauri ya Beka ameiweka moyoni anajiaminisha kuwa Bella akijipitisha ATAMTTIZAMA KWA MUDA MREFU UVUMILIVU UKIMSHINDA ATAMWELEZA Beka Jinsi anavyojisikia.
Duh! Kumbe ni kweli akipitaatajipitisha, mawazo ya Beka yalikuwa Postive, sura yake ndio mtaji wake, japo ni masikini lakini hajali sababu umasikini na utajiri ni mali ya Mungu, Mungu akikupa , asipokupa wajibu wako ni kumshukuru yawezekana kesho au kesho kutwa (leo pia) atakuongeza (kilicho bora zaidi ya ulicho nacho sasa. Riziki hutoka mikononi mwa mungu haki ya binadamu kupokea, upewe ,usipewe wewe shukuru. Akiokota mwenzio leo wewe usilale lango wazi jitume, jibidishe, fanya kutafuta utapata tu tena utapata zaidi ya kupata.
Kumbe, kumbe Bella ni miongoni mwa walemabinti warembo waliomtamani Beka, tusiende mbali wacha tumchambue chambue huyu Bella jinsi alivyo kiumbe majaliwa. Ni mweusi tena mweusi sana, mfupi hivi, mwembamba kiasi ana hips don’t lie’ kama vijana wanavbyopenda kuita , wimbo maarufu wa wa Shakira mwanadada wa kiamerika. Miguu na mikono yake Bella imekonda na kudhoofika.
Alizaliwa Mbeya, Mbeya mjini. Ujio wake Zanzibar ni wa Bahati, alifika Dar es salaam akiokea Mbeya mara ile amepewataarifa kuwa kuna kazi ndani ya kiwanda kimoja kikubwa ndani ya jiji la Dar es salaam. Ile anafika ndani ya Jiji la dare s alaam binti akaambia ‘Work is over now’ ‘NO JOB, HAKUNA KAZI’ ‘TAADHARI MBWA MKALI HAPA’ ‘KAZI ZIMEJAA’.oooshit! akapumua kwa hasira, si aliambiwa kuwa kuna nafsi tele za kazi ndani ya kwanda hicho.amepoteza muda amepoteza pesa amepoteza kila kitu.
Any way, uppo ukabadirishwa na Yule mmiliki wa kiwanda akamwita pembeni Bella akamnong’oneza akamwambia kama sio mbaya mapatie kazi za ndani, kulea motto anayenyonya na kunywa uji,, ashinde na motto, amdekez dekeze,, ampendelee pendelee. Bella hakukubali, hakuwa tayari aliona bora kufa maiskini kuliko hujuma, ulaghai na kujidharilisha. Awali ya yote mwenye kiwanda alifanya kutangaza kuwa kazi ndani ya kiwnda zimejaa tele inakuwaje Bella aingie mjini na kuambiwa ‘NO JOB! KAZI ZIMEJAA.” Duh! Bella alihisi anahujumiwa.
”Akha, mie sipo trayari kufanya kazi za kulea makinda yako mama, mie nilijua kuwa nimeletwa ndani ya jiji la Dar es salaam kufanya kazi niipendayo kumbe nahujumiwa, naambiwa niwe House Girl nioshe visepe vya watoto, niwakoroge uji nitumwe hapa na pale, kwa kweli mama utanisamehe hiyo kazi mie siiwezi.”
siku iliyofuata Bella akampigia Simu mamaye mdogo anayeishi ZENJI, ndani ya kijiji cha Kiwenga. Simu ilipokelewa na kujibiwa vizuri, Karibu mwana karibu Zenji, karibu kwetu , karibu uje ule samaki wa kila aina karibu uje uyaone maajabu ya Munguy aliyowajalia wazenji kabla ya ukoloni, baada ya ukoloni hata uhuru.” Bi. Mdogo aliongea kwenye simu Bella akapanda meli ikatua Zenji mamaye mdogo akampokea kwa furaha.
Bi. Mdogo alikuwa anajishughurisha na shughuri ndogo ndogo za kushonaa itambaa alivyouza na kununuliwa na wataliikwake pesa haikuwa tatizo, pesa ilikuwa nje nje, walikula walikunywa akiba ilisaza na uzuri wa Bella sio mvivu alijitolea kumsaidia mamaye mdogo kazi za kuingiz kipato.
Bella ndiye mpishi, mpishi wa nyumba ya Bi. Mdogo, Bella ndiye mmwenda sokoni kununua mahitaji mbali mbali ya kifamilia. Akipita pale Sultan Hotel mach yake yanaagaza huku na kule yapate kutua kwenye sura nzuri ya huyu Chotara aitwaye Beka, Chotara anayemtamanisha moyo, Chotara anayemfanya binti akose usingizi Chotara anayempa mawazo huyu binti, mmh! Chotara mashallah! Mzuri ajabu, kumbe Bella akijaliwa watoto Chotara atafurahi sana, kumbe watoto Chotara ni wazuri sana, duh! Wanamvuto, ndio maana Beka anavutia.

No comments:
Post a Comment